Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,408
33,285
12994408_860160067463388_2945698542477474622_n.jpg


MAMBO 17 YALIYOSABABISHA KUUAWA KWA GADAFFI

1. LIBYA kulikuwa hakuna bili ya umeme, means umeme ulikuwa bure kwa raia wote
2. Libya kulikuwa hakuna Riba kwenye mikopo, Benk zote Libya zilikuwa za Umma na mikopo ilitolewa kwa raia wote tena bila Riba.
3. Gadafi alisisitiza kwamba, wazazi wake hawatapata nyumba nzuri hadi raia wote wa Libya wawe na makazi. Baba mzazi wa Gadafi amefariki wakati, yeye, mke wake na mama yake wakiishi kwenye hema.
4. Kila mfanyakazi Mpya (Mwajiriwa mpya) nchini Libya alipewa Dola za kimarekani 50,000 ili aanzie maisha.
5. Kabla ya Gadafi, kulikuwa na 25% tu ya raia wa Libya ndio walikuwa na Elimu.
6. Elimu na Huduma za Afya (matibabu) nchini LIBYA zilitolewa bure.
7. Kama Mwananchi wa LIBYA aliyehitaji kujishughulisha na kilimo, alipatiwa ardhi, nyumba, mbegu na mahitaji mengine yaliyohitajika.
8. Iwapo mwananchi wa Libya akishindwa kupata Elimu au Huduma ya Afya ndani ya LIBYA, serikali ilimsafirisha nje ya nchi kwa ajili ya mahitaji hayo, pia alipewa Dola milioni 3 za kimarekani kwa ajili ya gharama .
9. LIBYA, Kila raia wa LIBYA aliyenunua gari, serikali ilimwongezea nusu ya bei ya gari, means kama gari itauzwa sh milioni tano, basi raia alilipia shilingi milioni mili na laki tano na kiasi kingine kinalipwa na serikali.
10. Bei ya Petrol nchini LIBYA ilikuwa ni Dola za kimarekani 0.14
11. Libya ilikuwa haina madeni ya Nje, ilikuwa haidaiwi na nchi yoyote na ilikuwa imehifadhi dola za kimarekani bilioni 150
12. Kila mwananchi wa Libya aliyekosa ajira baada ya kuhitimu kulingana na kiwango alichofikia, Serikali ilimlipa mshahara unaokaribiana na mtu aliyeajiriwa mwenye elimu sawa na aliyonayo yeye.
13. Sehemu ya mauzo ya mafuta nchini Libya ilipelekwa moja kwa moja kwenye akaunti za benki za kila raia wa LIBYA
14. Kila mwanamke aliyejifungua, alipewa Dola za kimarekani 5,000
15. Gharama ya mikate arobaini ilikuwa ni Dola za kimarekani 0.15
16. 25% ya raia wa LBYA walikuwa na kiwango cha Elimu cha SHAHADA (a university degree)
17. GADAFFI aliaanzisha mradi mkubwa zaidi kuwai kutokea duniani, mradi wa Umwagiliaji uliojulikana kama MAN- MADE RIVER PROJECT, Mradi uliowezesha upatikanaji wa maji eneo zima la jangwa.
Kama huu uliitwa “UDIKTETA” Basi WANADEMOCRASIA wote watakwenda Motoni
 
Ni Gaddafi sio Gadaffi.
Gaddafi ameuawa kwa sababu moja tu, ujinga na kutokuwepo kwa umoja wa nchi za Afrika, unafiki,ubinafsi, uoga na uzandiki wa nchi za Kiafrika. Walikuwa na uwezo wa kuungana na kumkingia kifua lakini walishindwa.

Kama sababu za kifo chake ni kuwa mzalendo wa nchi yake basi hakuna nchi Afrika itaendelea.
 
Mwandishi amejitekenya na kucheka mwenyewe.

Yaani uongo kwa miaka hii hauna nafasi kama miaka walau kumi iliyo pita.

Jamii za sasa diniani zina hoji zaidi,zinadadisi mambo,zina uliza maswa kwa kina ili kujua mambo kwa kina zaidi .

Hivyo Unge andika hata madhaifu matatu tu ya Gadafi ili ijulikane kuwa ndiyo sababu za wazungu kuoenyeza chuki kati ya wananchi wa Libya na Rais wao.
 
Kilichomuua gadafi ni kusapoti waasi, magaidi na kujifanya anasambaza dini ya mood. vingine vyote hivyo hazikuwa sababu za msingi. na cha kuongezea hapo, hata kama aliwapa kila kitu ila aliwafumba mdomo yeye akijitajirisha kwa mabilioni ya dola na kuua sana watu.

ukimtaja gadafi kumbuka ugaidi wa kwenye ndege, kiburi dhidi ya wamagaribi, usaidizi wake viza Niger na Chad na Sudan, usaidizi wake vita ya Idi amin daada dhidi ya Tanzania na mengine mengi. na alijiita yeye ndio mfalme wa africa. kibri ndio kilimteketeza.
 
Iwapo mwananchi wa Libya akishindwa kupata Elimu au Huduma ya Afya ndani ya LIBYA, serikali ilimsafirisha nje ya nchi kwa ajili ya mahitaji hayo, pia alipewa Dola milioni 300 za kimarekane kwa ajili ya gharama .
Ndugu muandishi hapa umetupiga na kitu kizito cha utosi.

Huyo mgonjwa anapewa pesa zote hizo ili akanunue uhai mwingine au kujenga hospitali kabisa?? Unajua hasa thamani ya $300 million??
 
Wazungu hawawezi kukubali watu kama kina gadafi, Saddam waishi.... Maana watawasanua kua tunaweza sana tukiamua bila wao, mbona kina Singapore wakianza taratibu sa hivi wanajitegemea.....

Watu kama kina magufuli mzungu hawezi ruhusu wawepo, kwasababu tunatumia internet zao uchwara tutaaminishwa ni magaidi na madikteta.....

Mzungu anapenda tuongozwe na Hawa kina air attendant ambao hawaelewi a wala b
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom