Kwa mtaji wa milioni 12, nifungue hardware, nafaka au phone and accessories?

Prakatatumba abaabaabaa

JF-Expert Member
Aug 2, 2022
1,512
4,848
Wakuu, nipo hapa napambania kujikwamua kwenye umaskini, nipo nachakata mawazo kwa ajili ya kufanya harakati, wengi walianzia chini sana na wakafanikiwa kupata pesa nyingi.

Mawazo yangu niliyonayo ni Nafaka, vifaa vya simu pamoja na umeme, mwisho ni hardware.

Nafaka nilitaka nideal na maharage, mchele pamoja na nafaka nyingine means nazitoa porini nakuja kuziuza mjini, changamoto Mimi ni Mwalimu kwahiyo muda wa kuzunguka porini nakua nimekosa, makazi Kwa Sasa nipo kigoma.

Vifaa vya simu, kigoma huku naona vitu ni bei kubwa sana mfano USB ni 7000, earphone 5000 na vitu vingine, nikatamani niingie kwenye hii biashara kwa sababu machimbo kariakoo ya bei rahisi nayafahamu.

Vifaa vya ujenzi, hii ni hobby yangu, naipenda sana na watu wamepata pesa kweli, kigoma mfuko wa cement ni 26,000/= pamoja na vifaa vingine changamoto mji ni mdogo na competition ni kubwa, hapa kwenye hardware nilitaka nijichanganye kwwnye kununua machine ya uchomeleaji pamoja na aluminum.

Wakuu, lengo langu nipate faida ya laki 5 tu kwa mwezi.

Asanteni
 
Nipe mbinu mkuu, najua wewe ni guru kwenye idara hii, nisaidie kuwaza nje ya box
Nani kakuambia mimi ni nguli kwenye hiyo idara, just try to be critical katika kufikiri biashara kulingana na eneo uliopo na uwezo wako, epuka biashara inao weza kufanywa na kila mtu, haihudumu ina leta ushindani mkali na kugombania wateja mwishowe mtaji unakata.
 
Wakuu, nipo hapa napambania kujikwamua kwenye umaskini, nipo nachakata mawazo kwa ajili ya kufanya harakati, wengi walianzia chini sana na wakafanikiwa kupata pesa nyingi.

Mawazo yangu niliyonayo ni Nafaka, vifaa vya simu pamoja na umeme, mwisho ni hardware,

Nafaka nilitaka nideal na maharage, mchele pamoja na nafaka nyingine means nazitoa porini nakuja kuziuza mjini, changamoto Mimi ni Mwalimu kwahiyo muda wa kuzunguka porini nakua nimekosa, makazi Kwa Sasa nipo kigoma.

Vifaa vya simu, kigoma huku naona vitu ni bei kubwa sana mfano USB ni 7000, earphone 5000 na vitu vingine, nikatamani niingie kwenye hii biashara kwa sababu machimbo kariakoo ya bei rahisi nayafahamu.

Vifaa vya ujenzi, hii ni hobby yangu, naipenda sana na watu wamepata pesa kweli, kigoma mfuko wa cement ni 26,000/= pamoja na vifaa vingine changamoto mji ni mdogo na competition ni kubwa, hapa kwenye hardware nilitaka nijichanganye kwwnye kununua machine ya uchomeleaji pamoja na aluminum.

Wakuu, lengo langu nipate faida ya laki 5 tu kwa mwezi.

Asanteni

Una kitu…
 
Kosa lako ni kutaka mafanikio kupitia biashara lakini kazi hutaki kuacha, nakuhakikishia Mimi kuwa utumishi wa umma na kipato kikubwa ni mbingu na ardhi na mchawi muda na usimamizi kwa sababu unataka ukabidhi watu walifanyie kazi itakula kwako na huwezi kuwa mtumishi wakati huohuo kuwa mfanyabiashara angalau ungekuwa DC, DED, RC etc lakini kazi ya ualimu halafu unataka kutusua you should not be serious na kitakacho kuumiza ni uoga vinginevyo hiyo hela itapotea na hutaelewa imepoteaje kama unataka kufanya biashara chukua maamuzi ya kufa umesimama otherwise endelea kuishi umepiga magoti.
 
Back
Top Bottom