Magufuli is Doing Good For This Nation, Tumuassess kwa Positive Attitude, Kwa Mazuri Tumpongeze, Tumuunge Mkono Kumsupport, lakini kwa Mabaya Tumkosoe

Kwani anakulipa kiasi gani kwa msifia kila siku.WATANZANIA SIO VIPOFU KAMA ANAFANYA VIZURI TUTAONA WENYEWE KWA NINI KUNA WATU WANAMSIFIA KIASI KWAMBA MPAKA MNAHARIBU UHALISIA WA MAMBO ALIYOYAFANYA.
Pasco sifia upendavyo lakini usikufuru kama yule RC alivomwita eti ni " Nabii" pale alipotoa hotuba wakimsubiria Uhuru Kenyatta...
 
Paskali kuna mahali nilisoma humu baada ya kuitwa bungeni hata tenda ya saba saba ulinyang'anywa

Imekuwaje tena ?

Halafu hapa umeniacha kidogo "ukiwa na positive atitude utasema maji ni half fool"
 
Duh kaka, umejitetea sana, waache tu hujui nia yao ni nini, maana hata DAB walianza naye hivi hivi, sasa kawa toilet paper.
Niliishasema Tumbo baya sana, ukilitumikia watu hawakuelewi hata ulie machozi ya damu.
 
Pascal ndugu yangu, Magufuli kufanya mambo ya maendeleo sio suala la hiari ni wajibu wake na sii jambo la muhimu kusifiwa.
Aliomba kazi hiyo kwa ahadi kemukemu na sasa hivi kwa kodi zetu tunazojikamua kumlipa,kumlisha, kumvesha na mazuri yote kwa kadri inavyo wezekana.
Lakini kubwa la kumtazama ni makosa yake hasa yale yahusuyo kukiuka katiba, uonevu kwa kutumia madaraka, upendeleo, ukatili na visasi.
Ndio maana 1992 sheria ilipitishwa kuwepo na vyama vya upinzani vitakavyotumika na chama chochote kitakacho kuwa madarakani kama kilo cha kujua wanapokosea ili kurekebisha mambo yaende sawia.
Kama makosa hayo hapo juu anayafanya na anazuia vyama vilivyo nje ya madaraka kufanya kazi yake ya kukosoa basi HAFAI NA HAFAI.
Hata apeleke umeme mpaka kwenye mazizi ya ng'ombe bado atakuwa hafai.
Umesema uko karibu naye, basi please tumia nafasi yako hiyo kumpa salamu za Chakaza wa JF na wengine wengi wenye mawazo haya niliyotoa.
Hivi baba wa familia, jamii inaweza inaweza kutumia muda kumsifia eti ananunua chakula cha watoto au analipa ada kila siku? Lakini anaweza kulaumiwa sana kwa watoto kutembea peku kwa kukosa viatu. The same to the president. Sifasifa za nini wakati hajitolei?
 
Wanabodi,

Mimi ni mdau mkubwa wa maonyesho ya Saba Saba, kwenye Saba Saba ya Mwaka huu, nimetembelea Banda la Wakala wa Nishati Vijijini, REA kwenye maonyesho hayo, nikazungumza Mwenyekiti wa Bodi ya REA, Mkurugenzi Mtendaji, Wajumbe wa Bodi, Menejimenti na wadau wa REA kuhusu kinachofanywa na REA.

Rais Magufuli amedhamiria kufikia mwaka 2025, wakati anaondoka madarakani, kupitia umeme wa Stigler na REA, kila mkoa, kila wilaya, kila kata, kila kijiji, kila kitongoji na kila kaya itakuwa na umeme.
Kwa dhamira hii, kwenye kipindi changu, nikampongeza rais Magufuli kuwa ana dhamira safi na ya kweli ya kulikomboa taifa letu na kuliletea maendeleo.
Nikaandaa kipindi kimoja cha 60 min, lakini kwa vile hakuna TV nchini yenye kuweza kutoa nafasi ya kurusha 60 min, nikakigawana kipindi kwenye vipindi 2 vya 30min each.


