Makosa matano ya Wafilisti kwa Samsoni

MAKOSA MATANO YA WAFILISTI KWA SAMSONI
By CK Allan - Kitabu Cha Rejea ni kutoka WAAMUZI (Biblia)

Inasadikika kuwa watu waliouwawa kwa mkono wa Samson kwenye ule ukumbi (uwanja wa michezo) siku Ile Samson anajitoa mhanga, walikuwa ni wengi KULIKO wale waliouwawa wakati wa uhai wake!

Kwa Lugha rahisi kama Samson aliishi miaka 30

Idadi ya watu aliowaua kwa miaka hiyo 30 ni wachache kuliko watu waliouwawa ndani ya dakika chache za mwisho za uhai wake..

Kwenye mpira tungesema what a comeback!! 😝

Yafuatayo ni MAKOSA ya kizembe kabisa kufanywa na Wafilisti mpaka kupelekea kuuliwa

1. Kushindwa kumuua kabisa Samson pale walipopata nafasi!
Yaani walikutana na adui yao, eti wakamtesa, wakamtoboa Macho tu! Walitakiwa wakate kichwa. Bila shaka ndio maana wafalme wa kale wakitaka kuua adui zao wanasema "niliteeni kichwa chake!"

2. Kusahau kabisa kuhusu nywele za Samson!
Yaani Wafilisti walijua kabisa "ASILI" ya nguvu za Samson ni nywele, kwahiyo Suluhisho ni ilikua ni kuweka ulinzi kwenye nywele zake yaani zikitokea tu! Wembe.. ilibidi Samson aitwe kipara mwanzo mwisho

3. Kumpa Samson adhabu ya kuzunguusha mashine ya kusaga nafaka!
Walidhani wanamkomoa, Lakini technically haya yalikuwa mazoezi ya misuli kwa Samson! Hebu fikiria zaidi ya miaka miwili Samson anafanya mazoezi makali, ulitegemea nini!

4. Kumdharau Samson
Wafilisti walikuwa na dharau sana kwa Samson, hata siku ya tukio bado walikuwa wanamfanya kama kichekesho! Hawakuona "hatari" yoyote kwake! Just imagine mtu aliyewahi kuua watu elfu 1, leo wanamchukulia poa tu!

5. Kukubali ombi la Samson la kupelekwa kwenye nguzo
Yaani mtu aliyewahi kung'oa lango la mji akaweka kwenye bega lake akasepa nalo. Leo anawaambia naomba nishike hizi nguzo za hii nyumba "nicheze" vizuri!

Wafilisti wanakubali! Yaani hakuna hata mmoja machale yanamcheza tu?
Ndio wapalestina wa leo
 
Dunia hii ya karne ya UELEWA bado kuna watu mnaamini hizi hadithi za kubuni za sungura na fisi?
Hadithi zinaendelea, miaka hamsini ijayo wenye uelewa hawata amini kuwa Israel ilivamia Gaza na kuchinja watu miezi sita bila jumuia ya kimataifa kuingilia, yaani hata waarabu na waislamu wenzao
wanachekacheka tu

Na hio Gaza ni mji wa wafilisti uliotoholewa na warumi badala ya philistine wanaita Palestine

Israel ni hadithi ya kutisha!
 
MAKOSA MATANO YA WAFILISTI KWA SAMSONI
By CK Allan - Kitabu Cha Rejea ni kutoka WAAMUZI (Biblia)

Inasadikika kuwa watu waliouwawa kwa mkono wa Samson kwenye ule ukumbi (uwanja wa michezo) siku Ile Samson anajitoa mhanga, walikuwa ni wengi KULIKO wale waliouwawa wakati wa uhai wake!

Kwa Lugha rahisi kama Samson aliishi miaka 30

Idadi ya watu aliowaua kwa miaka hiyo 30 ni wachache kuliko watu waliouwawa ndani ya dakika chache za mwisho za uhai wake..

Kwenye mpira tungesema what a comeback!! 😝

Yafuatayo ni MAKOSA ya kizembe kabisa kufanywa na Wafilisti mpaka kupelekea kuuliwa

1. Kushindwa kumuua kabisa Samson pale walipopata nafasi!
Yaani walikutana na adui yao, eti wakamtesa, wakamtoboa Macho tu! Walitakiwa wakate kichwa. Bila shaka ndio maana wafalme wa kale wakitaka kuua adui zao wanasema "niliteeni kichwa chake!"

2. Kusahau kabisa kuhusu nywele za Samson!
Yaani Wafilisti walijua kabisa "ASILI" ya nguvu za Samson ni nywele, kwahiyo Suluhisho ni ilikua ni kuweka ulinzi kwenye nywele zake yaani zikitokea tu! Wembe.. ilibidi Samson aitwe kipara mwanzo mwisho

3. Kumpa Samson adhabu ya kuzunguusha mashine ya kusaga nafaka!
Walidhani wanamkomoa, Lakini technically haya yalikuwa mazoezi ya misuli kwa Samson! Hebu fikiria zaidi ya miaka miwili Samson anafanya mazoezi makali, ulitegemea nini!

4. Kumdharau Samson
Wafilisti walikuwa na dharau sana kwa Samson, hata siku ya tukio bado walikuwa wanamfanya kama kichekesho! Hawakuona "hatari" yoyote kwake! Just imagine mtu aliyewahi kuua watu elfu 1, leo wanamchukulia poa tu!

5. Kukubali ombi la Samson la kupelekwa kwenye nguzo
Yaani mtu aliyewahi kung'oa lango la mji akaweka kwenye bega lake akasepa nalo. Leo anawaambia naomba nishike hizi nguzo za hii nyumba "nicheze" vizuri!

Wafilisti wanakubali! Yaani hakuna hata mmoja machale yanamcheza tu?
Hawakufanya makosa ila ni kusudio la mungu kutokea kwa mambo yote ili tutambue ya kuwa yupo
 
Back
Top Bottom