Machinga wa Kariakoo Dar kuhamishiwa Jangwani

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,620
55,261
Wafanya biashara ndogondogo (Machinga), watahamishiwa katika Viwanja vya Jangwani ili kupunguza msongamano Mjini.

Tayari Machinga wameshatangaziwa Jumatatu kuhamia Jangwani. Tayari Sehemu watakayo hamia imeshatengenezwa.

Mvua ikishaanza kunyesha, sijui kama jangwani kutafanyika biashara sababu hata Wananchi waliokuwa Wakiishi Jangwani wamehamishiwa Mabwepande.

Hii habari nimepewa na Jamaa yangu.

Wakuu hali si shwari mitaa ya Kariakoo.

Mgambo wa Jiji wakishirikiana na Polisi wametanda kila kona ya mitaa ya Kariakoo kupambana na wamachinga ambao wameambiwa kuanzia leo Jumatatu waende Jangwani kufanya biashara zao.

Baada ya tamko hilo wamachinga wamekataa wamedai HAIWEZEKANI tutapambana nao.

Nitaendelea kuwaletea chochote kitakachojiri!
 
Kama ni kweli hatuna serikali.Pale jangwani si sawa na kivukoni jamani.Tutazika machinga wa kutosha mvua zikianza.Au serikali inataka kuangamiza machinga nchini.!!!???
 
Wangeanza kwanza kuhamasisha waitumie Machinga Complex ipasavyo.

Tatizo ni kutokutenga miji mipya kisasa.
Kuna maeneo kama yakitengwa vizuri basi hata maduka makubwa ya jumla yangeweza kufunguliwa huko
Idadi kubwa ya wanaoenda kufanya shoping kariakoo sio wafanyakazi wa mjini.Wengi wakinunua wanasepa zao home.
Sasa ingetengwa kwamba ene jingine kama kitovu cha biashara basi naamini watu wange change mind set zao na kwenda huko kama option.

Mie bado naamini kama akitokea muwekezaji makini sana na mjanja akajenga mji wa biashara wa mfano kwa wafanyabiashara wadogo,basi naamini hata kama ni Chanika huko au Mvuti basi watu kibao wataenda huko.
Kwani Mlimani City kuna mtu alijua kama pale watu wataenda kununua bidhaa?lakini leo hii ndio habari ya mjini
 
Wakuu hali si shwari mitaa ya Kariakoo.

Mgambo wa Jiji wakishirikiana na Polisi wametanda kila kona ya mitaa ya Kariakoo kupambana na wamachinga ambao wameambiwa kuanzia leo Jumatatu waende Jangwani kufanya biashara zao.

Baada ya tamko hilo wamachinga wamekataa wamedai HAIWEZEKANI tutapambana nao.

Nitaendelea kuwaletea chochote kitakachojiri!
 
Wamachinga wamelelewa hivyo toka mwanzo, sasa wameshaona ni halali yao kufanya biashara kwa staili hiyo. Hawawezi kuhama kirahisi hivyo.
 
polisi wameamua kuondoka kuwachia machinga waendelee kupanga biashara zao.
 
Ili Dar es salaam iwe safi ni pamoja na Sisi raia kuwa pamoja na wasafisha jiji. Hawa watu wasumbufu sana barabara nzima wamepanga bidhaa.

Mi naona uchaguzi uishe tu ili wapigwe. Huwa nawashangaa wananchi wanao nunua bidhaa zilizo chini tena sehemu chafu!
 
Aliyetoa agizo waende jangwani pale si stand ya DART ama jangwani ya wapi.
 
Wajeuri sana hawa machinga wanapanga bidhaa zao mpaka barabarani alafu hata ukiwapigia honi wakupishe wanatoa matusi alafu hawasogei. Nchi hii hovyo sana.
 
Tatixo viongozi wetu hawasomagi alama za nyakati au huwa wanatumika na wenye maduka. Katika siku zoote waache kiwakimbiza waje kuwatimia leo ilhali tukijua keshokutwa ni sikukuu ina maana biashara ndio imechanganya. Kwann wasifanye zoezi hili wakati mwingine baadae? Au walikuwa wapi mwezi mmoja nyuma????
 
Serikali dhaifu, inashindwaje kuwatimua hawa watu, tumechoka barabara hazipitiki kisa machinga, UJINGA
 
Back
Top Bottom