Mada maalum ya ndege toka FB

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,678
698,788
JE, NDEGE INARUDI NYUMA?

Ndege nyingi za sasa zina mfumo wa kurudi nyuma #reverse' ambao mara nyingi hutumika kupunguza kasi wakati ikitua (#Braking).

Kwa baadhi ya ndege za 'Mapangaboi' #Propeller hutumia panga zake kubadili umbile (#angle) hivyo badala ya kuvuta hewa kwenda nyuma inasukuma kuelekea mbele na kusababisha ndege kupunguza kasi yake pale inapotua.

Hali kadhalika na kwenye injini zenye mfumo wa #Jet huwa zinafungua injini katikati na kubadili uelekeo wa hewa inayosukumwa nyuma kuvuja na kulazimishwa kuelekea mbele.

Baadhi ya Injini za mfumo wa 'jet nyingine zinafungua vimilango vyake vidogo katikati au nyuma ya injini.

Ndege nyingi kubwa zina mifumo mitatu ya kupunguza mwendo #braking ikiwemo

1>#Reverse' ya Injini au #Reverse_Thrust

2>'Brake' za matairi na

3> #Ground_Spoilers au #Speedbrake' ambazo ni bapa zinazo nyanyuka juu ya mbawa.

Hivi vyote mara nyingi hufanya kazi kwa pamoja ili kupunguza kasi ya ndege inapotua ili kusimama haraka kwakuwa hutua na kasi kubwa sana.
Kasi ya kutua ndege kama #MD11 ikiwa imejaa mzigo hata Gari yako yenye speed 260km/h haifukuzi.

Brake zote za kukinzana na upepo {spoilers na reverse thrust} husaidia kutozipa mzigo mkubwa 'brake' za matairi ambazo huweza kupasua tairi, kuharibika, kuwaka moto au mda mwingine kuteleza kama barabara #Runway ikiwa imetuama maji endapo kama zitatumika pekee bila msaada wa #brake' nyengine.

Licha ya kukinzana na upepo juu ya mbawa, 'spoilers/speedbrake' pia husaidia kukandamiza ndege chini hivyo tairi kushika barabara vizuri wakati zinakamata 'brake kupunguza mwendo.

Sasa kwanini ndege haitumii 'Reverse' kujitoa kwenye Maegesho?
badala yake inasukumwa kurudi nyuma (#Pushback) na vigari maalumu #Tow_Truck/#Tug

1>Kuepuka kelele kali za 'reverse'

2>Kuepuka ulaji mafuta

3>Kuepuka hatari ya ndege kugongana na vitu vingine nyuma.

4>Kuepuka uharibifu wa injini kwa kunyonya taka na vumbi kwasababu upepo wa 'reverse' hutokea pembeni ya injini kwa kasi kubwa kuelekea mbele ya injini.

5> Reverse ni mfumo wa dharura ambao kiufundi haishauriwi kutumika hovyo kwasababu hewa yake inapitia sehemu za injini ambazo ni rahisi kupata uharibifu.

#Admin
Credit
#boldmethod
FB_IMG_1683967037004.jpg
 
"Leo tumefurahi kupokea ujumbe wa makampuni 25 yanayoongoza kwa watalii nchini China. Ujumbe huo umeambatana na vyombo 6 vya habari mashuhuri kutoka nchini humo na umewasili na Air Tanzania kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Amani Abeid Karume, Zanzibar ukitokea Guangzhou, China"
(Jana)

Air Tanzania Company Limited
FB_IMG_1683967280283.jpg
 
IPI KAZI YA 'FLAPS' KWENYE NDEGE

VISAIDIZI VYA KUPAA
(Lifting Devices)

Kiufundi ndege inahitaji njia fupi ya kuruka na kutua ili ifanye kazi ndani ya mipaka ya kiwanja.
Lakini mwendo mdogo hauwezi kunyanyua ndege ikihitaji kupaa wala kushikilia ndege hewani ikitaka kutua kwasababu 'pressure' ya hewa inayohitajika kunyanyua mbawa chini pia itakuwa ndogo.

