Kwanini vitendo vya ukatili vinavyofanywa na viongozi wateule wa Rais Tanzania vinaongezeka kwa kasi na hakuna anayechukuliwa hatua za kisheria?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
912
4,249
Kwa miaka kumi tumeona wakuu wa wilaya na mikoa wakichapa na kupiga subordinate wao na kuishia kutenguliwa uteuzi kisha baada ya muda kuteuliwa tena.

Tumeshuhudia viongozi kama Naibu Waziri akituhumiwa kunyanyasa mwajiriwa lakini hakuna chombo kinachochunguza na hata wanaotaka kuchukua hatua wanakatazwa na viongozi wale wale wanaodai wanapinga ukatili

Tumeona wakurugenzi na katibu tawala wakishukiwa sometimes kwa kubaka lakini hakuna Sehemu serikali inatoka adharani kuchukua hatua za kisheria.

Lakini juzi tumeona kichaa Kabaka kuku magazeti na vyombo vya dola vimeripoti wiki nzima na mjadala mkali ukiendelea. Tumeshuhudia waziri Gwajima akisikia maskini ametuhumiwa kwa tukio la unyanyasaji anakuja hapa Jf na kujibu hoja asubuhi mpaka jioni. Tumeshuhudia wanaharakati wanaposikia ubakaji kanda ya ziwa na mikoa ya kusini wanakimbia kwenda kuripoti; Je, sheria imetoa kinga kwa viongozi kutochukuliwa hatua kwa unyanyasaji?

Unyanyasaji linakuwa kosa pale linapofanywa na masikini tu?
 
Urais wa kifalme,
Tatizo liko kwenye katiba, ilibidi taasisi ziwe na uhuru na uwezo wa kumshughulikia yeyote bila kusubiria muongozo au maelekezo "kutoka juu"
 
Kwa miaka kumi tumeona wakuu wa wilaya na mikoa wakichapa na kupiga subordinate wao na kuishia kutenguliwa uteuzi kisha baada ya muda kuteuliwa tena.

Tumeshuhudia viongozi kama Naibu Waziri akituhumiwa kunyanyasa mwajiriwa lakini hakuna chombo kinachochunguza na hata wanaotaka kuchukua hatua wanakatazwa na viongozi wale wale wanaodai wanapinga ukatili

Tumeona wakurugenzi na katibu tawala wakishukiwa sometimes kwa kubaka lakini hakuna Sehemu serikali inatoka adharani kuchukua hatua za kisheria.

Lakini juzi tumeona kichaa Kabaka kuku magazeti na vyombo vya dola vimeripoti wiki nzima na mjadala mkali ukiendelea. Tumeshuhudia waziri Gwajima akisikia maskini ametuhumiwa kwa tukio la unyanyasaji anakuja hapa Jf na kujibu hoja asubuhi mpaka jioni. Tumeshuhudia wanaharakati wanaposikia ubakaji kanda ya ziwa na mikoa ya kusini wanakimbia kwenda kuripoti; Je, sheria imetoa kinga kwa viongozi kutochukuliwa hatua kwa unyanyasaji?

Unyanyasaji linakuwa kosa pale linapofanywa na masikini tu?
Baba ukiwa legelege home basi ni chanzo cha nidhamu mbovu
 
Mfano mzuri ni kile cha kule Babati cha mteule wa Raisi (Gekul) vyombo wa haki na sheria vilivyotumika kuwakandamiza wale vijana! Anyway, Mungu yupo
 
Mchakato mzima wa uteuzi umekaa kimagumashi. Yeye mwenyewe hata hawajui wengi wa hao anaowateua. Majina yanapenyezwa tu.

Kama unamjua mtu sahihi basi uteuzi unakula bila shaka.
 
Back
Top Bottom