SoC03 Makosa yetu ndio maradhi yetu, Afya ni mtaji

Stories of Change - 2023 Competition

KENGE 01

JF-Expert Member
Mar 12, 2021
1,597
3,860
MAKOSA YETU NDIO MARADHI YETU

UTANGULIZI

Wasomaji
Nawasalimu kwa jina la JMT,Kazi iendelee.

Kwanini nasema makosa yetu ndio maradhi yetu?Kwasababu makosa mengi tuyafanyayo kwa kujua au kutokujua ndio yanatuletea maradhi na Magonjwa.Jamii inawatu mbalimbali wanaoishi maisha ya kutofautiana hivyo kuna wachafu,Wasafi,Wakorofi,wastaarabu na tabia za kutofautiana.

Miili yetu imejengeka kwa ustadi na kufanya kazi kwa kipimo maalumu.Unapoambiwa usinywe pombe kupita kiasi elewa pombe inaathari mwilini.

Sasa tuangalie baadhi ya makosa tuyafanyayo kwa kujua au kutokujua yanayotusababishia magonjwa na maradhi;

1.Ulevi.
Ulevi wa pombe ni tabia waliojijengea watu kwa kujua au kutokujua madhara yake.Kunywa pombe kupita kiasi inaathari kubwa sana katika mwili na jamii
•Ulevi husababisha magonjwa sugu kama vile Maradhi ya moyo,Shinikizo la damu,Magonjwa ya figo,Mwili kupooza,Kansa ya koo,Neva na maradhi mengine mengi.

•Ulevi unashusha Heshima ya mhusika kwenye jamii

•Kupoteza marafiki na ndugu,kwasababu ya matendo uyafanyayo wakati unapokuwa umelewa
Alcoholism.jpg


2.Uzinzi.
Vitendo vya uzinzi vinazidi kuongezeka kila uchwao.Uzinzi ni hatari kwa husababisha magonjwa hatari sana.Ngono zembe ndio sababu kuu inayotajwa kusababisha magonjwa ya uzinzi.

•Ngono zembe husababisha maambukizi ya magonjwa sugu ya ngono kama kaswende,kisonono,UKIMWI na magonjwa mengine hatari.

•Uzinzi husababisha matukio hatari kama vile ubakaji na vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia.

•Uzinzi husababisha kudharaulika na kukosa heshima katika jamii.
STDs.png


3.Uvivu.

Kubweteka na kukaa bila kufanya mazoezi ni tabia nyingine watu wengi hujijengea,pengine kwa kujua au kutokujua madhara yake.Mwili unapokosa mazoezi ya kutosha husababisha damu kutosafiri vizuri hivyo kusababisha ongezeko la mafuta mwilini na matokeo yake ni unene na kukosa afya nzuri.

•Kukosa mazoezi husababisha magonjwa sugu kama unene kupita kiasi(Obesity),Maradhi ya moyo(High blood pressure,High cholesterol,Coronary artery disease)

•Kutouahughulisha mwili husababisha kupata maradhi mengi kiurahisi kwani mwili unadhoofika na kukosa uwezo wa kupambana na visababishi vya magonjwa.
Mazoezi.png



4.Kutozingatia mlo sahihi.

(Balanced diet)Kipato kinaweza kuwa ni sababu ya kukosa mlo stahiki.Lakini imekuwa ni tabia watu wamejijengea pengine kwa kujua au kutokujua madhara yake.

•Kula vyakula visivyofaa (junk food)vyakula vya kwenye kopo,Hivi vinakemikali ambazo zinaudhohofisha mwili

•Vinywaji venye sukari nyingi maarufu kama (soda na energy drink)pia vyaweza sababisha magonjwa ya kisukari(Duabetes type 2)
Energy drink.png



5.Kujichua.

Kujichua(punyeto) imesababisha vijana wengi kudhohofisha mwili na akili na kusababisha maradhi mengi mwilini.Hii inachangiwa na uwepo wa picha za ngono mtandaoni.

•Kujichua kuna athari kubwa kwa jinsia zote lakini hasa kwa jinsia ya kiume.Husababisha misuli kusinyaa na kupunguza uwezo wa uume kufanya kazi vizuri(Upungufu wa nguvu za kiune) kitaalamu huitwa Erectile dysifunction

•Pia husababisha maumivu wakati wa tendo la ndoa na kukosa hamu ya tendo.maumivu ya misuli(fatiguae) na kumwaga haraka kwa wanaume(premature ejaculation)

•Kujichua inatajwa pia kupunguza uwezo wa kuona,uwezo wa kufikiri na kutokuota kwa nywele (Hair loss)
flyerdesign_12062023_195830.png



6.Kutokupima Afya.

Maradhi au magonjwa hayana ratiba kusena yatakutaarifu muda wa kuunwa.Hapana!!Magonjwa yanamvamia mtu muda wowote saa yoyote,Lakini imekuwa ni kawaida jamii kujenga tabia ya kutopima mpaka pale watakapoumwa.

•Kupima Afya kutasaidia kujua kama mwili wako uko salama au kuna vimelea hivyo kuviwahi kabla havijasababisha magonjwa(Primary treatment)

•Na kama ukiumwa ukaenda kupima.Unashauriwa kutumia dawa kwa ufasaha ili kupunguza madhara zaidi(Secondary treatment)

7.Kutokwenda kituo cha Afya badala yake kwenda kwa waganga wa kienyeji.

