Kwanini Polepole, Bashiru, Makonda, Kabudi nk walikuwa wanaamini katika maguvu na ubabe tu?

Chikenpox

JF-Expert Member
Oct 15, 2022
784
1,247
Katika uongozi uliopita kila kitu ilikuwa amri na bunge lilikosa kabisa uelekeo wake mana wanachojadili kinaweza kupinduliwa kibabe na asiwepo wa kuhoji.

Ikatengenezwa image kwamba wapinzania ni maadui wa nchi kumbe siyo kweli. Mpaka lisu akashambuliwa kwa masasi eti ni msaliti while in actual fact alikuwa mwiba kwa jiwe tu na udictator wake na makesi kibao yalirundikwa kwake lakini kila jaji anamwogopa Lissu.

Sasa nauliza kwa nini Hao wanaojiita wasomi wakienda contrary na wanachofundisha? Kwa sababu daradani Kuna Somo la human rights na rule of law ila wakavikana vyote hivyo
 
Katika uongozi uliopita kila kitu ilikuwa amri na bunge lilikosa kabisa uelekeo wake mana wanachojadili kinaweza kupinduliwa kibabe na asiwepo wa kuhoji...
Ilikua ni maelekezo ya principal za utawala kipind hicho! Nadhan unaelewa hata mkuu alikua on that way, ubabe na nguvu nying then akili kiduchu tuu!!
 
Ni wapi Polepole, Bashiru na Kabudi waliwahi kutumia nguvu?

Au unamaanisha kuongea kwa makasiriko? Ikiwa jibu ni ndio, vipi kuhusu Lema, Lisu na Sugu?

Binafsi nawashukuru sana hawa watu. Wametuonyesha sura halisi za wapinzani.

Wametuonyesha aina ya demokrasia tunapaswa kuwa nayo.

Katika kipindi chao CCM imekuwa imara, huduma za kijamii ziliboreshwa kwa kiwango kikubwa na hata uchumi ukaimarika mpaka tukaingia katika uchumi wa kati.

Mungu awabari sana hawa watu, walifanya kazi ya kutukuka chini ya kamanda wao John Pombe Joseph Magufulu.
 
Ni wapi Polepole, Bashiru na Kabudi waliwahi kutumia nguvu?

Au unamaanisha kuongea kwa makasiriko? Ikiwa jibu ni ndio, vipi kuhusu Lema, Lisu na Sugu...
Unakumbuka neno "vyuma kukaza" lilianzia awamu ya tano. Sasa hivi halisikiki tena. What sdoes it imply?
 
Katika uongozi uliopita kila kitu ilikuwa amri na bunge lilikosa kabisa uelekeo wake mana wanachojadili kinaweza kupinduliwa kibabe na asiwepo wa kuhoji...
Hawa watu unajua wana ukwasi kiasi gani sasa? Kama unafikiri enzi ya jiwe kulikuwa hakuna ufisadi, pole sana. How wealthy is Makonda? Polepole? Huu utajiri wamepata wapi?

Kulikuwa na kikundi fulani kilichoongozwa na shetani, kilizuia wizi mdogomdogo kwenye halmashauri na miradi kadhaa ya serikali, ila wao wakawa wanajichotea watakavyo kupitia mamiradi makubwa ya serikali. Taratibu za manunuzi ya umma zikawekwa kando.

Ili kufanikisha hayo, vyombo vya habari vikawekwa mfukoni, sheria kandamizi eg sheria ya takwimu etc zikawekwa, uchaguzi ukanajisiwa kuwa uchafuzi, tukapat bunge la ovyo la kusifia serikali, na mambo kama hayo. Unakumbuka ile kauli 'watimue huko bungeni Mimi niwashughulikie huku nje?

Hawa uliouliza, na wengine wao, walikuwa wanufaika wa mfumo ule uliojaa uovu kwa kisingizio cha uzalendo. Leo mara usikie kuna pesa imefichwa China mara Seychelles nk.

Na ni kwa vile ccm ni wale wale, there is a lot to be uncovered-shangaa ule ukaguzi ulioagizwa ufanywe bot kwenye transactions za January to march 21 ripoti yake hutaisikia milele.
 
Katika uongozi uliopita kila kitu ilikuwa amri na bunge lilikosa kabisa uelekeo wake mana wanachojadili kinaweza kupinduliwa kibabe na asiwepo wa kuhoji...
Kuanzia namba 1 Hadi Mwenyekiti wa Kijiji wote walikuwa washamba na limbukeni wa madaraka na kukosa exposure.
 
Unakumbuka neno "vyuma kukaza" lilianzia awamu ya tano. Sasa hivi halisikiki tena. What sdoes it imply?
Hii nchi ina wehu wengi ikiwemo wewe. Unataka kusema watanzania wote ni kina Mo Dewji siku hizi? Kwamba wote wanahela? Yaani mchele leo kilo moja 3500 halafu unaleta uchawa???????

Maisha ya watanzania yamezidi kuwa magumu kwa matozo yasiyoisha halafu unasema watu wamekaa kimya kumanisha wanahela????

Hujui waliokuwa wanalalamika na kusema ulichokiandika hapo kuwa ndiyo wanaonufaika na hizo tozo na wanalamba asali ndiyo maana wako kimya?

Jitambue. Nyie ndiyo mnasababisha tudai katiba Mpya!
 
Unangoja nini kuandamana
 
Kwa kawaida sisi wabongo tumeshazoea kusukumwa kuliko kutembea wenyewe ndio maana hata kauli ikitoka ni lazima itoke na kitisho.
1. Usikojoe hapa, faini 50000
2. Usipite hapa, kuna mbwa mkali
N.K
 
Ni wapi Polepole, Bashiru na Kabudi waliwahi kutumia nguvu?

Au unamaanisha kuongea kwa makasiriko? Ikiwa jibu ni ndio, vipi kuhusu Lema, Lisu na Sugu...
Eti mkaingia uchumi wa kati, ilikuwa ni uchumi wa chini wa kati na ndio kipindi vyuma vilikaza na ukosefu mkubwa wa ajira.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom