Maboresho ya JF - 2019

Maxence Melo

JF Founder
Staff member
Feb 10, 2006
4,235
13,436
Wakuu,

Naomba kuwafahamisha kuwa siku si nyingi tutafanya maboresho kidogo kwenye mwonekano na matumizi ya JF.

Lengo ni kuzingatia mahitaji ya wadau (ambayo yamekuwa yakiombwa), kuendana na mabadiliko ya kiteknolojia na kuimarisha zaidi uimara wa platform.

Aidha, maboresho hayo yataenda hadi kwenye kuimarisha miundombinu (infrastructure) ili kuongeza uimara wa kukabiliana na hali yoyote.

Mabadiliko mengine ya aina hii yanaweza kufanyika 2021 au 2022.

Maboresho ya Miundombinu yamepangwa kufanyika usiku wa manane wa tarehe 26/03/2019. Ni nyongeza ya servers kuongeza ufanisi zaidi.

Maboresho upande wa mwonekano (UI) yatafanyika Machi 30, 2019.

Asante kwa ushirikiano mnaoendelea kutupa.

=====
Edit:
Maboresho yote yamekamilika 100%.

Asanteni kwa uvumilivu
 
Thumbs down inaharibu saikolojia ya mtu. Kuna watu wanaandika nyuzi ambazo zinaonyesha wazi hawana watu wa kuongea nao ikitokea na thumb down ikawepo na akazipata nyingi huyu mtu atajiona ametengwa na jamii zote, aliyopo na ya mtandaoni.

Wanaweza wakajidhuru.

Kwakua kutojulikana humu ni kwingi mtu hata akijiua tunaweza tusijue kabisa hivyo hakuwezi kua na takwimu za kitu kilichosababishwa na thumb down.

Pia isifananishwe thumb down ya FB na ya JF.
Maamuzi ni yenu
 
Wakuu,

Naomba kuwafahamisha kuwa siku si nyingi tutafanya maboresho kidogo kwenye mwonekano na matumizi ya JF.

Lengo ni kuzingatia mahitaji ya wadau (ambayo yamekuwa yakiombwa), kuendana na mabadiliko ya kiteknolojia na kuimarisha zaidi uimara wa platform.

Aidha, maboresho hayo yataenda hadi kwenye kuimarisha miundombinu (infrastructure) ili kuongeza uimara wa kukabiliana na hali yoyote.

Mabadiliko mengine ya aina hii yanaweza kufanyika 2021 au 2022.

Asante kwa ushirikiano mnaoendelea kutupa.
Mkuu ombi letu la muda mrefu la kuwa na jukwaa maalum la ushirikina na mambo ya giza mlikumbuke tafadhali

Jr
 
usisahau malalamiko yangu ya muda mrefu kuwa kila unapochangia uzi tayari unakuwa ume "subscribe" huo uzi, inasumbua sana kupata notification ya kila mchangiaji...tafadhali fikirieni hili pia
Maxence Melo

Sent using Jamii Forums mobile app
Hilo tatizo lilikuwepo mwanzoni kwa upande wangu ila liliisha kadri siku zilivyodhidi kusonga mbele. Jitahidi u-subscribe kila jukwaa na utaweza kupata notification ya uzi mpya kila ukiwekwa jukwaa husika.
 
Back
Top Bottom