Kufuatia pongezi hizo, kumbe kuna mwana jf aliangalia kipindi na kanianzia thread


Mkuu the Retired, kwanza asante kuangalia kipindi changu, kwanza mimi Pasco, nafahamika sio humu tuu jf, kwa kuwa critical na mkweli, bali nafahamika hadi Bungeni, hadi Ikulu, kuwa Pasco ni mkweli, critical na very bold. Siku zote kwenye ukweli nausema, kwenye mazuri napongeza, kwenye mabaya nakosoa, kwa hili la azma ya rais Magufuli kusambaza umeme kila kaya, hili ni zuri, la kustahili pongezi na kuungwa mkono asilimia 100%.

Hivyo kwenye bandiko hili nina hoja zifuatazo
Magufuli is Doing Good For This Nation, Tutumie Positive Attitude Kumfanyia Assessment, Akifanya Mazuri, Apongezwe, Aungwe Mkono, Akikosea, Akosolewe! nitaziweka in number format
  1. Magufuli is Doing Good For This Nation, Rais Magufuli ndiye rais wetu, yeye sio malaika ni binaadamu tuu kama sisi na anaweza kukosea, kitu muhimu tunachokiangalia ni dhamira yake ya dhati kulikomboa taifa hili kutoka katika lindi la umasikini uliotopea na kuliletea maendeleo ya kweli ambayo ni maendeleo ya watu. Katika kuyatekeleza haya, naamini hakuna anadhani kuwa rais Magufuli he must be perfect, he is a human being, hivyo anaweza kukosea, lakini kukosea huko kunaweza kuwa kumefanyika kwa nia njema, hivyo kuna mipango mingi ya rais Magufuli aliyoidhamiria kwa taifa hili na ikifanikiwa, this man is real diong good for this nation, anastahili pongezi na kuungwa mkono.
  2. Tutumie Positive Attitude Kumfanyia Assessment. Kwa vile nimeishasema toka mwanzo kuwa rais Magufuli sio malaika, wala hategemewi kuwa malaika, ni binadamu kama sisi hivyo kuweza kufanya makosa ya kibinaadamu kama binaadamu wengine wote, hivyo katika kumfanyia a fair assessment lets not concentrate on the negatives, lets look at hizi positives. Kuna type ya watu wanaitwa fault finders, wao kazi yao na kutafuta makosa tuu na kuangalia mapungufu, hata mtu ufanye mazuri mangapi wao hawayaoni na hawayazungumzi, lakini ukifanya kosa moja tuu, linageuka wimbo!. Tutumie ile yardstick ya kanuni ya maji nusu katika glass, ukiwa na negative atitude utasema maji ni half empty, ukiwa na positive atitude utasema maji ni half fool, hivyo tukimfanyia rais Magufuli assessment with positive attitudes, utajikuta hata zile negatives zake, ukiwemo hoja ya udikiteta, utauchukulia positive kuwa ni a benevolent dictator, yaani dikiteta mwema anayetumia udikiteta kuletea maendeleo, kwa sababi kiukweli kabisa, hapa Tanzania tulipofikia, tulihitaji mtu kama huyu.
  3. Akifanya Mazuri, Apongezwe, Aungwe Mkono. Kwa vile rais Magufuli ni binadamu tuu kama sisi, Watanzania wote wazalendo wa kwenye wenye nia njema na taifa hili, wata wish rais Magufuli afanikiwe katika azma yake ya kulikomboa taifa hili toka katika lindi la umasikini uliotopea, kwa kujenga Tanzania ya viwanda, na kuipeleka Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati. Katika kutekeleza haya, Rais Magufuli akifanya mazuri, anastahili pongezi na kuungwa kuungwa mkono ili kumtia moyo, encouragement azidi kufanya mazuri. Kama Mungu tuu mwenyewe hana mpinzani ni wajibu wa binadamu na viumbe wote kumwabudu Mungu, kumsifu, kumtukuza na kumwimbia nyimbo za shangwe sifa na utukufu, hakuna ubaya wowote, pale ambapo rais Magufuli anafanya mazuri, apongezwe, asifiwe na kuungwa mkono. Hapa naomba kutoa angalizo, sijasema aabudiwe!, kuna watu wanataka kumwabudu, au kuna wale wa type ya yule kichaa wetu, kazi yake ni kusifuu tuu, mimi sizungumzii kumsifia kwa mtindo wa mapambio, bali kupongeza, kumtia moyo, kum encourage na sio kumvimbisha kichwa.
  4. Akikosea, Akosolewe!. Kama nilivyoeleza mwanzo, rais Magufuli sio malaika ni binaadamu, na hakuna binaadamu mkamilifu, no one is perfect, hivyo kuna kuna maeneo rais Magufuli anakosea kama binadamu wengine, mimi na watu wa type yangu, ambao ni waumini wa ukweli, tukiongozwa na falsafa ya ukweli usemwe, siku zote tutaendelea kusema kweli daima, hivyo rais Magufuli kama binadamu, akikosea, akosolewe kwa heshima kwa kutumia lugha ya staha na kuambiwa ukweli, na sio kukosolewa kwa kubezwa, kudhalilishwa kwa lugha za machukizo. Kwa mtu yoyote au kiongozi yoyote, mwenye akili, akikosolewa atafurahi na kujitathmini, utakuta sisi wakosoaji wa rais Magufuli na serikali yake, ndio watu tunamsaidia zaidi rais Magufuli kuwa rais bora, kuliko wasifiaji na waimba nyimbo za sifa na mapambanio na naamini rais Magufuli anachukulia ukosoaji very positively, katika hili la ukosoaji, mimi naamini kuna tatizo la wapambe nuksi wanaomsingizia rais kuwa anachukia wakosoaji, Najitolea mfano mimi mwenyewe, kuna kazi fulani fulani nimezuiliwa kuzifanya nikielezwa na hao wanaonizuia kuwa ni amri kutoka juu, ati kuna siku fulani, sisi waandishi tulialikwa mahali fulani, mimi nikauliza swali fulani, kwa fulani, ninaelezwa juu juu kuwa huto fulani alikasirika sana na na mtu wa visasi, ati kufuatia hasira hizo, ndio ameamrisha mimi nisiruhusiwe kufanya vitu fulani!. Wapambe hao hawasemi ni amri kutoka wapi, hivyo mimi mimi siamini kuwa ni kweli ni amri kutoka juu, bali wasaidizi wake wakiisha kuambia ni amri kutoka juu, wewe utakwenda wapi kuuliza?. Hawa watu walionipa hiyo amri kudai kuwa ni amri kutoka juu, hawanijui, wakijua ukiambiwa tuu amri kutoka juu, utaogopa!, kumbe mwenzaa ndio kwanza niko kwenye mchakato wa kufika huko juu kabisa, kilele na kuuliza "Mzee, kweli hii amri yako mimi sifanye hili na lile?!", nikijibiwa ni kweli, then nitakuwa sina jinsi bali ni kutundika tuu daluga na kutafuta shughuli nyingine ya kufanya kuendesha maisha yangu!.
  5. Jee ukiwa Critical, ni mkosoaji mzuri wa maeneo yenye makosa, siku rais Magufuli akifanya mazuri, ukampongeza, huwezi kumpongeza genuinely bila kuonekana unajikomba, unajipendekeza, ni njaa tuu ya kusaka uteuzi?. Naomba niwahakikishie wana JF, mimi Pasco, sio mwanachama wa chama chochote cha siasa, na kwa trends za siasa za Bongo, kama unasaka uteuzi wowote, chama cha kujiunga nacho ni CCM tuu, yaani CCM ndio mpango mzima, Dr. Bashiru namfahamu toka UDSM, nikitaka uteuzi, ningeisha jiunga CCM siku nyingi!. Toka enzi za rais Mwinyi, huyu Dr. Husein Mwinyi ni school mate wangu Tambaza, ningekuwa msaka uteuzi, nimngemvaa Dr. Mwinyi anipaleke kwa baba. Rais Mkapa, mtoto wake ni Class mate wangu darasa moja na ni rafiki yangu, akiwa US nami nilikuwa US, Mkapa nakwenda kumsalimia kama baba fulani, hivyo ningetaka uteuzi, it was simple!. Enzi za JK hata kabla hajawa rais, JK anakuja UDSM kutangazia kugombea mimi ndio nili handle ile publicity. Riz One tunasoma naye sheria UD ni rafiki. Hotuba ya kwanza JK anahutubia UN GA, pale New York, mimi niko bennet na Riz, ningetaka uteuzi, it was very simple kupitia kwa Riz anipeleke kwa mshure!. Magufuli ndio usiseme!, kwanza ni home boy wangu, nikiwa na kazi zozote Geita, Biharamulo na Bukoba, nafikia Chato nyumbani kwa Magufuli, tena kuna siku nilikuwa na wageni fulani menu ikasumbua kidogo, mama Janet in person aliingia jikoni lirekebisha, hivyo kama kama ni kusaka uteuzi, it is as simple as ABC!. Kuna watu fulani humu ni wajinga wajinga wanadhani uteuzi is a very big deal kwa kila mtu, kuna watu wengi tuu, japo ni masikini wa kutupwa, hawana mpango wowote na uteuzi!, mimi sijawahi hata kuwa class monitor, hivyo nitafute uteuzi nikafanye nini?. Kuna watu hawataki hata kusikia kazi zozote za kitumwa na kutumwa kutumwa, wao wanapenda kujifanyia tuu mambo yao tuu kwa uhuru, hivyo naombeni sana wajameni, tuheshimiane!.
Paskali
Hakuna point hata moja hapa ni tumsifu yesu kiristo tu
 
In my opinion, unaweza fanya mema 1,000,000 lakini kwa:

- Kutoa amri ya moja kwa moja au isiyo ya moja kwa moja binadamu na Mtanzania mwenzako apotezwe au;

- Kutofanya, au kutokufuatilia upelelezi wa jaribio / majaribio ya kuuwa mtu / watu yaliotokea na yanayoendelea kutokea nchini au;

- Kukaa kimya wakati una uwezo wa kusimamisha vitendo vya utekaji vinavyoendelea hapa nchini au;

- Kuwakosesha wananchi haki yao ya kikatiba;

Yanafuta vizuri vyote unavyovifanya / yanavifanya visiwe na maana yoyote tena.

Unaweza kumnunulia Mama yako mzazi nyumba, gari na kila kitu hapa duniani. Lakini ukimtukana siku moja tu KILA kitu ulichomfanyia kimekosa maana MPAKA akusamehe yeye mwenyewe kwa moyo mmoja.

Wahanga wa mauaji yasiyo elezeka na watu wasiojulikana bado hawajasemehe. Wazazi, kaka, dada, wake, watoto wengi wamekaa kimya wapendwa wao wakiteseka chini ya huyo unaemsifia. Ukweli ni kwamba, hayawezi kukugusa mpaka yamfikie baba yako, kaka yako, mume wako, mke wako ndo utaonja maumivu yasiyoelezeka.

Hapo SGR na flyover hazitakuwa na maana kwako. Maisha ni watu, not materials. Life cannot be measured - it is priceless. One life is one too many.
 
  • Biashara zinakufa
  • Ajira hakuna
  • Korosho zinachipukia ghalani
  • Mzigo bandari umepungua
  • Maslahi ya wafanyakazi chini
  • Kilimo kinakwenda arijojo
  • Export ziko hoi bin taaban
  • Kila mara kuna taarifa za kutekwa watu
  • Wastaafu wanasaga vumbi mafao ya kukimbizanakimbizana
  • Sheria kandamizi za kuminya uhuru wa raia kila kukicha
  • Kodi hadi mawigi na taulo za akina mama
  • Uonevu kwa wapinzani
  • Abuse of power na kutoheshimu katiba ya nchi
  • Kuumiza raia kwa Kuwavunjia nyumba kibabe
  • Kamatakamata ya wafanyabiashara na kuwafungulia kesi za uhujumu uchumi kisha kuwaachia kwa kuwatoza pesa

Halafu kuna mtu anakaa chini kupoteza MB zake eti tumsifie, tumsifie kitu gani?, Wewe tuambie tumvumilie ifike mwakani tumtoe, huu si muda wa kusifianasifiana katupotezea our 5 good years bure!

Mazuri yake na mabaya yake ukiyaweka kwenye mzani utaelemewa kwa uzito wa ubaya!

Paskali tupishe, kama unampenda sana kanywe naye chai, lakini kiuhalisia amekuwa "mzinguaji" namba moja wa dira ya Taifa
Anayofanyiwa lissu peke yake , yanaonyesha picha halisi

Yaani sikutegemea paskali awe hivi

Hivi wakitaka kututeka , watatuteka wote !! ?

Mwisho aanze kuwateka na wanae maana nao , wataanza kumpinga !

Ukweli ni kama mwanga haufichiki !

Katika maisha yetu, kama ilivyo kwenye nguo, upo ule uzi unaojitokeza na kukera ambao ukikosea kuufumua au kuuvuta nguo nzima huraruka, au sweta zima hufumuka na kugeuka uzi. Somo hapa ni kuwa hasira na nguvu hazitatui kila tatizo".

Huu ujumbe umwendee!!
 
Wanabodi,

Mimi ni mdau mkubwa wa maonyesho ya Saba Saba, kwenye Saba Saba ya Mwaka huu, nimetembelea Banda la Wakala wa Nishati Vijijini, REA kwenye maonyesho hayo, nikazungumza Mwenyekiti wa Bodi ya REA, Mkurugenzi Mtendaji, Wajumbe wa Bodi, Menejimenti na wadau wa REA kuhusu kinachofanywa na REA.

Nilichokiona hapo REA, kiukweli kabisa na msema kweli ni mpenzi wa Mungu, Rais Magufuli is doing good for this nation, amedhamiria kufikia mwaka 2025, wakati anaondoka madarakani, kupitia umeme wa Stigler na REA, kila mkoa, kila wilaya, kila kata, kila kijiji, kila kitongoji na kila kaya itakuwa na umeme wa uhakika.

Kwa dhamira hii, kwenye kipindi changu, nikampongeza rais Magufuli kuwa ana dhamira safi na ya kweli ya kulikomboa taifa letu na kuliletea maendeleo.
Nikaandaa kipindi kimoja cha 60 min, lakini kwa vile hakuna TV nchini yenye kuweza kutoa nafasi ya kurusha 60 min, nikakigawana kipindi kwenye vipindi 2 vya 30min each.


Kufuatia pongezi hizo, kumbe kuna mwana jf aliangalia kipindi na kanianzishia thread

Mkuu the Retired, kwanza asante kuangalia kipindi changu, kwanza mimi Pasco, nafahamika kwa kuwa mkweli daima na very critical sio humu jf pekee, bali nafahamika hadi Bungeni, hadi Ikulu, kuwa Pasco ni mkweli daima, very bold na critical. Siku zote kwenye ukweli nausema ukweli jinsi vile ulivyo, kwenye mazuri napongeza, kwenye mabaya nakosoa, hivyo kwa hili la azma ya rais Magufuli kusambaza umeme kila kaya, hili ni zuri, la kustahili pongezi na kuungwa mkono na rais Magufuli apewe all the support kwa asilimia 100%.

Hivyo kwenye bandiko hili nina hoja zifuatazo
Magufuli is Doing Good For This Nation, Tutumie Positive Attitude Kumfanyia Assessment, Akifanya Mambo Mazuri, Apongezwe, Aungwe Mkono, Akikosea, Akosolewe! nitaziweka in number format
  1. Magufuli is Doing Good For This Nation, Rais Magufuli ndiye rais wetu, yeye sio malaika ni binaadamu tuu kama sisi na anaweza kukosea, kitu muhimu tunachokiangalia ni dhamira yake ya dhati kulikomboa taifa hili kutoka katika lindi la umasikini uliotopea na kuliletea maendeleo ya kweli ambayo ni maendeleo ya watu. Katika kuyatekeleza haya, naamini hakuna anaedhani kuwa rais Magufuli ni malaika, such that he must be perfect, he can't be wrong, it is not, rais Magufuli is a human being, hivyo anaweza kukosea, lakini kukosea huko kunaweza kuwa kumefanyika kwa nia njema, hivyo kuna mipango mingi ya rais Magufuli aliyoidhamiria kwa taifa hili ni mipango mizuri, ikifanikiwa, italibadili kabisa taifa hili, hivyo this man is real diong good for this nation, anastahili pongezi na kuungwa mkono, kumsifia kwa mazuri ni kujipendekeza?.
  2. Tutumie Positive Attitude Kumfanyia Assessment. Kwa vile nimeishasema toka mwanzo kuwa rais Magufuli sio malaika, wala hategemewi kuwa malaika, ni binadamu kama sisi hivyo kuweza kufanya makosa ya kibinaadamu kama binaadamu wengine wote, hivyo katika kumfanyia a fair assessment lets not concentrate on the negatives, lets look at hizi positives. Kuna type ya watu wanaitwa fault finders, wao kazi yao na kutafuta makosa tuu na kuangalia mapungufu, hata mtu ufanye mazuri mangapi wao hawayaoni na hawayazungumzi, lakini ukifanya kosa moja tuu, linageuka wimbo!. Tutumie ile yardstick ya kanuni ya maji nusu katika glass, ukiwa na negative atitude utasema maji ni half empty, ukiwa na positive atitude utasema maji ni half full, hivyo tukimfanyia rais Magufuli assessment with positive attitudes, utajikuta hata zile negatives zake, ukiwemo hoja ya udikiteta, utauchukulia positive kuwa ni a benevolent dictator, yaani dikiteta mwema anayetumia udikiteta kuletea maendeleo, kwa sababi kiukweli kabisa, hapa Tanzania tulipofikia, tulihitaji mtu kama huyu.
  3. Akifanya Mazuri, Apongezwe, Aungwe Mkono na Kupewa Support. Kwa vile rais Magufuli ni binadamu tuu kama sisi, Watanzania wote wazalendo wa kwenye wenye nia njema na taifa hili, wata wish rais Magufuli afanikiwe katika azma yake ya kulikomboa taifa hili toka katika lindi la umasikini uliotopea, kwa kujenga Tanzania ya viwanda, na kuipeleka Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati. Katika kutekeleza haya, Rais Magufuli akifanya mazuri, anastahili pongezi na kuungwa kuungwa mkono ili kumtia moyo, encouragement azidi kufanya mema na mazuri zaidi na zaidi. Kama Mungu tuu mwenyewe hana mpinzani lakini ni wajibu wa binadamu na viumbe wote kumwabudu Mungu, kumsifu, kumtukuza na kumwimbia nyimbo za shangwe sifa na utukufu, hivyo hakuna ubaya wowote, pale ambapo rais Magufuli anafanya mambo mazuri, apongezwe, asifiwe na kuungwa mkono. Hapa naomba kutoa angalizo, sijasema aabudiwe!, kuna watu wanataka kumwabudu, au kuna wale wa type ya yule kichaa wetu, kazi yake ni kusifuu tuu, mimi sizungumzii kumsifia kwa mtindo wa mapambio, bali kupongeza, kumtia moyo, kum encourage na sio kumvimbisha kichwa.
  4. Akikosea, Akosolewe!. Kama nilivyoeleza mwanzo, rais Magufuli sio malaika ni binaadamu, na hakuna binaadamu mkamilifu, no one is perfect, hivyo kuna maeneo rais Magufuli anakosea kama binadamu wengine, mimi na watu wa type yangu, ambao ni waumini wa ukweli, tukiongozwa na falsafa ya ukweli usemwe, siku zote tutaendelea kusema kweli daima, hivyo rais Magufuli kama binadamu, akikosea, akosolewe kwa heshima kwa kutumia lugha ya staha na kuambiwa ukweli, na sio kukosolewa kwa kubezwa, kudhalilishwa kwa lugha za machukizo. Kwa mtu yoyote au kiongozi yoyote, mwenye akili na busara, akikosolewa atafurahi na kujitathmini, na sio kukasirika. Utakuta sisi wakosoaji wa rais Magufuli na serikali yake, ndio watu tunaomsaidia zaidi rais Magufuli na serikali yake kuwa rais bora, kuliko wasifiaji na waimba nyimbo za sifa na mapambanio na naamini rais Magufuli anachukulia ukosoaji very positively, katika hili la ukosoaji, mimi naamini kuna tatizo la wapambe nuksi wanaomsingizia rais kuwa anachukia wakosoaji. Najitolea mfano mimi mwenyewe, kuna kazi fulani fulani nimezuiliwa kuzifanya nikielezwa kuwa ni amri kutoka juu, ati kuna siku fulani, sisi waandishi tulialikwa mahali fulani, mimi nikauliza swali fulani, kwa mtu fulani, ninaelezwa juu juu kuwa huyo fulani alikasirika sana na mtu wa visasi, eti kufuatia hasira hizo, ndio ameamrisha mimi nisiruhusiwe kufanya kazi fulani fulani!. Wapambe hao hawasemi ni amri kutoka wapi, hivyo mimi siamini kuwa ni kweli ni amri kutoka juu, kwa sabubu huko juu kuna watu wakikasirika, utavanish into a thin air bali ni wasaidizi wapambe tuu ndio wanatoa hizo amri na kusingizia ni amri kutoka juu, ukiisha ambiwa ni amri kutoka juu, utakwenda wapi kuuliza?. Hawa watu walionipa hiyo amri kudai kuwa ni amri kutoka juu, hawanijui, wakijua ukiambiwa tuu amri kutoka juu, utaogopa!, kumbe mwenzao ndio kwanza niko kwenye mchakato wa kufika huko juu kileleni amri zinakotokea na kumuliza "Mzee, jee ni kweli hii amri ya mimi sifanye hili na lile ni amri yako?!", nikijibiwa ni kweli, then nitakuwa sina jinsi bali ni kutundika tuu daluga na kutafuta shughuli nyingine ya kufanya kuendesha maisha yangu!. Nikiambiwa sii kweli, nawashukia hao watoa amri fake za kutoka juu hadi kumfikia huyu anayejiita amri kutoka juu.
  5. Jee ukiwa Critical, ni mkosoaji mzuri wa maeneo yenye makosa, siku rais Magufuli akifanya mazuri, ukampongeza, huwezi kumpongeza genuinely bila kuonekana unajikomba, unajipendekeza, ni njaa tuu ya kusaka uteuzi?. Naomba niwahakikishie wana JF, mimi Pasco, sio mwanachama wa chama chochote cha siasa, na kwa trends za siasa za Bongo, kama unasaka uteuzi wowote, chama cha kujiunga nacho ni CCM tuu, yaani CCM ndio mpango mzima, Dr. Bashiru namfahamu toka UDSM, nikitaka uteuzi, ningeisha jiunga CCM siku nyingi!. Toka enzi za rais Mwinyi, huyu Dr. Husein Mwinyi ni school mate wangu Tambaza, ningekuwa msaka uteuzi, nimngemvaa Dr. Mwinyi anipaleke kwa baba. Rais Mkapa, mtoto wake ni Class mate wangu darasa moja na ni rafiki yangu, akiwa US nami nilikuwa US, Mkapa nakwenda kumsalimia kama baba fulani, hivyo ningetaka uteuzi, it was simple!. Enzi za JK hata kabla hajawa rais, JK anakuja UDSM kutangazia kugombea mimi ndio nili handle ile publicity. Riz One tunasoma naye sheria UD ni rafiki. Hotuba ya kwanza JK anahutubia UN GA, pale New York, mimi niko bennet na Riz, ningetaka uteuzi, it was very simple kupitia kwa Riz anipeleke kwa mshure!. Magufuli ndio usiseme!, kwanza ni home boy wangu, nikiwa na kazi zozote Geita, Biharamulo na Bukoba, nafikia Chato nyumbani kwa Magufuli, tena kuna siku nilikuwa na wageni fulani menu ikasumbua kidogo, mama Janet in person aliingia jikoni lirekebisha, hivyo kama kama ni kusaka uteuzi, it is as simple as ABC!. Kuna watu fulani humu ni wajinga wajinga wanadhani uteuzi is a very big deal kwa kila mtu, kuna watu wengi tuu, japo ni masikini wa kutupwa, hawana mpango wowote na uteuzi!, mimi sijawahi hata kuwa class monitor, hivyo nitafute uteuzi nikafanye nini?. Kuna watu hawataki hata kusikia kazi zozote za kitumwa na kutumwa kutumwa, wao wanapenda kujifanyia tuu mambo yao tuu kwa uhuru, hivyo naombeni sana wajameni, tuheshimiane!.
Paskali

Pascal Mayalla sawa mkuu pongeza tu ila huku jikoni mambo siyo kabisaaa
1149466
 
Back
Top Bottom