Kwa wafugaji wa kienyeji wa wanyama na ndege huko vijijini kwetu, kuna vitu au maarifa ya kienyeji ambayo huwa wanatumia, naomba tuyajadili na kujulishana pia tuonyeshane kama kweli yanafanya kazi. Na kama ni muhimu kuyaendeleza kwa manufaa yetu.
Mfano; Kuku mgeni akiletwa nyumbani, nimekuwa nikiona watu wakinyoa manyoya kisha kuyachoma motoni, wanamzungusha kuku na baadae wanamwachia. Mkulima huamini kuwa kwa kufanya hivyo kuku hawezi kutoroka. Juzi nimeipata mpya, eti vitoto vya bata ili visife, wenyewe huwa wanavivuta shingo mapema,wanaamini kwamba vinapona vyote.
Vitu ni vingi vinafanyika huko vijijini, ukikijua tupa hapa ili tujadili.