Magufuli wana hasira na wewe, mpe Makonda Unaibu Waziri Mkuu, anaweza

Sijawahi kudhani kuwa watanzania wengi ( sio wote ) ni wajinga wa ngazi hii tunayoiona. Ndio maana ni ngumu kutofautisha mtanzania wa kidato cha sita na yule wa chuo kikuu. Katika IQ zao, kuwaza kwao, kufikiri kwako.

Maana hata huyu aliyesoma kasomeshwa kuwa manamba, robot ambaye hawezi kujiuliza, kuuliza, hawezi kuwa na simile ya kuongea. Ila muonekano wao na maelezo yao wanajiita wasomi! Waliosoma sana ........wenye PhD, Masters, Degree za kwanza mpaka Darasa la saba.

Hii jamii inayoishi kwenye uchafu wa kila aina, rushwa, uvivu, madawa ya kulevya, shisha, uwizi na mabaya yote , yalifikia hatua yanaonekana kama ni sehemu ya ustaarabu wa mtanzania! Hakuna wa kuyakemea! Na anayeoneana anayakemea basi aidha ana nguvu nyuma yake, mbele yake, kuna kitu anajiamini, wengine wakadiriki kusema amezindikwa kwao! Maana watanzania hawa wanafiki watakubadilisha

Matokeo yake hatuna viongozi wanao THUBUTU….WANAOAMUA, WANAOTENDA….

MHE. RAISI NIKUKUMBUSHE KUWA MAADUI WA MAKONDA NDIO WAKO PIA, NI HAWA HAPA
Lowassa, Rostam, Chenge

Hawa waliambiwa wazi wazi, bila kificho kuwa ni wezi wakubwa kwa nafasi zao, kupoka utajiri wa watanzania. Hakuna mtu yeyote mwenye akili Timamu aliyeweza kuwaona hawa watu ni wasafi.

CHADEMA pale mwembe Yanga walisema wazi kabisa kuwa Lowassa ni Mwizi, Rostam hafai na Chenge hakukosekana! Hawa n wahujumu uchumi, pamoja na wezi wengin wengi waliomo ndani ya CCM, CHADEMA, CUF, NCCR n.k

Makonda bila kupepesa macho pale CCM ilipoamua hawa wajivue gamba, Makonda alieleza publickly na HAKUNA KATI YA HAWA aliyefurukuta mbele ya Makonda , walikuwa wachafu

Kundi hili linaloishi kwa jina la 4U movement, huku Chenge akiwa Bungeni wanaona ni naasi nzuri ya kulipiza kisasi. Kati ya hao Rostam ana hasira Zaidi! Hajawea mtu wake ( king maker) na aliyeko madarakani haingiliki kirahisi

Jamii ya walioamini Tukio la Warioba
Pamoja na warioba mwenyewe kukanusha kuwa Makonda hakutaka kumpiga, bado jamii ile ya watanzania wale, wanaoamini kila kitu mpaka wanaambiwa mavi ni dawa ya upako, au kuwa mkojo unaponya HIV, jamii ile ile ya waamini dini zile zile , wenye akili zile zile.

Walipoaminishwa na kundi la U4 movement, kuwa ni Makonda…..wale wenzangu na wale wasiojielewa wakaanza kutupa shutuma kila mahali. Leo hii wengi wana hasira na Makonda wakikumbuka lile tukio kumbe Halina ukweli,bali Makonda alikuwa anamkimbiza warioba asishambuliwe

VIONGOZI WENZAKE WA MKOA
Madiwani, mameya, wanachama wa chadema, wengi hawampendi kabisa Makonda. Ufanyaji kazi wa Makonda umekuwa wa ubunifu, na kuna akili za kijinga eti hakuna alichokifaya kikafanikiwa..kana kwamba waliweka timeline! Kuwa hiki kiishe hapa.

Hata zile personal initiatives ambazo zingefanywa na mawaziri, vyama vya upinzani na NGOs kama kusaidia walimu wapande daladala bure. Bado zilionekana kama ni ‘eti’ makonda mwenyewe kumbe uwezo wake uliishia kwenye ushawishi tu. Kundi la hawa wanachadema ambao hawana jipya, hawawezi kuwaza/kufikiri, hawana utatuzi na matatizo yanayoikabili nchi hii…

HAWA ndio wanaokejeli na kumpinga Makonda kila Kona! Kila anachokifanya…KANA KWAMBA tushawahi kuwa na kiongozi ambaye ameishaonyesha UTHUBUTU WA kutatua kero!! He just needs support. Bahati mbaya watanzania WENGI wanawapenda viongozi…wasiokuja na mbinu mpya, mawazo mapya…kwa sababu anayejaribu TUNAMKEJELI! Hawa ndio watanzania

NDANI YA CCM
Tunajua na sio siri, CCM imekuwa chama kikubwa japo wengi ni wezi kwa sababu ya uwezo wao wa kuwa na makundi makubwa ya ushawishi na hatarishi sio kwa chama bali kwa nchi pia. CCM ni Tanzania kubalini, kataeni. Makonda alivyo wapelekesha wachafu wa CCM wa kipindi kile, na hawa wa sasa wa madawa! Ni dhahiri chuki juu ya Makonda inakuwa kubwa Zaidi

Kibaya Zaidi, anachukiwa Magufuli ila chuki na mtu rahisi Zaidi wa kumtupia Lawama zote ni Makonda…MAGUFULI CCM YA SASA HAIKUPENDI UMEWABANIA HASIRA ZINAENDA KWA YULE DOGO!

MBOWE
Mbowe ni kama kanisa, kuna watu wanampenda mbowe kuliko kitu chochote, wako tayari kuambiwa chochote na mbowe wakakubali dakika yoyote, hawa wana mapenzi ya upofu ambayo ni hulka ya kiasili kabisa ya binadamu!! Ila wana chuki, wivu na hasira…

wapenzi wa Mbowe sio wanachadema, na mbowe sio mwanachadema….affairs za Mbowe sio za chadema, na sura ya chadema kama chadema aidha inakuwa ya kichama kama wanachama wako juu , au inakuwa ya Mbowe kama mbowe kama yuko juu, saa hizi anakuja Lowassa ambaye anaweza kuvunja ndoa au uhusiano wa Mbowe na chadema.

Mbowe kawa tajiri kabla ya chadema, kafungua Bilicanas kabla ya chadema…Mtaji wa Mbowe hakuna mwanachadema anayeujua! Hata mkwe wake alipompa chama hakuna wa kuuliza hata hii leo

ILA BAVICHA kuna wakati wanaona wako sawa kabisa kumuhusisha affairs zote za mbowe na chama. Utajiri wa Mbowe chanzo ni nini? Je anawajua wauza madawa?? Mbowe anafungua kesi yay eye kuitwa KAACHA KESI YA MUHIMU KABISA YA KUWA TUWE NA TUME HURU YA UCHAGUZI!!! MBOWE NI NIGGER, NI MFANYABIASHARA, NI EXPERT AMBAYE ANAANGALIA HELA TU!! Ebu amkeni wenzetu

KAMA KUNA KITU AMBACHO WAPENDA MABADILIKO TUNAKITAKA NI TUME HURU YA UCHAGUZI……tufungue mgogoro wa kikatiba kuhusu hili, si kuwa na MAWAKILI KUMI KUTETEA MBOWE KUITWA NA MAKONDA!!! Aisee!! Lini mtaanza kufikiria kama wanaume???

MAADUI WA MAGUFULI
Hawa ni wengi sana, ukimchukia Magufuli utamchukia na kila aliye karibu naye. Kipindi cha kampeni ilikuwa shida hata kumtetea magufuli! Maana wafuasi wa Lowassa wangekukula Nyama…….wafuasi wa Magufuli hawajawahi kupendwa kuanzia Kampeni mpaka leo utendaji wake

Tumbua tumbua, kuzuia rushwa, kuhamishia hela benki kuu kumeongeza sana maadui wa magufuli. Na mh. Makonda ambaye kila saa anataja jina la JPM…anavuna maadui wote wa magufuli kuja kwake….hasira zile zile ambazo zingempata magufuli, matusi yale ambayo angeyaoga Magufuli yanaenda kwa makonda ndio DUNIA.....

GWAJIMA wa Slaa, wa Lowassa wa ukiwa
Ni mkiwa, hawezi kukaa kimya, wala hawezi kunyenyekea na kuonyesha sura ya Yesu halisi. Hakuweza kufanya hayo kipindi cha ugomvi wake na Slaa, ugomvi wake na Mbasha alipoiba mke wa Emmanuel Mbasha, na migogoro mingine mingi ndani ya kanisa.

Ni kwa vile TRA yetu haina utaratibu wa kufuatilia mapato ya kanisa. Leo angekuwa na helkopta zingine kumi na investments kibao……..Gwajima ni mchafu! Makanisani anahubiriwa hivyo, anajulikana hivyo. Yeye kuanza vita au kuendeleza vita na Makonda ilitarajiwa , si mtu wa kusamehe, ni mafia ana bodyguard na walinzi kama rais wa Korea na sio kama Yesu alipokuwa Duniani…

Ila watanzania wenzetu wale wakishapenda……bas watamtetea sana tu….ndio mapenzi upofu. Gwajima ni Mkiwa! Njia pekee ya yeye kuwafurahisha chadema, Lowassa na 4U movements ni lazima awe upande wao. Hata sasa yumo. Muda utaamua tuhuma zake hizi.

TRA mna muda wa kurudia kufuatilia income, manunuzi, kodi halali na projections…kuna mahali akili haiingii. Ni muda sasa wa serikali kuweka kodi kwenye haya makanisa ambayo na mimi ni mwanachama.
Gwajima ilitakiwa kanisa lake lifungwe! kwani nini kitatokea?? yeye ni nani? sio kanisa lile ni social club fulani hivi

WABUNGE
Vijana wanakatwa 15% ya mkopo, NSSF, PSPF, n.k hakuna mafao…….KODI KUBWA kila mahali, CCM walijiwekewa mazingira ya kuwa na investiments na vipato rahis kila mahali. Hawa wabunge kila kona wamebanwa kuanzia mashirika ya umma, na saari za nje ….WOTE HAWA KISAIKOLOJIA WANA HASIRA NA MAGUFULI, then Makonda kaingia kwenye anga zao……

Plus Chenge+ Plus Testimony ya Steve Nyerere……..Bunge ni chafu, na liko low sana kuanzia kujadili vitu, kuwaza kwa mapana na kujipambanua kuwa wao ni mhimili. Wabunge kamwe hawako kumsaidia mwananchi wa kawaida. Wadogo zetu wanatumia madawa ya kulevya, Bunge halikuwa kushinikiza wala kuongea kuhusu madawa….WOTE WALIENDA DODOMA KUTALII NA WALIPOSIKIA HABARI YA MJINI NI MADAWA kila mmoja akawa akisimama anachangia kuhusu MADAWA…

Raisi Bunge hili ni la kudharauliwa!!! Wana hasira na wewe!! Makonda ni punching bag tu

SI WA MADAWA TU
Wauzaji wa madawa, shisha, wapora viwanja vya watu ambavyo makonda alivizuia, mashoga, wale wavivu na jobless ambao waliambiwa watafute kazi!!!…achilia mbali wale watumishi waliotumbuliwa kila mahali-DSM na wilaya ya kinondoni!! Limekuwa jeshi kuwa sana, linasema na kuongea kila mahali. Wana hasira sana.

WALE WAFAFUATA MKUMBO.
Hawa na wafuata upepo, kuna wasomi humu, wenye degree 10, mbili, tatu. Kuna mabosi wa mashirika, wengine madaktari na wengine wanasheria…..hawa ni wengi wanatia huruma. Hawa ni wale waliambiwa Lowassa ni Fisadi kisha ghafla wakaambiwa Ni msafi akiwa chadema!! Kichekesho. Sidhani kama kuna mtu kasemwa nchi hii kuhusu ufisadi Zaidi ya Lowassa! hakuna

Kundi hili huwa hawajiulizi, kwa mfano waumini wa kanisa lile….unapanda gari na kwenda kusikiliza mchungaji wako akisema Makonda kaiba cheti! Anatumia jina la mtu.

Hawa ndio wanajiita walokole…..wameacha njia ya awali, na walokole wengine maeneo mbalimbali wanashangilia hili swala wakati Gwajima anatumika na shetani kuufanya ulokole uonekane wa KISASI, MAGUBU, CHUKI….Sura ya Ulokole ya Marehemu Mozes Kulola sio hii ya Gwajima, anawaharibia….vita ya kiroho Zaidi hii!

Wafuata upepo: matokeo tu ya kubandika, au ya website au yaliyobandikwa ubao wa matangazo wa hapo shuleni ya daudi bashite au paul kagenzi YAKO WAPI??

Aliyeuza cheti yuko wapi? Anafanya nini? Kweli kwa pesa ya Gwajima, chadema, Lowasa na vyombo vya habari vya chadema hawezi kupatikana huyu?? Achilia mbali vyeti!..Hamuoni sisi wapiga kele wanatuchora??

Au kwa nguvu hii hii ya kwenda mahakamani, kweli Lissu na asivyo na simile asingeuwa ashampeleka Makonda mahakamani, au evidence za haya mambo huwa ni kazi sana??

Inachukua muda gani kuonyesha matokeo hata yale ya jumla tu...yakiwa na wenzake wengine??



MWISHO
Makonda anafaaa kuwa Naibu waziri mkuu, cheo kile kama cha mrema kwa nini??

1. Anawaza
2. Anajaribu
3. Anafikiri
4. Anakuja na kitu kipya
5. Ni jasiri na haogopi

Atasimamia na kuinyoosha nchi……kama anakosea hapa na pale anaelekezwa! Lakini ni Asset ya Taifa! tunamuhitaji zaidi sana kipindi hiki kuliko wakati wowote, pale ambapo system zimefail, watu wanaogopa kuusema ubaya, Makonda anasimama kuusemea ubaya kwa jina lake!!

Kwani unahitaji nini Kingine Rais??


Kaka gwajima mbona hamsemi magufuli na wakati magu kamponda kupeleka kwanya polisi, kama yy kidume angemjibu rais kwa nini anakimbilia kwa makonda? nimekuelewa mkuu na wanao isoma number ni ccm waliozoea vya dezo wacha wanyooshwe, hawa akina rizwan walitaka kuifanya nchi ya kifalme sasa nao wananyenyekea safi sana hii nchi ni ya wote
 
Naibu waziri mkuu mmnh sijawahi kusikia kitu hii Tanzania. Naona umeungaunga sana hoja zako pole Waberoya umeroya kweli kweli
 
Vya mropokaji mtavipata, na vita ya madawa ya kulevya inaendelea kama kawaida, kwani lengo lenu ni kujaribu kukwepesha mada muhimu kwa jamii yetu.

Tumewashtukia na lazima macho manne akapimwe mkojo, tunataka tuanze kukata mirija ya soko la wanunuaji wa ngada kuanzia juu kabisa mpaka uswahilini.

asante mkuu
 
Kaka gwajima mbona hamsemi magufuli na wakati magu kamponda kupeleka kwanya polisi, kama yy kidume angemjibu rais kwa nini anakimbilia kwa makonda? nimekuelewa mkuu na wanao isoma number ni ccm waliozoea vya dezo wacha wanyooshwe, hawa akina rizwan walitaka kuifanya nchi ya kifalme sasa nao wananyenyekea safi sana hii nchi ni ya wote

Hasira zile zimeenda kwa Makonda!! ajaribu kumjibu Magufuli aone
 
Hasira zile zimeenda kwa Makonda!! ajaribu kumjibu Magufuli aone

hahaaaaaaaaa mkuu kila anaepanda jukwani ni makombora kwa Makonda huku wakijifanya kumshauri rais amshughulikie makonda na wakizidi kusema eti hajatumwa na mkulu haaaaa wabongo bana na ingali walimsikia ikulu akiwaponda hata wabunge ila nao wakaenda kucheza mziki wa makonda, kidogo zitto ndo alimjibu mkulu avunje bunge.
 
Waberoya nakukubali sana tatizo watanzania wengi wanapenda mabadiliko na maendeleo lakini akitokea mtu wa kushughulikia hayo basi huanza kuoneka Ima anajipendekeza au watasema anataka sifa Kwakweli tunashida kubwa ya uwelewa IQ
 
Wauza ngada chadema watakushambulia sana
yooote semeni, tunataka kuona vyeti vya Makonda ndiyo tunyamaze aviweke mezani haonewi mtu hapa yeye ni kioo cha Jamii lazima kila jambo analofanya liwe na katika utaratibu na sheria za nchi likiwemo hili la kuwa na vyeti sahihi.
 
mbowe kafungua kesi ya kikatiba, ni AG will stand for those fellas, not Makonda as individual

Mbowe can not be taken to court, kazuia mahakamani

usijishushe rafiki kwa kudhani anayewaza tofauti na wewe anataka teuzi, kwa jina la bandia???

wala haina presha, evidence hamna rafiki, kama unazo ziweke hapa...utatusaidia, hata hii thread nitaifuta ukiziweka hizo evidence
AG cannot stand for those fellas, yeye mwenyewe ni mshitakiwa katika kesi hiyo.
Mbowe anaweza kushitakiwa mahakamani, ila wamekatazwa kumkamata wala kumuweka rumande, wameruhusiwa kumuita na kumuhoji, ikithibiti wanaweza kumpeleka mahakamani.
Hatua ya awali, mahakama inatakiwa ithibitishe kuwa RC hakuwa na mamlaka ya kisheria kufanya alivyofanya, ikishafanya hivyo, nakala ya hukumu hiyo itatumika kama evidence ya kumshitaki Makonda (or Bashite or whatever) as an individual kwa kutumia vibaya cheo chake na kufanya defamation, fidia atapaswa ailipe yeye binafsi na wala sio ofisi yake.
Meanwhile, madai ya kupinga sheria ya detention without trial, mamlaka waliyopewa RCs na DCs ya kuweka watu ndani watakavyo, yamekuwa lodged kwakuwa sheria hiyo inaenda kinyume na katiba!
 
Hayo ni maamuzi yaliyo juu ya uwezo wako na wangu.
Kwani hatufuati sheria na taratibu tulizojiwekea kwa mujibu wa katiba?hakuna maamuzi ya juu kushinda katiba na yakitokea ndio malalamiko yanaanza hadi wale wanaochukia madawa wanaona hakuna kinachofanyika zaidi siasa chafu na badala ya kuunga mkono juhudi nzuri ila njia mbaya maana inakuwa imeshahalibika
 
WAZO BINAFSI LIKIAMBATANA NA CHUKI LINAKOSA MASHIKO...USINGEKUWA MNAFIKI UNGETAJA ORODHA YOTE YA WALIOTUHUMIWA/WALIOTAJWA PALE MWEMBEYANGA AKIWEMO MKAPA, KIKWETE NA WENGINE, ORODHA ILE ILIKUWA NA WATU 11 AU 12 HIVI NA WOTE WALIKUWA VIGOGO NA VIONGOZI WA CCM...!!




Tafakari...!!
kila aliopo ccm ni mchafu lakini akihamia chadema msafi ni shida.
 
Pamoja na hayo, kuna Tuhuma za cheti bandia, kwa mujibu wa sheria, kama ikibainika ni kweli hatostahili kuwa naibu Waziri bali mfungwa wa Segerea.
Unadhani kuna mtu anamwonea wivu Makonda? Au anamchukia? Ukweli kuhusu vyeti utaamua usafi wake...
 
Sawa basi awe naibu Waziri Mkuu na pia Wale wote waliokutwa na vyeti feki wakaondolewa waludishwe tena wapewe Vyeo zaid ya walivyokuwa Navyo...!!
 
Back
Top Bottom