Hii tabia imekua kwa kasi sana.Unakuta mtu anaumwa Malaria,Typhoid,Cholera n.k sasa badala ya kwenda kituo cha afya, anaenda kwa mganga wa kienyeji kupata matibabu.

•Mganga wa kienyeju hana vifaa tiba vinavyomuwezesha kupima magonjwa ya binadamu hivyo awezi kujua ugonjwa sahihi unaokusumbua.

•Baadhi ya waganga hawana vibali hivyo kutoa dawa za kienyeji ambazo zinaweza kuwa sumu na kusababisha madhara zaidi.

8.Uvutaji sigara .
Uvutaji sigara ni kosa jingine tunalolifanya katika miili yetu.Sigara hutoa moshi ambao ni hatari kwa mapafu na mfumo mzima wa hewa(Gaseous exchange)

•Uvutaji sigara husababisha kansa ya mdomo na koo,kuingilia mfumo wa upumuaji(respiratory system disorders)na kusababisha magonjwa kama mafua ya njano(Sinusitis),Pneumonia,Tuberclosis,Bronchial Athma n.k


NINI KIFANYIKE(MABADILIKO)

•Elimu juu ya athari za ulevi itolewe ipasavyo kwenye jamii.

Jamii inabidi ielimishwe juu ya madhara yatokanayo na ulevi.Hii itaongeza uelewa na kupunguza waathirika wa ulevi.

Adhabu kali kwa wanauza vilevi kwa wenye umri chini ya miaka 18.
Ili kuokoa nguvu kazi ya taifa,Mamlaka itoe adhabu kali kwa wauzaji wa vilevi kwa wenye umri chini ya miaka 18 na mama wajawazito

Elimu itolewe juu ya athari za tabia za uzinzi na ngono zembe
Mamlaka husika inabidi ikae chini na vijana.Pia wazazi wakae chini na watoto wao.waelezeni athari na magonjwa ya ngono kama vile Maambukizi ya virusi vya UKIMWI,Kaswende na kisonono.

Jamii ihamasishwe juu ya umuhimu wa mazoezi
Hapa kwakweli niipongeze nchi yetu pendwa kwa kuamka na kuhamasika kufanya mazoezi.

Kupitia matamasha ya mbio kama vile kili-Marathon,CRDB-Marathon,Twaweza-marathon,Tulia-Marathon na kadharika.Jamii iendelee kuhamasika juu ya umuhimu wa mazoezi kwa kushiriki kampeni hizi.

Mamlaka itoe adhabu kali kwa waganga wa jadi wasio na vigezo na vibali.
Mamlaka husika itoe onyo kwa waganga wa kienyeji wasio na vibali na pia ichunguze na kuthibitisha dawa za kienyeji zinazotolewa na waganga wa kienyeji.

Vituo vya Afya vipunguze gharana za vipimo na kutoa elimu juu ya umuhimu wa kupima.
Vituo vya afya vitoe wito kwa wananchi kupima magonjwa hatarishi kama Malaria,Kipindupindu na mengine mengi


HITIMISHO.

•Jamii inapaswa kufahamu kwamba Afya ndio mtaji namba moja kwenye maisha.Unapofanya mambo yanayohatarisha afya yako,Ni sawa na kuhatarisha maisha yako.

•Kila mmoja anahaki ya kulinda afya ya mwingine.Unapoona jirani yako anafanya mambo ya kuhatarisha Afya yake huna budi kumuelimisha na kuilinda afya yake.

•Usafi ndio nyenzo ya kwanza inayotumika kulinda afya zetu.Tufanyie usafi miili yetu na mazingira yanayotuzunguka.

kwa hakika,AFYA NI MTAJI........

NAWASILISHA
WAKO MTIIFU,jini genious


Baada ya kusoma bandiko ili.Naomba ushiriki kwa kupiga kura uzi huu kwa kubonyeza mshale umeandikwa 'vote'.

AHSANTE
 
Acha kututisha mkuu maisha ni mafupi tu hivyo jibalance..Mimi ndugu yangu hakuwahi kunywa pombe Wala hakuwa mzinzi Ila akafariki kwa homa ya ini na hatujui aliipatia wapi kijana mdogo sana
 
Habari Kenge 01
Hongera kwa andiko zuri.
Kura yangu umepata.
Naomba kura yako kwenye andiko langu lonalojibu hoja za ripoti ya CAG. Ahsante.
 
Hapo kwenye macho ni kweli kabisa!!asilimia kubwa tumeshaathirika na kuvaa miwani ni msala mwingine.Je unaalternative yoyote kwasisi ambao hatupendi miwani na tunaumwa macho??
 
Hapo kwenye macho ni kweli kabisa!!asilimia kubwa tumeshaathirika na kuvaa miwani ni msala mwingine.Je unaalternative yoyote kwasisi ambao hatupendi miwani na tunaumwa mach

Akijujibu niTag namm
Nachojua kuna Contact lens kwa ambao hawapendi miwani(Spectacles) lakini pia kuna LASER therapy na Corneal surgery ambayo ni expensive sana kwa ushauri zaidi fika clinic ya macho au CCBrT
 
Back
Top Bottom