#COVID19 Mahakama yafuta agizo la Rais kupiga marufuku mikutano ya umma na kisiasa kudhibiti maambukizi ya COVID-19

Behaviourist

JF-Expert Member
Apr 8, 2016
39,902
95,422
Jaji wa Mahakama kuu ya Kenya Anthony Mrima amefuta maagizo yaliyotolewa na Kamati ya Ushauri ya Usalama wa Kitaifa(NSAC) iliyopiga marufuku mikutano ya umma na ya kisiasa nchini humo katika kudhibiti kuenea kwa maambukizi ya UVIKO 19.

Jaji Mrima amesema agizo hilo lilikuwa kinyume cha katiba.

My take:
Haya hayawezi kamwe kutokea Tanzania kwa sababu mihimili yetu ya Mahakama na Bunge huwa inawekwa mfukoni na Rais.

Ni jukumu la Raia wote bila kuangalia vyama vyetu kupigania uhuru wa mihimili hii ili kuwa na Taifa linalojali haki za binadamu,demokrasia, maendeleo na kuheshimu katiba.

Hongera sana Wakenya kwa kufikia hatua hii.

EAIPEO1.jpg



Source:
 
Hapa kwetu serikali imeanza kufuata ushauri wa kina Mbowe, Lisu, Zito na magenge yao ambao waliitaka serikali iwaweke wananchi wake kwenye lockdown, ili kuzuia maambukizi ya uviko 19 kuenea zaidi. Serikali hii sikivu imeanza kufuata ushauri na matakwa ya viongozi hao wa upinzani kwa kuanza na hatua ya kwanza ya kuzuia mikusanyiko ya watu ktk mikutano mbali mbali hapa nchini.
 
Back
Top Bottom