Katiba ya ACT-Wazalendo sura ya 4 ibara 29 inamtaka kiongozi atakayeshindwa uchaguzi wa kiserikali lazima ajieleze, akishindwa anaondolewa kwenye nafasi yake.
xiv) Endapo Kiongozi wa Chama atashindwa katika uchaguzi wowote wa kiserikali, Halmashauri Kuu ya Taifa itabidi ikutane katika kipindi kisichozidi miezi sita tangu kufanyika kwa uchaguzi huo ili kujadili mazingira ya kushindwa kwake na kupiga kura ya siri ya kuamua kama Kiongozi wa Chama anastahili kuendelea na nafasi yake au la. Kiongozi wa Chama ataendelea na nafasi yake endapo zaidi ya nusu ya wajumbe watapiga kura ya kuwa na imani naye.