Hapo ndipo wataalamu wa maumbohewa (Aerodynamics) wakabuni vifaa vya kusaidia ndege kuruka na kutua katika mwendo mdogo.
Vifaa hivyo ni kama 'Flaps, 'Slats na 'Spoilers' /Speedbrakes n.k

#FLAPS
Ni sehemu inayotembea nyuma ya mbawa(trailing edge) ambayo hupinda kuelekea chini au kuchomoka nyuma na kupinda kuelekea chini.
Wakati wa kupaa 'Flaps' hupinda chini kwa nyuzi kadhaa (degrees°) ili kusaidia kuongeza pressure zaidi ya kusukuma mbawa juu (lift).
Flaps kwa urukaji huongeza kiasi ukubwa wa bawa na kulazimisha hewa inayopita chini ya bawa kugonga kunyanyua bawa juu (action & reaction)

Wakati wa kutua 'Flaps' hupinda chini kwa nyuzi nyingi zaidi kuongeza ukubwa wa mbawa na kubadili kuwa umbo ambalo linahifadhi 'pressure' kubwa zaidi na kuburuta (drag) ili kutua kwa mwendo mdogo pasipo kupoteza mnyanyuo (lift).

#SLATS (pia Slots)
Ni sehemu inayotembea mbele ya mbawa.
Hizi ni kama bapa nyembamba za chuma zinazokunjuka na kufunga mbele ya mbawa ili kuongeza ukubwa na ufanisi wa hewa kupita.
'Slats' mara nyingi zinatembea pamoja na 'Flaps'
Hii mara nyingi ni Kwa ndege kubwa.

Kuongezeka ukubwa wa mbawa husaidia ndege kuruka na kutua kirahisi katika mwendo mdogo zaidi.
'Flaps na Slats' hutumika mara nyingi kwenye kuruka na kutua.

#SPOILERS/SPEEDBRAKE
'Spoilers' ni paneli zilizowekwa juu ya mbawa.
Mara nyingi ndege inapogusa chini wakati wa kutua huwa zinanyanyuka juu ya mbawa.
Kazi yake ni kukinzana/kuvuruga/kukinga hewa inayopita juu ya mbawa ili kuongeza mburuto kwenye ndege (drag) iweze kupunguza mwendo kwa haraka zaidi.

Pia zinasaidia kuongeza uzito wa ndege kwa kuikandamiza kwenye barabara ili breki za tairi zikamate vizuri inapotua
'Spoilers' au 'SpeedBreak' pia hutumika angani kama kupunguza kasi ya ndege kwa dharura/haraka.

Katika ukataji wa kona angani, baadhi ya 'Spoilers' inaweza kusaidiana automatiki na vielekezi vingine kama #Aileron au #Flaperon.

Kumbuka 'Spoilers' na 'Slats' sio rahisi kukuta kwenye ndege zote hasa ndogo kwakuwa hazina mwendo mkubwa wa kupaa na kutua.

Lakini pia Ndege kubwa (heavy aircraft) zinahitaji kupunguza mwendo haraka wakati wa kutua hivyo mara nyingi zinatumia brake tatu kwa wakati mmoja ili kusimama haraka,
1>'Spoilers'(speedbrake),
2>'Reverse' za injini (Thrust reverser) na
3>'Brake' za tairi.

NB:
Lengo la Elimu hii ni kutoa mwangaza mdogo tu wa awali.
Tumia muda wako kujisomea kiundani.
FB_IMG_1683967345078.jpg
 
NDEGE HUTUMIA MAFUTA GANI?

Aviation Fuel ni mafuta yanayotumiwa kwa kuendeshea injini za ndege.
Kimsingi zipo kama aina nne za mafuta zinazotumika katika usafiri wa anga.

1> Jet A-1 ambayo ambayo kwa uhalisia ni mafuta ya taa

2> Jet B, Mchanganyiko wa mafuta ya taa na petroli

3> Avgas ambayo ni kama petrol ya ndege.

4> Biokerosene ambayo ni mchanganyiko wa mafuta ya taa na mimea.

1> #JetA_1

Mafuta haya pia huitwa JP-1A hutumiwa ulimwenguni kote katika injini za turbine (injini zenye mfumo wa 'jet na turboprops')
Haya ni kama mafuta ya taa yaliyosafishwa kwa uangalifu ambayo yapo fanisi kuwaka kwenye joto la kiwango cha 38 °C na kiwango cha chini -47 °C.

Mafuta haya taa yanasafishwa kwa ustadi mkubwa sana na baada ya kusafishwa yanachanganywa na kiwango kadhaa cha viambatanishi vinavyo wezesha kuwaka katika hali iliyodhibitiwa, kuzuia viumbe kukua ndani yake kama fangasi, bakteria, pia kuzuia kuganda kwenye ubaridi wa -30°C n.k
Ndege za kijeshi mfano za NATO hutumia mafuta haya na viongezeo maalum zaidi na kuitwa jina la #Jet_Propellant_8 (JP-8).

