lee Vladimir cleef
JF-Expert Member
- Feb 5, 2013
- 9,238
- 33,979
Pamoja na mapungufu ya awamu zilizopita kiutawala, lakini awamu hii ya tano haikufuata kabisa utawala Bora.
Watu wamekuwa wakifokewa hovyo hadharani, watu wamekuwa wakidhalilishwa hovyo hadharani, watendaji wa Serikali wamefukuzwa kazi mabarabarani, kwa kile kinachoitwa kutumbuliwa.
Wafanyakazi waliambiwa hatawaongeza Mishahara, madaraja Wala increment kwa sababu anajenga miundo mbinu na kuwaambia kuwa wafanyakazi kwanza sio wengi sana nchi hii,yeye anashughulikia miundombinu kwa ajili ya Watanzania wote. (Sasa hapa sijui watangulizi wake walikosea kuwapandisha Mishahara na wakati huohuo kuendelea kujenga miundombinu?)
Aliona kwamba wafanyakazi ni wachache kura zao hata wakimnyima hatoshindwa Uchaguzi wakati hali halisi ni kwamba kila mfanyakazi mmoja wa Tanzania ana watu kumi wanaohitaji msaada wake na wanajua machungu yake.
Sasa umefika wakati na yeye anasemwa hadharani. Tena anasemwa vibaya,mbele ya wananchi, kwa maneno ambayo nadhani hapendi kuyasikia, wapambe wake hawapendi kuyasikia. Yanamchoma, yanamkera, yanamchafua na yanamuaibisha.
Tundu Lissu Ni Mtundu kwelikweli, anapohoji habari za Ben Sanane hadharani anamuumiza sana, anapohoji kuhusu waliompiga risasi anamchoma sana Mzee ambae hajawahi kusemwa hadharani kwa miaka mitano.
Mzee Mwinyi, Mzee Mkapa na Mzee Kikwete walipojaribu kumsema walidhalilishwa sana kwa kuambiwa Wazee hao waache kuwashwawashwa. Akina Kinana, Membe na akina Makamba walipojaribu kumsema faraghani walidukuliwa na maneno yao yakawekwa hadharani Aibu ikawapata.
Leo hii Tundu Lissu anamsema hadharani asiyesemwa, kiasi cha kuwa mpole kuliko mtoto mchanga. Lissu anamsema kwelikweli tena kwa nguvu, tena mbele ya halaiki na mbele ya makamera na waandishi.
Yale yaliyokua yanaongelewa kwa kificho na kwa uoga, Lissu anayasema waziwazi. Kwa kifupi “mzee baba” ana hali ngumu. Hakufuata utawala wa sheria, sasa anaonja joto la jiwe.
Watanzania wenzangu, mtu huyu msifanye makosa ya kumrudisha tena madarakani, kwani awamu hii ni ya mwisho kuja kuomba kura. Akirudi hana cha kupoteza, mateso mliyopata awamu yake ya kwanza yatakuwa mara mbili na hayatakuwa na kikomo. Huyu hana tabia za kujuta kama Mkapa na Kikwete, hajali, mjivuni.
Kura yangu nitampa Tundu Lissu, jamaa zangu wameniahidi watampa kura Lissu, nakuomba na wewe mpe kura yako Lissu ajenge utawala wa sheria. Utawala Bora wenye kuheshimu utu wa kila mtu.
Uhuru, Hali na maendeleo ya watu.
Chagua Diwani CHADEMA, Mbunge CHADEMA na Rais Lissu.