Mkuu ndio mana kwenye comments zangu nyingi kwenye huu uzi nimerudia mara nyingi kusema sitamani vita.Very wrong! Takwimu hazina mikono na miguu kwenda na kupigana vita. Achana na vita. Nakumbuka wakati wa vita ya Tanzania na Uganda sisi tuishio ukanda wa ziwa licha ya kuwa ni mbali na mpakani tulikuwa hatuna amani. Hata ukiona jani linaelea majini unadhani ni bomu la adui. Tuliacha mikusanyiko na hata kwenda kwenye nyumba za ibada kwa kuhofia kushambuliwa na adui. On top of that, baadhi ya watu walifia kwenye mahandaki kwa kuumwa na nyoka. So, achana na kitu kinachoitwa vita - it's ugly na has neither friend nor relative!
Mimi sio muumini wa vita isiyo kua na lazma...sipendi vita kabisa. Hata pamoja na kwamba kitakwimu tuko superior...bado tutaumia na ni jambo la kuepukwa kwa nguvu zote.