Lissu kamnyamazisha mtu?

Hongera kwa kuwa na a.k.a hiyo mkuu, ila mimi ni jina langu kabisa la ukoo.
Mkuu a.k.a Lwambo, mlichokuwa mnajadili ni nani zaidi kati ya Zitto na Lissu, wewe ukadai kuwa Zitto ni zaidi, mimi ndio nikasema kuwa Zitto si lolote kwa kuwa hata hoja anazotoaga bungeni sio zake, anapewa tu, ndio ilikuwa argument hiyo.
Mjuni Lwambo a.k.a yangu ni Lwambo Lwanzo Makiadi...

kwani kuna tatizo gani akiwa anatoa madongo ambayo sio yake ila kwa faida ya wote? Mbona akina Slaa walisema waziwazi wanapewa na watu walio usalama wa taifa kuibua hoja?? sioni tatizo la mtu yeyote bungeni kusema hoja ambayo hata kama sio yake, unless ameiiba na mwenye hoja alitaka aiseme yeye..............that one I wont accept

bado sijaona tatizo,
 
Tuwe na subira tungojee kesi ianze kusikilizwa hafu siku iktoka hukumu ndiyo tujue nani ni nani!
 
Critically ! Lissu akili nyingi na kiongo anazo zi wa kuigwa ktk machambuzi yakinifu. Zz bado sana hajui kuwa concensus ni nguzo ya utawala bora? Mwana mpotevu alitaka urithi kwa babaye badae akala mabaki na ...
 
Critically ! Lissu akili nyingi na kiongozi wa kuigwa ktk machambuzi yakinifu. Zz mtalamu wa kupewa asome tu, bado sana wala hajui kuwa concensus ni nguzo muhimu kwa utawala bora ? Eti wabunge wa Kigoma wahamie kwake kwa lipi ? Zz apewe dawa labda ana maralia kichwani. Mwanapotevu alipotaka urithi kwa babaye badae alikula na ...
 
Baadhi Wanajamvi kweli mmepotoka. Yaani zile harakati za kupambana na CCM zimefifia, siku hizi ni Zito Kabwe. Kila kukicha ni ZZK, je mnataka kutuamnisha kuwa huyu bwana ana nguvu kuliko CCM? ZZK ni mtu mmoja tu, keshafukuzwa CHADEMA it is over, tuendelee na mambo mengine.
 
Huyu Mtu habari zake hata huhitaji kuzitafuta maana zimejaa kila sehemu. Mie inatosha kufungua JF au Group langu la FB na unakuta kila kitu. Ukiona kimya, basi ujuwe hakuna kitu. Mie muda wa kwenda kupekua huwa sina na sipendi ila itokee tu kama Sheick mpenda Neema za Allah.

Sasa nkizikuta kwenye JF au FB wall ya group letu, ni dhambi kuzitumia? Na hapa nimeweka swali tu kuwa tangu Tundu Lissu amtege mtu wako na yeye akategeka haswaaa na AKAROPOKA ovyo.........
Hii inanikumbusha ile story ambayo Mama alienda kumshitaki Baba na Shahidi akawa binti yao na Binti akaanza kutoa ushahidi "...... Baba huwa anampiga Mama na siku nyingne usiku, Baba ananyenyuka na kumlalia Mama, Mama analia, ila Baba anamlalia tu na kumpiga, akimaliza anakuwa hoi kwa kuhema haraka haraka....." Kumtaja Mkono na Rostam Azziz lilikuwa kosa la Mwaka ambalo alitegwa. Alijitahidi afute haraka haraka ila hao Troroller unaowasema, ndiyo wakawa wameshawahi kum-Copy na ku-Paste kwenye mitandao.

Mi-CCM nayo ikakazania kumshambulia Mbowe bila kujua wanamjeruhi Advocate wao na King Maker. Poleni.

BTW: Mie na Complex wapi na wapi? Wee huna maana na unanipotea muda wangu, ngoja niendelee na Gongo langu.
.........
...........Mkuu umepotea sana
 
Huyu jamaa alionywa sana na watu kila sehemu akae kimya ila akagoma. Nakumbuka hata Pasco wa JF aliandika barua ya wazi kumuonya huyu jamaa ila akagoma na akaendeleza vita na kila mtu ndani ya Chadema kasoro tu watu wake.

Nampa sana heshima Dr. Kitila Mkumbo kwa kusikiliza ushauri na kukaa kimya na kugoma hata kwenda Mahakamani kupinga kufukuzwa kwake kwa sababu kwa kufanya hivyo, kuna siku itafika na Mkumbo anaweza kuja juu sana ndani ya chama chake cha zamani. Mifano ipo mingi sana kwani Binadamu tunakosea na kusameheana. Kitila ni jembe lililowekwa pembeni na limetulia tuliii likisubiri tu muda wake uwadie lifanye mambo yake. Nategemea siku moja itakuwa hivyo.

Ila kuna jamaa ambaye aligoma kabisa kusikiliza na akaamua kuwasha moto wake ambao CCM waliufurahia sana. Chadema kila walichojitahidi kumuweka chini atulie, jamaa aliruka viunzi mithili ya Swala anayefukuzwa na Chui. Baada ya Chadema wote kushindwa, kama ile hadithi ya jinsi Sungura alivyokatwa mkia na Kobe, nyuma yake alikuwa muda wote anavizia Tundu Lissu na kisu chake mkononi. Kama Chui anavyokimbia, Tundu Lissu aliendelea kumfukuza adui yake kwa kuwa na imani, kila hatua akiruka, anazidi kumsogolea na mwisho, adui huyo baada ya kufikiri kasharuka viunzi vyote na yuko salama kwa msaada wa kichaka kirefu kilichomficha asionekane, Tundu Lissu akaja na Bomu mkononi na kulirusha kwenye kichaka hicho. Huku akiwa kashajaa misifa ya kushangiliwa kwa kumgaragaza Tundu Lissu na Chadema kwenye mbio za Savana, ghafla akasikia bomu limelipuka.

Mlipuko wa Bomu hilo, ulimfanya asiwe mwangalifu tena na akajikuta anaanza kukimbia ovyo bila kujipanga. Kama alivyo Nungunungu, akaanza kurusha mishale yake ovyo bila kuangalia hiyo mishale inaweza kumchoma hata Tembo aliyepo pembeni mwake au Mbongo wanaoweza kumtetea. Mbogo hao wakampa ONYO kali sana aache kurusha mishale ovyo na aliyorusha aukusanye na kuichoma. Ila bahati mbaya sana, watu wa JF walishaikusanya mishale hiyo na kubaki nayo kama ushahidi. Wapenzi wa CCM wakaanza kuitumia mishale hiyo kuwashambulia Chadema na magazeti yakaandika kila siku na kumsifia mtu huyu. Muda huo, kila mshale ukirushwa kwa chadema, kumbe katikati wamesimama hawa Mbogo ambao ni watetezi wake. Watetezi wakaja na maneno meengi kuwa hawajamtetea na hata kuitetea Chadema au kuisaidia. Ila tatizo likawa kubwa kwani CCM waliendelea kushambulia bila kujua kuwa wanawashambulia Mbogo ambao ni ndugu zao.

Masikini mtu huyu hakujua kuwa Tundu Lissu bila mabavu, hatakiwi kujibiwa kichwa kichwa. Alitegegwa kama Global Publisher walivyomtega Kapuya na wakamnasa akipekechwa na Kibinti kilicholowa Kikwapa. Alikurupuka na kuanza kumwaga MBOGA kwa kudhani Tundu Lissu kamwaga UGALI. Kumbe Tundu Lissu kamwaga ugali wa Advocate Mkono na kumpa Binadamu Mboga ambayo nayo ilikuwa ya Mkono. Amekuja kushtuka, kashajifunga goli.

Tangu siku hiyo, hadi leo hii naona amekuwa kimya kabisa. Hakuna cha FB wala JF kwa kutumia jina lake. Nashindwa kuelewa kupotea kwake ni kwa sababu ya kosa hilo au ndiyo ile wanasema "ukiona Kobe kainama, ujuwe anatunga sheria....." Labda atakuja kwa Ari Mpya, Nguvu Mpya na ....... Ngoja tusubiri siku ya Mahakama atacheza film gani.

Ngoma ikivuma sana.......... Mungu ampe maisha marefu ili siku moja aje akiri makosa.
Wanabodi, mimi nilidhani Lissu hatarejea
Kwa mliomsikia Tundu Lissu kwenye Hard Talk, unadhani atarejea nchini? Mimi sina hakika na akirejea, atakuwa ni shujaa kuliko hata Nelson Mandela!

Wanabodi,

Hili ni bandiko la swali, "Kwa Mliomsikia Tundu Lissu Kwenye Hard Talk, Jee Unadhani Atarejea Nchini?. Mimi kwa upande wangu, I seriously doubt kama atarejea, na ikitokea kweli akarejea, then Tundu Lissu atakuwa ni shujaa mwenye uthubutu na ushujaa mkubwa kuliko hata ushujaa wa Nelson Mandela!.

Nimesema hivyo kwa sababu nimemsiliza kwa makini Tundu Lissu, him being a Lawyer, kwa yale aliyoyasema, kwa tuhuma alizoshusha bila ushahidi, I seriously doubt if Tundu Lissu will ever return home during this era, na ikitokea kweli akarejea, then Tundu Lissu atakuwa ni shujaa kuliko Nelson Mandela.
Hongera zake.

Paskali
Final Update
Tundu Lissu leo amerejea nyumbani Tanzania, hivyo naomba kuthibitisha humu kuwa Tundu Lissu ni Jasiri na Shujaa Kuliko Nelson Mandela.

Hivyo sasa, kufuatia kurejea huku, ule ushauri wangu nilioutoa kwake kabla hajashambuliwa, sasa utekelezwe.

Uchaguzi 2020 - Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha Uwezo Zaidi ya Magufuli!

Shujaa Kamanda Tundu Lissu, karibu nyumbani.
Mungu ni mwema amekutendea muujiza, hivyo endelea kutimiza ndoto yako, Mungu aliyekuponya ni Mungu mwenye uwezo, anaweza kabisa kulifanya "Jiwe Walilolikataa Waashi, Likafanywa Jiwe Kuu la Pembeni"

I wish him all the best.
Paskali
 
Huyu jamaa alionywa sana na watu kila sehemu akae kimya ila akagoma. Nakumbuka hata Pasco wa JF aliandika barua ya wazi kumuonya huyu jamaa ila akagoma na akaendeleza vita na kila mtu ndani ya Chadema kasoro tu watu wake.

Masikini mtu huyu hakujua kuwa Tundu Lissu bila mabavu, hatakiwi kujibiwa kichwa kichwa kwa kudhani Tundu Lissu kamwaga UGALI. Kumbe Tundu Lissu kamwaga ugali wa Amekuja kushtuka, kashajifunga goli.
Mungu ampe maisha marefu ili siku moja aje akiri makosa.
Duh...!.
P
 
Mkuu Sikonge, amini nakuambia, kuelekea 2015, Lissu ataigharimu sana Chadema!. Tatizo la Mhe. Lissu ni dogo tuu, anatumia zaidi hoja za nguvu badala ya nguvu za hoja!.

Tofauti kubwa kati ya Lissu na Jamaa yangu, they are both brilliant upstairs, both are waropokaji, neither of them is a critical thinker, ila katika uropokaji huo, Lissu ni mbwatukaji kitendo cha jamaa yangu kuropoka kwa kurusha mishale ovyo was a mistake!. Tofauti kubwa kati yao, Lissu ni mtu wa papara bila strategies , jamaa yangu ni strategist !. Kikubwa zaidi , Jamaa yangu has "powers from within" ambazo Lissu hana!. Kukitokea mashindano kati ya mtu mwenye powers from within na mtu asiye nazo, mwenye nazo ndio atakaeshinda.

Ukimya wa Dr. Kitila sio kuwa amekubaliana na maamuzi, amegundua anadeal na mijitu mijinga ajabu!, ule waraka ni just "the winning coalition" mijitu mijinga inauita uhaini!, halafu watu humu wanasifu, kupongeza na kushangilia ujinga!. Mungu bariki ndani ya Chadema bado kuna wachache wenye akili kama Prof. Beregu, tunasikilizia kama watasikilizwa!.
Pasco
rejea tuu.
P
 
Nampa sana heshima Dr. Kitila Mkumbo kwa kusikiliza ushauri na hivyo, kuna siku itafika na Mkumbo anaweza kuja juu sana Kitila ni jembe lililowekwa pembeni na limetulia tuliii likisubiri tu muda wake uwadie lifanye mambo yake. Nategemea siku moja itakuwa hivyo.

Mungu ampe maisha marefu ili siku moja aje akiri.
Mkuu Sikonge, youare dam right kumhusu Kitila,baada ya uchaguzi, jamaa ni ndani ya cabinet!.
P
 
Leo uwezi kukusikia ukisemea katiba mpya tena; kweli wasioitakia mema Tanzania Mungu anawaona.
Watu mtahangaika sana kutembelea mitandao yote mnatafuta neno la mtu mnayedhani 'kanyamazishwa'. Internet trolling is a form of psychological torture. You'll never rest.

Clicking and looking around inasema mengi kuhusu state of mind. You'll never settle down and get focused kwenye issue ambazo wengine tunaziona ndizo za muhimu kuliko hii ambayo inawasumbua kila minute.

Bandiko lako linaonyesha kuwa huwezi kuacha trolling kwa sababu mmejawa na inferiority complex.

Get life. Tuna issue ya Rasimu ya Katiba ambayo ni muhimu kwa Wapenda maendeleo nchini.
abi
 
Back
Top Bottom