Kwanini wadau wanajamii forum mnabeza mtandao wa TikTok.

Msuli wa mbu

Senior Member
May 4, 2021
100
318
Binafsi sijapendezwa na baadhi ya wanajamii forum kubeza mtandao wa TikTok. Mwanzo nilikuwa sio mfuatiliaji wa mtandao huo(TikTok) kwakuwa niliona watu wengi hapa wakisema kuwa hauna maudhi mazuri na kuudharau kutokana na wao wanavyo uchukulia.

Cha ajabu na kushangaza nina mwezi sasa naufuatilia nimekutana na mambo mazuri na yana manufaa sana katika jamii na taifa hili Kama mtu atautumia in positive way nasisitiza "in positive way".

Lakini nikija hapa nakutana na watu sijui wana elimu ya juu sana au tuu ni watu class fulani sijaelewa wanaubeza, ndio nakubali kuwa Kuna baadhi ya maudhui zisizofaa lakini kwanini tusichukue zinazotufaa.

Hapa Duniani Kuna vitu vingi lakini huwezi kutaja kitu chenye chanya bila kuwa na hasi ila Kama binadamu tujitahidi kuwa positive....., Na maisha haya yatakuwa mazuri sana na sio kubeza kila kitu ama wazo.


Asanteni muwe na weekend njema.
 
Binafsi Nilicho gundua kuhusu Tik tok ni kwamba Kusogeza kwa mfululizo kunakuza muda mfupi wa umakini.

Usogezaji au ku scroll mfululizo kupitia video fupi hudumisha umakini wa muda mfupi, hivyo kufanya iwe vigumu kuangazia kazi zinazohitaji umakini wa muda mrefu.
 
Tik tok inapigwa vita na Kila nchi iliyoendelea Ile ni cocaine/heroine ya kidigitali
Ukisikia kijana ana depression ujue video yake inakosa like tiktok
Amna hoja ngepesi sana hii, kivip mkuu? kuwa iwe cocaine mkuu wakati Kuna content za kijamii Kama upishi, uashi, na mambo mbalimbali yanayo saidia jamii.

Sababu za TikTok kuzuiliwa ni kuingilia mifumo ya kinchi sio digital cocaine Kama unavosema mkuu.
 
Vichekesho vyote vya tiktok vina maudhui mazuri sana.
Ukiwa interested na vichekesho watakuletea vichekesho, ila ukiwa interested na mambo positive wanakuletea pia.

Nina mashaka nahisi watu wengi humu hawajanielewa
Binafsi Nilicho gundua kuhusu Tik tok ni kwamba Kusogeza kwa mfululizo kunakuza muda mfupi wa umakini.

Usogezaji au ku scroll mfululizo kupitia video fupi hudumisha umakini wa muda mfupi, hivyo kufanya iwe vigumu kuangazia kazi zinazohitaji umakini wa muda mrefu.
Kwa nini uingie TikTok kwajili ya ku- scroll na si kujifunza mkuu.

Pia kujifunza kwa video fupi kunasevu data kwa watanzania wa Hali ya chini wakajifunza kitu.
 
Back
Top Bottom