Kwanini wali unaotokana na mpunga unaolimwa katika maeneo ya nchi yetu hivi sasa siyo hauna ladha na siyo mtamu?

Wali ulikua zamani bhana, unapikwa mtaa wa 7 unanukia hadi mtaa wakumi
Siku hizi wanasayansi wanakwenda na Madai ya Soko kwamba Je, Walaji wanataka nini? Kama walaji wanataka Uwingi i.e. Mavuno kwa wingi basi watazalisha mbegu zenye (Tija / Productivity) ya mavuno mengi lakini kwa bahati mbaya hayo mavuno hayana harufu kama mtoa mada anavyodai.
Ila kama ikitokea walaji wanataka Harufu (Rihi /Flavor) basi wataalam watajikita kwenye kuzalisha mbegu zenye kutoa harufu nzuri lakini kwa bahati mbaya mbegu zitoazo harufu sana (nzuri) huwa hazitoagi mazao kwa wingi. Wataalam wanacheza na Genetic Traits. Je, mnaukumbuka ule mchele uliozalishwa Morogoro na ukapewa jina la utani la Mdundiko? Wataalam wanajitahidi sana ili wakupe au wanakupa kile unachotaka.
 
Nimekumbuka zamani tulikua tunauza mchele kwa maeneo, Mchele wa magugu, kahama na mbeya hii ilikua bei juu Michele wa Moshi bei rahisi ukipika magugu unanukia hadi kwa majirani Ile harufu siisikii sikuhizi
 
Siku hizi wanasayansi wanakwenda na Madai ya Soko kwamba Je, Walaji wanataka nini? Kama walaji wanataka Uwingi i.e. Mavuno kwa wingi basi watazalisha mbegu zenye (Tija / Productivity) ya mavuno mengi lakini kwa bahati mbaya hayo mavuno hayana harufu kama mtoa mada anavyodai.
Ila kama ikitokea walaji wanataka Harufu (Rihi /Flavor) basi wataalam watajikita kwenye kuzalisha mbegu zenye kutoa harufu nzuri lakini kwa bahati mbaya mbegu zitoazo harufu sana (nzuri) huwa hazitoagi mazao kwa wingi. Wataalam wanacheza na Genetic Traits. Je, mnaukumbuka ule mchele uliozalishwa Morogoro na ukapewa jina la utani la Mdundiko? Wataalam wanajitahidi sana ili wakupe au wanakupa kile unachotaka.
Jibu la kitaalamu kabisa hili.
 
Ninaomba Wizara ya Kilimo ufanye utafiti ni kwa nini wali unaotokana na mpunga unaozalishwa katika maeneo yanchi yetu ladha yake siyo tamu? Nimenunua mchele ambao ni mzuri kabisa lakini ulipopikwa kwa kweli hauna ladha na siyo mtamu.
Mbegu....mbolea....madawa.....
Zamani jirani akipiga wali harufu mpaka mtaa wa pili.
 
Siku hizi wanasayansi wanakwenda na Madai ya Soko kwamba Je, Walaji wanataka nini? Kama walaji wanataka Uwingi i.e. Mavuno kwa wingi basi watazalisha mbegu zenye (Tija / Productivity) ya mavuno mengi lakini kwa bahati mbaya hayo mavuno hayana harufu kama mtoa mada anavyodai.
Ila kama ikitokea walaji wanataka Harufu (Rihi /Flavor) basi wataalam watajikita kwenye kuzalisha mbegu zenye kutoa harufu nzuri lakini kwa bahati mbaya mbegu zitoazo harufu sana (nzuri) huwa hazitoagi mazao kwa wingi. Wataalam wanacheza na Genetic Traits. Je, mnaukumbuka ule mchele uliozalishwa Morogoro na ukapewa jina la utani la Mdundiko? Wataalam wanajitahidi sana ili wakupe au wanakupa kile unachotaka.
Nidokeze hapo kwa mchele wa mdundiko mkuu
 
OK; ilkuwa (kama sijakosea)kipindi 1985+ kulikuwa na njaa au uhaba wa chakula nchini na mchele uliadimika sana hata ikabidi nchi iagize mchele kutoka Taiwan. Watafiti wakakubali mbegu ya mchele pia iletwe kutoka huko Taiwan. Mbegu hiyo ilikuwa na sifa yakukomaa(Kuiva) mapeema, kuzaa sana na kuwa na punje kubwa zaidi ya hizi tulizozoea za kienyeji.
Mbegu ile ilipandwa na ilistawi na kuzaa sana kama ilivyo tarajiwa. Lakini mchele huo kasaro yake kubwa ilikuwa mchele huo ukipikwa unaumuka sana na hauna ladha yoyote wala kale kaharufu ka Mchele na wali wake uliopikwa unashikamana kama ugali hata ufanyeje....(Hiyo ikawa tayari ni kero na kasoro kwa walaji) Matokeo yake - Mchele huo ulikosa soko na hivyo kupelekea kutokulimwa tena.
 
Na ule mchele wa kitumbo ndio ulitoka Thailand. Au wa Thailand ulikuwa mwingine, kipindi mdogo tulitazama movies za Tony Jaa tukaijua Thailand hasa Bangkok (Mukandara Lufufu aliita Bankoko). Nikasikia na mchele unatoka Thailand nikaitambua nchi kirahisi.
 
Ninaomba Wizara ya Kilimo ufanye utafiti ni kwa nini wali unaotokana na mpunga unaozalishwa katika maeneo yanchi yetu ladha yake siyo tamu? Nimenunua mchele ambao ni mzuri kabisa lakini ulipopikwa kwa kweli hauna ladha na siyo mtamu.
Mchele wa Kyela original na unanukia upo Mbeya kilo ni shs 3,500! Mpunga huo unalimwa bila kuwekwa mbolea ya chumvichumvi. Unauzwa uarabuni maana ni ghali.
 
Back
Top Bottom