Lazaro Nyalandu: Tatizo kubwa la CHADEMA ni Uongozi wa juu, CCM imejaliwa mfumo

Huyu kuna namna.. na Chadema wanamjua sana tu, asijione mwerevu. Ndio maana Mbowe alimkatalia msaada wake wa kumkodia Lissu ndege, wakati alipopigwa zile risasi.. Pengine wangemmaliza Lissu wa watu hawa. Wakina Mbowe wanamjua sana tu, asitake wamuongelee.
 
Nchi hii Dictator number 1 ni Freeman Aikaeli Mbowe huyu siku Mungu akimuita utazuka ugomvi mkubwa sana wa kugombea madaraka Chadema kati ya familia na ukoo wa Mbowe na wanaharakati uchwala kina Lissu na wenzake.
Mungu amjalie afya njema na maisha marefu Mh Mbowe. Hakika wewe ni Jabali.

Jiwe kahangaika na wewe katangulia yeye. Tujenge Chadema yetu Mkuu.
 
Mpuuzi tu huyo. Kwanza Kamati kuu hachagui wagombea, inapendekeza majina... Na wote tunajua CDM walikua na majina 3....Bora angesema kuwa alidhulumiwa kura kwenye baraza kuu.

Hivi hao waandishi wa Habari hawajui kuuliza maswali au ndiyo upeo wao ulipoishia...!?
Ukmuona kobe juu ya mti ujue kapandishwa.
 
Hapana wapo wengi wenye akili kumzidi tatizo wananjaa sana. Visenti kidogo tu wanauza chama imagine Halima Mdee au Bulaya mmoja wapo angepewa uenyekiti ingekuwaje ? Wangeuza sio chama tu wangetuuza mpaka wanachama wenyewe
Kwa hiyo Mbowe akifa inakuwaje?
 
Nae alikua anajifanya kukimbilia Kenya walimdaka mpakani hapo Wakenya walijua sio mpinzani ndio maana walimrudisha upande wa Tanzania wahangaike nae hata hatukujua tena iliishia wapi anakuja na story za kutengeneza kila kukicha hawa ndio wale maisha yao ni siasa tuu bila siasa hakuna maisha...
Kama Tyson
 
Kuna vitu unajiuliza sana kuhusu Watanzania

Nayalandu kama raia ana haki ya kushiriki siasa popote pale alipo bila kuulizwa lolote au chochote
Nyalandu alipohama CCM ilikuwa kwa matakwa yake binafsi

Kinachokera ni kwamba baada ya kurudi CCM sasa anakwenda kueleza katika vyombo vya habari mambo yasisyohusiana na haki yake kama Raia ya kushirikia siasa.

Nyalandu alikuwa na haki ya kueleza hayo akiwa katika chama halafu aondoke. Hili la kueleza baada ya kupokewa ambalo tunajua lina ahadi ni njia ya kujitangaza ili mkono uende kinywani.

Kukaa kimya kunamjengea mtu heshima, haya ya Nyalandu ni kujivua nguo hadharani
Ipo siku tutasikia pia akitueleza ya chumbani sidhani kama anaelewa haki, wajibu na stara.

This is too low Nyalandu, hata kaheshima ulikokuwa nako sidhani kama kapo tena.
Ukimuona alivyo nadhifu hutaamini ..

JokaKuu Pascal Mayalla
Naunga mkono hoja. Niliwahi kusema kitu kuhusu hili...
P
 
Back
Top Bottom