Mama Mzazi wa Erick Kabendera amuomba Rais Magufuli kumsamehe mwanae

Kabendera anakabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la utakatishaji za zaidi ya Sh173 milioni na tayari amemuandikia barua mkurugenzi wa mashtaka (DPP) kukiri makosa na kuomba msamaha. Oktoba Mosi , 2019 kupitia wakili wake Jebra Kambole, alimuomba msamaha Rais Magufuli kama kuna makosa ameyafanya.




View attachment 1291137



Tatizo linaanzia hapo. Unakiri kosa halafu unasema "kama lipo kosa nililofanya"

Alipaswa akiri jumla jumla

Ndio tulipofikia hapo. Pole mama Kaflag
 
Hayo mambo ya laana kuna watu hawayafikirii aise! Muhimu ni kutii mamlaka na kujiepusha kushindania na wenye mamlaka vinginevyo mnyonge utaishia kuumia

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa mamlaka upo waikati bado hajahukumiwa. Upelelezi hauishi. Hivi unanikamata na issue ya money laundry unajiridhisha kuwa unanipeleka mahakamani bado upelelezi unachukuwa zaidi ya two years hata kama umekosa sasa unakuwa ni uonevu kwa kweli.Mahakama na mamlaka zijitafakari haingii akilini kesi zinachukua miaka na miaka
 
Mtukufu Rais dokta muweza wa yote na asieshindwa kwa lolote. Alisema tutalimia meno na tutaishi kama MASHETANI. Yametimia ..AMEEN!
Tulianza kwa kumpongeza na kumshukuru na sasa tunamuomba..! Kumsujidia na kumuabudu ... AMEEN..!
 
Kama mashtaka ni ya kupikwa,kuna mtu atakula laana

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahaha laana! Huyu kabendera alipokamatwa alivitumia vyombo vya habari kuichafua inchi kuwa amekamatwa kwa sababu ya kuandika taarifa za kiuchunguzi, alivyoonyeshwa makosa yake ndipo alipougua nakukondagafra!

Huyu kijana alikuwa ktk makundi hatari yakuhujum na kufadhiri magenge hatari sana kwa usarama wa nchi. Na mama yake pamoja na uzee wake lakini hajatumia Busara za uzee kuongea au kumwombea nwanae msamaha hata waliorusha hiyo clip nikama wamemuharibia tu.au wangemshauri maneno yakuongea.

Bora angemalizia kwakusema akitoka nitamuonya km mzazi. Nasi kwamba asamehewe aje amlee km mh raisi anavyolea wazazi wake. Hii anamuweka raisi ktk kundi moja na mwanae. Hajui km mwanae alihatarisha usarama wa watanzania zaidi ya mil.50
 
Hiyo attachment hAifunguki... nataka kujua hao waandishi kuongea na huyo mama ilikuwa planned au coincidentally tu maana isije ikawa ni seeking for the sympathy

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Changanya dua za wafungwa elfu tano na ushee +ndugu na jamaa za wafungwa,ukipata jumla yake,kaanayo

Kisha laana huyo bibi na kijana wake msaliti wa taifa upime mzani .
Kosa alilofanya huyu dogo kwa taifa hili alistahili kunyongwa,sema Magufuli anahuruma sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Kweli kabisa mkuu. Huyu kijana angekuwa yupo china asingekuwepo saivi
 
Verdiana Mjwahuzi (81) ambaye ni mama wa mwandishi wa habari, Erick Kabendera amemuomba Rais wa Tanzania, John Magufuli kumsamehe mwanaye.

Akizungumza kwa huzuni leo Ijumaa Desemba 13, 2019 katika mkutano na waandishi wa habari, Verdiana amesema Kabendera ni mwanaye pekee anayemsaidia katika matibabu.

Kabendera anakabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la utakatishaji za zaidi ya Sh173 milioni na tayari amemuandikia barua mkurugenzi wa mashtaka (DPP) kukiri makosa na kuomba msamaha.

Oktoba Mosi , 2019 kupitia wakili wake Jebra Kambole, alimuomba msamaha Rais Magufuli kama kuna makosa ameyafanya.

Verdiana amesema kati ya watoto wake wanane, Kabendera ni wa saba kuzaliwa na ndio alikuwa na uwezo wa kumtunza na kumuuguza.

"Mheshimiwa Rais na yeye ni mtoto kama walivyo watoto wengine hata kama ni mkubwa. Ni mzazi na analea watoto. Namwomba anionee huruma.”

"Angalia maisha yalivyo magumu, dawa sipati. Naomba Rais anisaidie kama anavyosaidia wazazi wake,” amesema.
Amesema mwanaye alijitahidi kuitunza familia yake, yeye na ndugu zake wengine na kusisitiza kuwa ndio mhimili wa familia

"Siwezi kumsifia mwanangu, wanaume wengi wakitoka kazini wanakwenda kulewa lakini Eric anafanya kazi zake hapa nyumbani hadi saa saba usiku na wakati mwingine hadi saa nane . Mambo yote aliyopata ni kwa sababu ya kufanya kazi," amesema mama huyo huku akibubujikwa machozi.

Ameongeza, “kule Segerea (gerezani) siwezi kwenda kwa sababu kuna msongamano wa watu, mahakamani kuna ngazi.

Lakini mara ya mwisho nilijitahidi nikaenda nilipomuona mwanangu sikulia, nilijikaza lakini chozi moja lilinitoka. Sikujua kama ni yeye, amekonda na ana nywele nyingi kama mwehu. Ni mweusi lakini amezidi kuwa mweusi.
"Huyu mtoto ni Mungu amenizawadia, ni tunu kwangu.

Akisikia mama anaumwa anakimbia haraka. Sasa hizo dawa sizipati tena, macho yalikuwa yanauma na moja halioni tena na hili linaloona naona vitu vyeusi."
 
Kwa huruma za mh rais naamini atamsikiliza huyu mama na kumsamehe mwanae. Tafadhali mheshimiwa kwa niaba nami namuombea msamaha maana nami najua uchungu wa mama kwa mwana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nashauri wale waliokuwa wakimshabikia Sasa wampatie msaada huyo Mama na Familia yake.
Wanaharakati Pamoja na Chadema kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom