KWELI Manchester City wamtaka Bukayo Saka kuelekea msimu mpya wa EPL mwaka 2022/23

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Inadaiwa Klabu ya Manchester City imeongeza jitihada za kutaka kumsajili nyota wa Klabu ya Arsenal na timu ya Taifa ya England, Bukayo Saka.


1657964991611.png
 
Tunachokijua
Mabingwa hao wa England wanafuatilia kwa karibu mustakabali wa Saka katika Klabu ya Arsenal ambapo amebakiza miaka miwili katika mkataba wake.

Kocha wa Arsenal ya London Mikel Arteta amekuwa na wasiwasi ya kuikosa huduma ya winga huyo kutokana na Bukayo Saka kutamani kucheza UEFA ambapo Manchester city tayari ameshafuzu kucheza mashindano hayo na Arsenal wameshindwa kufuzu. Ambapo klabu hiyo imempa mkataba wa miaka miwili kwa kumuongezea mshahara na kumuhaidi kuanza kikosi cha kwanza msimu wa 2022/23.

Arteta aliweka wazi kwamba klabu haina mpango wa kuuza wachezaji kwakuwa bado anaijenga timu baada ya kudondoka kwa mda mrefu na wachezaji waliokuwepo hawawezi kuuzwa labda kuongeza usajili ili kufanikisha kufika kwenye malengo walio tarajia ikiwemo kumaliza kwenye nafasi nne za mwanzo ili kufuzu kombe la mabingwa wa Ulaya 2023.

Hata hivyo, hadi mwishoni mwa dirisha la usajili, Bukayo Saka aliendelea kusalia kwa washika Bunduki hao wa jiji la London.

Bukayo Ayoyinka Temidayo Saka alizaliwa Uingereza mnamo Septemba 5, 2001. Hucheza kama winga wa kulia kwenye Klabu ya Arsenal na timu ya Taifa ya Uingereza . Anachukuliwa kuwa mmoja wa wachezaji bora wachanga ulimwenguni.

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom