Mahakama yakubali ombi la DPP kuondoa rufaa dhidi ya Sabaya, sasa yupo huru na hana rekodi ya uhalifu

Heparin

Senior Member
Sep 24, 2021
152
575

Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) Silvester Mwakitalu, Leo amewasilisha katika Mahakama kuu ya Tanzania masijala ya Arusha ombi la kuiondoa Rufaa No.155 ya Mwaka 2022 Aliyokua ameikata dhidi ya Aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya Na wenzake.

Rufaa hiyo ilikatwa na Jamhuri baada ya Sabaya na wenzake kushinda kesi hiyo ya Uhujumu uchumi No.27 ya mwaka 2021 katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Arusha Mbele iliyosikilizwa na Kuambuliwa na Hakimu Patricia Kisinda.

Rufaa hiyo ilipangwa kusikilizwa Mfululizo na Mahakama kuu kuanzia tarehe 29/04 hadi 03/05 Mbele ya Mhe Salma Maghimbi Jaji wa Mahakama kuu kanda ya Dar es salaam aliyefika Kusikiliza shauri hilo.

Akiwasilisha nia Ya kuliondoa shauri hilo mbele ya Jaji Salma, Muendesha mashtaka Muandamizi wa serkali Akisa mhando Alieleza “Mhe Jaji,Shauri hili limekuja kwa ajili ya kusikiliza rufaa,hata hivyo mrufani (Jamhuri) imewasilisha ombi chini ya kifungu cha sheria No.386 (1) cha sheria ya muenendo wa makosa ya jinai marejeo ya mwaka 2022,ombi letu ni kwamba Jamhuri haina nia ya kuendelea na Rufaa hii dhidi ya Sabaya na wenzake,hivyo tunaomba kuiondoa hapa mahakamani”

Baada ya Uamuzi huo,Jaji Maghimbi alitoa uamuzi kwamba rufaa hiyo imeondolewa mahakamani Rasmi.

Kufuatia uamuzi huo, sabaya Anakuwa hana shauri lolote linalomkabili mahakamani na anahitimisha rasmi leo safari ya kesi alizokuwa anakabiliana nazo kuanzia tarehe 04/06 /20201 alipopandishwa kizimbani mara ya kwanza.

Wakili wa sabaya,Moses Mahuna mbele ya waandishi wa habari ameeleza kwamba kuanzia sasa,sabaya ni mtu huru na kwa mujibu wa mahakama yenyewe,hana rekodi yotote ya uhalifu na hana shauri lingine lolote katika chombo chochote cha sheria,na kumfanya kumalizana Rasmi na Mahakama.
 
Habari za hivi punde: Sabaya afutiwa rufaa aliyokatiwa na Serikali Arusha, DPP hana nia "kesi zote zimeisha"
Sabaya anarudi kwenye uongozi baada la hili kesi zote zimeisha tusubiri muda ufike tuone
 
View attachment 2979790
Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) Silvester Mwakitalu, Leo amewasilisha katika Mahakama kuu ya Tanzania masijala ya Arusha ombi la kuiondoa Rufaa No.155 ya Mwaka 2022 Aliyokua ameikata dhidi ya Aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya Na wenzake.

Rufaa hiyo ilikatwa na Jamhuri baada ya Sabaya na wenzake kushinda kesi hiyo ya Uhujumu uchumi No.27 ya mwaka 2021 katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Arusha Mbele iliyosikilizwa na Kuambuliwa na Hakimu Patricia Kisinda.

Rufaa hiyo ilipangwa kusikilizwa Mfululizo na Mahakama kuu kuanzia tarehe 29/04 hadi 03/05 Mbele ya Mhe Salma Maghimbi Jaji wa Mahakama kuu kanda ya Dar es salaam aliyefika Kusikiliza shauri hilo.

Akiwasilisha nia Ya kuliondoa shauri hilo mbele ya Jaji Salma, Muendesha mashtaka Muandamizi wa serkali Akisa mhando Alieleza “Mhe Jaji,Shauri hili limekuja kwa ajili ya kusikiliza rufaa,hata hivyo mrufani (Jamhuri) imewasilisha ombi chini ya kifungu cha sheria No.386 (1) cha sheria ya muenendo wa makosa ya jinai marejeo ya mwaka 2022,ombi letu ni kwamba Jamhuri haina nia ya kuendelea na Rufaa hii dhidi ya Sabaya na wenzake,hivyo tunaomba kuiondoa hapa mahakamani”

Baada ya Uamuzi huo,Jaji Maghimbi alitoa uamuzi kwamba rufaa hiyo imeondolewa mahakamani Rasmi.

Kufuatia uamuzi huo, sabaya Anakuwa hana shauri lolote linalomkabili mahakamani na anahitimisha rasmi leo safari ya kesi alizokuwa anakabiliana nazo kuanzia tarehe 04/06 /20201 alipopandishwa kizimbani mara ya kwanza.

Wakili wa sabaya,Moses Mahuna mbele ya waandishi wa habari ameeleza kwamba kuanzia sasa,sabaya ni mtu huru na kwa mujibu wa mahakama yenyewe,hana rekodi yotote ya uhalifu na hana shauri lingine lolote katika chombo chochote cha sheria,na kumfanya kumalizana Rasmi na Mahakama.
FB_IMG_1714737156736.jpg
 
kwamba kuanzia sasa,sabaya ni mtu huru na kwa mujibu wa mahakama yenyewe,hana rekodi yotote ya uhalifu na hana shauri lingine lolote katika chombo chochote cha sheria,na kumfanya kumalizana Rasmi na Mahakama.
Maandalizi ya kurudishwa tena madarakani.

Ila hii nchi uongozi una madaraka makubwa sana. Yani watu wanaamua uhalifu na kutokuwa muhalifu kwa mtu kirahisi rahisi tu.
 
Though haki haijafanyika, tunashukuru ole aliwekwa ndani, akala makozi ya kutosha na makofi. Akakonda. Alipokua ndani. Acha mioyo yetu iridhike kwa hayo tu. Funzo alipewa sasa afanye atakalo.
 
Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) Silvester Mwakitalu, Leo amewasilisha katika Mahakama kuu ya Tanzania masijala ya Arusha ombi la kuiondoa Rufaa No.155 ya Mwaka 2022 Aliyokua ameikata dhidi ya Aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya Na wenzake.

Rufaa hiyo ilikatwa na Jamhuri baada ya Sabaya na wenzake kushinda kesi hiyo ya Uhujumu uchumi No.27 ya mwaka 2021 katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Arusha Mbele iliyosikilizwa na Kuambuliwa na Hakimu Patricia Kisinda.

Rufaa hiyo ilipangwa kusikilizwa Mfululizo na Mahakama kuu kuanzia tarehe 29/04 hadi 03/05 Mbele ya Mhe Salma Maghimbi Jaji wa Mahakama kuu kanda ya Dar es salaam aliyefika Kusikiliza shauri hilo.

Akiwasilisha nia Ya kuliondoa shauri hilo mbele ya Jaji Salma, Muendesha mashtaka Muandamizi wa serkali Akisa mhando Alieleza “Mhe Jaji,Shauri hili limekuja kwa ajili ya kusikiliza rufaa,hata hivyo mrufani (Jamhuri) imewasilisha ombi chini ya kifungu cha sheria No.386 (1) cha sheria ya muenendo wa makosa ya jinai marejeo ya mwaka 2022,ombi letu ni kwamba Jamhuri haina nia ya kuendelea na Rufaa hii dhidi ya Sabaya na wenzake,hivyo tunaomba kuiondoa hapa mahakamani”

Baada ya Uamuzi huo,Jaji Maghimbi alitoa uamuzi kwamba rufaa hiyo imeondolewa mahakamani Rasmi.

Kufuatia uamuzi huo, sabaya Anakuwa hana shauri lolote linalomkabili mahakamani na anahitimisha rasmi leo safari ya kesi alizokuwa anakabiliana nazo kuanzia tarehe 04/06 /20201 alipopandishwa kizimbani mara ya kwanza.

Wakili wa sabaya,Moses Mahuna mbele ya waandishi wa habari ameeleza kwamba kuanzia sasa,sabaya ni mtu huru na kwa mujibu wa mahakama yenyewe,hana rekodi yotote ya uhalifu na hana shauri lingine lolote katika chombo chochote cha sheria,na kumfanya kumalizana Rasmi na Mahakama.
Serikali ya Utakatishaji.
Hicho ndicho kitu serikali ya CCM inaweza kukifanya. Kutakatishana mpaka kutakata.
Peoples Laundering.
 
Back
Top Bottom