2> #JetB

Mchanganyiko wa mafuta ya taa na petroli.
Mafuta haya hutumiwa sana katika ndege za kijeshi.
Mchanganyiko huu maalum wa daraja la Jet B, pia huitwa JP-4 ambapo Petroli asilimia 65% na Mafuta ya Taa asilimia35%.
Haya hutumiwa zaidi kwenye sehemu zenye ubaridi sana kwa sababu yanaweza kuwaka kwa joto la 20°C.
Lakini pia injini lazima ziwe zimeundwa maalum kwa matumizi ya mafuta haya.

3> #AvGas (Aviation Gasoline)

Hii ni kama Petroli maalum kwaajili ya ndege hasa zile zenye injini za piston.
Mafuta haya katika usafiri wa anga kawaida hutumiwa tu katika injini za Piston hasa ndege za michezo,ndege ndogo za kibinafsi ambazo zinahitaji mafuta ya kuongezwa kiasi kikubwa cha octane.

Kwahiyo Avgas ni kama petroli iliyoongozwa octane 100 ili kukidhi mahitaji haya.
Hapa Ulimwenguni ni aina ya #Avgas100LL tu ambayo bado inapatikana kirahisi na ndege zilizo na injini ya petroli tu ndiyo zinaweza kuendeshwa na avgas, ndege zinazotumia turbine au zile zilizo na injini za mfumo wa kerosene/dizeli zinahitaji jetA.

Kwa kuwa avgas ni ghali kutokana na kiwango cha chini cha uzalishaji, njia ndefu za usambazaji, na udhibiti wa ubora.

4> #Biokerosene

Biokerosene mchanganyiko wa mafuta ya taa na nishati ya mimea ambayo imeanza kutumiwa na tasnia ya usafiri wa anga.

Tafsiri kutoka mitandaoni.

Admin,
Aviation media Tz

Like & share.
FB_IMG_1683967427786.jpg
 
Jumba la kifahari la muigizaji John Travolta lenye gharama ya dola milioni $10 huko Ocala, Florida si tu nyumba ya kifahari ya vyumba vitano, lakini pia ni uwanja wa ndege wa binafsi.
Nyota huyo wa Grease alijenga nyumba hiyo kwenye makazi ya kipekee ya Jumbolair Aviation Estates miaka ya 1990.
Mali hiyo inajumuisha sio tu uwanja wa ndege, lakini nafasi ya kuegesha jeti zake mbili nje ya nyumba yake na kwa dakika chache anaingia njia ya kurukia kutokea kwa mlango wa mbele mara nyingi akipaisha ndege mwenyewe.

Soma zaidi:
www.hellomagazine.com/homes/490618/john-travoltas-florida-home-also-private-airport/%3fviewas=amp
FB_IMG_1683967519318.jpg
 
Like & share.View attachment 2620062
Interesting
 
Ndege aina ya Hawker 900XP, PK-LRU, imechochora nje ya njia ya kurukia namba 23 baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Maleo (WAFO), Indonesia hapo jana.
Ndege hiyo ilisimama umbali wa mita 200 hivi kutoka mwisho wa njia ya kurukia ndege na kupata uharibu mkubwa.
Hakuna majeruhi aliyeripotiwa kati ya abiria wanne na wahudumu wanne.

Chanzo:
@aviation safety network
ASN
FB_IMG_1683967718143.jpg
FB_IMG_1683967714889.jpg
FB_IMG_1683967711632.jpg
 
Jumba la kifahari la muigizaji John Travolta lenye gharama ya dola milioni $10 huko Ocala, Florida si tu nyumba ya kifahari ya vyumba vitano, lakini pia ni uwanja wa ndege wa binafsi.
Nyota huyo wa Grease alijenga nyumba hiyo kwenye makazi ya kipekee ya Jumbolair Aviation Estates miaka ya 1990.
Mali hiyo inajumuisha sio tu uwanja wa ndege, lakini nafasi ya kuegesha jeti zake mbili nje ya nyumba yake na kwa dakika chache anaingia njia ya kurukia kutokea kwa mlango wa mbele mara nyingi akipaisha ndege mwenyewe.

Soma zaidi:
www.hellomagazine.com/homes/490618/john-travoltas-florida-home-also-private-airport/%3fviewas=ampView attachment 2620064
watu wanaishi aisee, umenikumbusha kazi ya ndoto yangu pindi nikiwa mdogo
 
JE, VITI GANI NI SALAMA ZAIDI NDANI YA NDEGE?

Akiandikia CNN Travel, mtaalamu wa masuala ya usafiri wa anga Doug Drury alisema kwamba “hakuna haja ya kuwa na wasiwasi kuhusu usalama unapopanda ndege ya abiria” akithibitisha kwamba “usafiri wa anga ndio njia salama zaidi ya usafiri.”

Kulingana na Bw Drury ametoa ushauri wake kuhusu mahali salama pa kukaa kwa ujumla wakati wa safari. Aliiambia CNN kwamba viti vya kati vya safu ya nyuma kwenye ndege ilikuwa mahali pazuri pa kukaa, akiongea kitakwimu, Mtaalamu huyo amechambua utafiti wa TIME uliochapishwa mwaka wa 2015.

Utafiti huu uliangalia data ya ajali za ndege kwa muda wa miaka 35, ili kubaini viti salama zaidi ambavyo ilionekana viti vya kati katika safu ya nyuma huwa vinasalia salama mara nyingi katika ajali zilizotokea.

Chanzo:
FB_IMG_1683968045939.jpg
 
Azul Embraer E-195-E2 (PS-AED ya mwaka 2020) ilipitiliza Nje ya njia ya kutua namba 17 katika uwanja wa Salvador de Bahia (SBSV), Brazili hapo Jana.
Mashuhuda wanasema mvua mkubwa ilinyesha.
Ndege hiyo namba #AD4372 ilitoka Sao Viracopos. Bado hakuna taarifa ya majeruhi.

@Aviationbrk
FB_IMG_1683968118546.jpg
FB_IMG_1683968113873.jpg
FB_IMG_1683968107856.jpg
 
JE, NDEGE INARUDI NYUMA?

Ndege nyingi za sasa zina mfumo wa kurudi nyuma #reverse' ambao mara nyingi hutumika kupunguza kasi wakati ikitua (#Braking).

Kwa baadhi ya ndege za 'Mapangaboi' #Propeller hutumia panga zake kubadili umbile (#angle) hivyo badala ya kuvuta hewa kwenda nyuma inasukuma kuelekea mbele na kusababisha ndege kupunguza kasi yake pale inapotua.

Hali kadhalika na kwenye injini zenye mfumo wa #Jet huwa zinafungua injini katikati na kubadili uelekeo wa hewa inayosukumwa nyuma kuvuja na kulazimishwa kuelekea mbele.

Baadhi ya Injini za mfumo wa 'jet nyingine zinafungua vimilango vyake vidogo katikati au nyuma ya injini.

Ndege nyingi kubwa zina mifumo mitatu ya kupunguza mwendo #braking ikiwemo

1>#Reverse' ya Injini au #Reverse_Thrust

2>'Brake' za matairi na

3> #Ground_Spoilers au #Speedbrake' ambazo ni bapa zinazo nyanyuka juu ya mbawa.

Hivi vyote mara nyingi hufanya kazi kwa pamoja ili kupunguza kasi ya ndege inapotua ili kusimama haraka kwakuwa hutua na kasi kubwa sana.
Kasi ya kutua ndege kama #MD11 ikiwa imejaa mzigo hata Gari yako yenye speed 260km/h haifukuzi.

Brake zote za kukinzana na upepo {spoilers na reverse thrust} husaidia kutozipa mzigo mkubwa 'brake' za matairi ambazo huweza kupasua tairi, kuharibika, kuwaka moto au mda mwingine kuteleza kama barabara #Runway ikiwa imetuama maji endapo kama zitatumika pekee bila msaada wa #brake' nyengine.

Licha ya kukinzana na upepo juu ya mbawa, 'spoilers/speedbrake' pia husaidia kukandamiza ndege chini hivyo tairi kushika barabara vizuri wakati zinakamata 'brake kupunguza mwendo.

Sasa kwanini ndege haitumii 'Reverse' kujitoa kwenye Maegesho?
badala yake inasukumwa kurudi nyuma (#Pushback) na vigari maalumu #Tow_Truck/#Tug

1>Kuepuka kelele kali za 'reverse'

2>Kuepuka ulaji mafuta

3>Kuepuka hatari ya ndege kugongana na vitu vingine nyuma.

4>Kuepuka uharibifu wa injini kwa kunyonya taka na vumbi kwasababu upepo wa 'reverse' hutokea pembeni ya injini kwa kasi kubwa kuelekea mbele ya injini.

5> Reverse ni mfumo wa dharura ambao kiufundi haishauriwi kutumika hovyo kwasababu hewa yake inapitia sehemu za injini ambazo ni rahisi kupata uharibifu.

#Admin
Credit
#boldmethodView attachment 2620053
Hakuna sauti huwa inaniudhi kuisikia kama ndege ikitua halafu rubani anafanya reverse thrust
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom