UZUSHI Ligi ya soka ya Afrika (African Football League) haina kanuni ya faida ya goli la ugenini

Baada ya tathmini, tumebaini kuwa taarifa hii ni ya uzushi
CAF wamethibitisha kuwa kwenye michuano ya AFRICAN FOOTBALL LEAGUE hakuna kanuni ya goli la ugenini (away goal rule) hivyo mechi ya Simba na Al Ahly ni mpya kabisa kule Cairo, yani lazima timu ishinde kuvuka nusu fainali. - Farhan kihamu jr
IMG_8846.jpeg
 
Tunachokijua
Ligi ya Soka ya Afrika (African Football League-AFL) ni shindano maarufu la kila mwaka la kandanda la vilabu linalotumika kama sherehe ya ubora wa kandanda na urafiki katika bara la Afrika.

Ilianzishwa kwa maono ya kuimarisha ubora wa soka barani Afrika na kukuza ukuaji wa kifedha kwa vilabu na wadau wanaoshiriki.

Mashindano ya kwanza ya AFL yameanza Oktoba 20, 2023 kwa kuzikutanisha Simba SC na Al Ahly ya Misri, mchezo uliotamatika kwa sare ya kufungana bao 2-2.

Timu zilizotajwa kushiriki kwenye awamu ya kwanza ya shindano hili ni Al Ahly SC (Misri), Enyimba FC (Nigeria), Espérance Sportive de Tunis (Tunisia), Mamelodi Sundowns FC (Afrika Kusini), Athletic Petroleos ya Luanda (Angola), Simba SC (Tanzania), TP Mazembe (DR Congo), na Wydad AC (Morocco).

b37b8f_06869788cd904e3da16d1d4899c691c0~mv2.jpeg

Ratiba ya Mashindano
Mkusanyiko huu mkubwa wa vilabu unaonyesha dhamira ya AFL ya kuunganisha tamaduni mbalimbali za kandanda kwenye jukwaa moja.

Dhamira kuu ya AFL inahusu maendeleo ya soka ya Afrika katika masuala ya ustadi na ustawi wa kifedha.

Kwa kutoa jukwaa la ushindani lisilo na kifani, ligi inalenga kuinua ubora wa mchezo huku ikizalisha vyanzo vingi vya mapato ambavyo vinasambazwa sawia kati ya vilabu shiriki na washikadau wote wanaohusika.

AFL inafanya kazi kama chombo huru, ikichukua jukumu la kuanzisha, kuendesha na kusimamia shindano. Uhuru huu unahakikisha kwamba ligi inaweza kutenda kwa manufaa ya mchezo na washiriki wake, huku ikizingatia viwango vya juu vya haki, uwazi na weledi.

Madai ya kutokuwepo kwa kanuni ya faida ya Goli la ugenini
Baada ya kumalizika kwa mechi ya ufunguzi kati ya Simba SC ya Tanzania na Al Alhly ya Misri ambapo timu zote zilitoshana nguvu kwa kufungana mabao 2-2, madai ya kutokuwepo kwa kanuni ya goli la ugenini yaliibuka.

Kupitia mtandao wa X (Zamani Twitter), Mdau mkubwa wa masuala ya michezo Ndugu Michael Mwebe aliweka chapisho linalodokeza uwepo wa sinfohamu katika kanuni zinazohusu goli la ugenini.

Mwebe alibainisha kuwa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) lilikuwa limechapisha kwenye tovuti yake kuwa kanuni ya faida ya goli la ugenini ilikuwa imefutwa, huku chapisho lingine la tovuti rasmi ya AFL ikibainisha kuwa kanuni ya faida ya goli la ugenini ilikuwa bado ipo.

Baadae, baadhi ya wachambuzi wa mpira wa miguu akiwemo Farhan Kihamu walithibitisha kuwa Shirikisho la Mpira Barani Afrika (CAF) rasmi lilikuwa limeondoa kanuni ya goli la ugenini.

“CAF wamethibitisha kuwa kwenye michuano ya AFRICAN FOOTBALL LEAGUE hakuna kanuni ya goli la ugenini (away goal rule) hivyo mechi ya Simba na Al Ahly ni mpya kabisa kule Cairo, yani lazima timu ishinde kuvuka nusu fainali” aliandika Farhan.

Pia, baadhi ya kurasa za michezo na vituo vya redio viliripoti habari hiyo.

Kanuni za Mashindao ya AFL zinasemaje?
Kanuni ya 15.1 hadi 15.3 inafafanua jinsi mshindi atakavyopatikana kuanzia hatua ya robo fainali hadi fainali.

15.1. Raundi zote za Mashindano zitachezwa chini ya mfumo wa mtoano, kwa msingi wa nyumbani na ugenini kwa mechi mbili.

15.2. Kwa hatua ya robo fainali na nusu fainali, timu ambayo itafunga magoli mengi ya jumla katika mechi hizo mbili inafuzu kwa hatua inayofuata ya Mashindano. Kwa fainali, timu itakayofunga jumla ya mabao katika mechi hizo mbili inatangazwa mshindi wa Ligi ya Soka ya Afrika ya 2023.

15.3. Katika tukio la idadi sawa ya mabao ya jumla yaliyofungwa mwishoni mwa kanuni muda wa mechi ya pili:
  • Kwa robo fainali na nusu fainali: Timu yenye idadi kubwa ya mabao ya ugenini inafuzu hatua inayofuata.
  • Timu yenye idadi kubwa ya mabao ya ugenini itatangazwa kuwa mshindi wa AFL 2023.
img_8850-jpeg.2790622

Kanuni za goli la ugenini kwenye AFL
Kwa kurejea kanuni hizi, JamiiForums imebaini kuwa madai yanayosambaa mtandaoni kuhusu kuondolewa kwa kanuni hii hayana ukweli.

Makala ya tovuti rasmi ya AFL iliyokuwa inatoa taarifa ya kilichojiri kwenye mchezo wa ufunguzi kati ya Simba na Al Ahly ilidokeza pia juu ya uwepo wa kanuni ya goli la ugenini.

“………….na sasa wanaelekea katika mchezo wa marudiano mjini Cairo wikendi ijayo wakihitaji ushindi wa moja kwa moja au sare ya juu ya zaidi ya mabao mawili ili kusonga mbele.” Ilibainisha sehemu ya taarifa hiyo.

Aidha, Oktoba 22, 2023, mchambuzi wa masuala ya mpira wa miguu kutoka Ghana, Micky Jnr alichapisha kwenye mtandao wa X kuwa alizungumza moja kwa moja na waandaaji wa michuano hii kwenye uwanja wa Mkapa na wakamhakikishia kuwa kanuni ilikuwa haijaondolewa, hivyo goli na ugenini litaendelea kuhesabika kama kawaida.

Baraza linalosimamia ligi hii linashikilia haki za kipekee kwa vipengele vyote vya kibiashara kwenye mashindano ya AFL. Hii ni pamoja na utangazaji, ufadhili, uuzaji, na njia nyinginezo za kuzalisha mapato.

Mbinu hii itawezesha ligi kutumia uwezo wake wa kuongeza mapato na kuwekeza tena katika ukuaji endelevu wa soka la Afrika.

Msimu wa kwanza wa ligi hii utahitimishwa Novemba 21, 2023.
Nimempa Robertinho mbinu za kupunguza MAGOLi.

Zile Tano Tano za Ausems ilikuwa ni uzembe WA KOCHA.
Hakuna cha kupunguza magoli mkuu, mnyama anashinda muhimu umakini tu na mbinu sahihi hakuna timu isiyo fungwa
 
CAF wamethibitisha kuwa kwenye michuano ya AFRICAN FOOTBALL LEAGUE hakuna kanuni ya goli la ugenini (away goal rule) hivyo mechi ya Simba na Al Ahly ni mpya kabisa kule Cairo, yani lazima timu ishinde kuvuka nusu fainali. - Farhan kihamu jr
Source ni Farhan sio CAF?
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom