Kwa hili lililotokea leo kwenye mechi kati ya Simba na Tabora basi Tanzania na Africa hatuwezi kusonga mbele kwenye mpira

Clark boots

JF-Expert Member
Jun 5, 2017
6,424
5,567
Waamuzi kama Amina na Tatu Malogo ambao wanaonesha dhahiri ushabiki wao na kununuliwa kwao na Simba basi Tz na Africa hatuwezi kufika kokote kwenye Dunia ya michezo.

Jambo hili lilionekana pia kule South Africa baada ya Vyura kukataliwa bao lao la wazi kabisa.

Mechi ya Leo ni wazi kuwa Tabora United wamenyimwa bao na Simba wamepata goli batiri la Counter attack iliyoanza kwa makosa. Ilitakiwa mpira uanza kati kwa kuwa Tabora walishafunga goli halali..
 
Uko sahihi, hii Simba feki inashusha kiwango cha Mpira wetu, mi niliangalia marudio ya mechi kati ya Simba na Coastal union nikasikitika sana, Fred alimsukuma hadi kuanguka vibaya mchezaji wa Mangushi aliekuwa akimkaba kisha akiwa huru mpira ukaja akafunga kwa mshangao mkubwa eti refa akawapa Simba goli nikasema what is this nonsense?

Mara kiungo fundi Ibrahim Ajibu akawachomoka mabeki wa Simba akaingia kwenye penati box ya Simba mabeki wawili wa Simba wakamchangia kwa pamoja na kumuangusha ndani ya box bila kuugusa mpira na refa akapeta badala ya kuipa Coastal union penati, ilinichukiza sana, sikupenda jinsi yule refa mweusi aliwanyonga Coastal union kisa wanacheza na Simba!! Hii mechi haikuwa halali Simba kupata yale matokeo

Mechi ingine ni lile goli halali la Singida big star refa na kibendera wake kulikataa bila aibu! Singida big stars walikuwa bora sana ila refa alihakikisha hawashindi mechi, Ile mechi ilitakiwa iishe Simba ikipokea kichapo but ikawa tofauti. Ukweli niliwachukia sana marefa wa ile mechi kuwanyima ushindi wale waliostahili

Yani Simba ikicheza ni maamuzi mabovu tu yanaonekana sijui kuna nini kwenye hii timu na marefa wa kibongo kuipendelea bila aibu maana mpira tunauona live. Huwa najiuliza hivi hawa TFF hawaangalii hizi mechi?
 
Hamkuona makosa ya marefa kwny mechi zenu mnakuja kushupalia mechi zetu...kaeni kwa kutulia nyie utopolo...kwanza goli la kagera sugar mrudishe...pili kumchezesha mchezaji ambaye hastahili mvuliwe point...yani mna ma ujinga ujinga mengi sema Simba huwa hatuna midomo kama nyie...
 
Uwe na usiku mwema dada yangu kipenzi, haha
 
Hamkuona makosa ya marefa kwny mechi zenu mnakuja kushupalia mechi zetu...kaeni kwa kutulia nyie utopolo...kwanza goli la kagera sugar mrudishe...pili kumchezesha mchezaji ambaye hastahili mvuliwe point...yani mna ma ujinga ujinga mengi sema Simba huwa hatuna midomo kama nyie...
Ubuntu botho
 
Haya mambo hata ulaya yapo ndio maana wakaanzia VAR na Goal line technology. Ok sawa mnataka haya mambo yaishe mnaweza kugharamia VAR na Goal line technology?.
Man u na Barcelona ndiyo wamefanya goal line na VAR zije,walikua wakibebwa
 
Waamuzi kama Amina na Tatu Malogo ambao wanaonesha dhahiri ushabiki wao na kununuliwa kwao na Simba basi Tz na Africa hatuwezi kufika kokote kwenye Dunia ya michezo.

Jambo hili lilionekana pia kule South Africa baada ya Vyura kukataliwa bao lao la wazi kabisa.

Mechi ya Leo ni wazi kuwa Tabora United wamenyimwa bao na Simba wamepata goli batiri la Counter attack iliyoanza kwa makosa. Ilitakiwa mpira uanza kati kwa kuwa Tabora walishafunga goli halali..
Tatizo la kuweka wanawake kua WAAMUZI ndio chanzo
 
Uko sahihi, hii Simba feki inashusha kiwango cha Mpira wetu, mi niliangalia marudio ya mechi kati ya Simba na Coastal union nikasikitika sana, Fred alimsukuma hadi kuanguka vibaya mchezaji wa Mangushi aliekuwa akimkaba kisha akiwa huru mpira ukaja akafunga kwa mshangao mkubwa eti refa akawapa Simba goli nikasema what is this nonsense?

Mara kiungo fundi Ibrahim Ajibu akawachomoka mabeki wa Simba akaingia kwenye penati box ya Simba mabeki wawili wa Simba wakamchangia kwa pamoja na kumuangusha ndani ya box bila kuugusa mpira na refa akapeta badala ya kuipa Coastal union penati, ilinichukiza sana, sikupenda jinsi yule refa mweusi aliwanyonga Coastal union kisa wanacheza na Simba!! Hii mechi haikuwa halali Simba kupata yale matokeo

Mechi ingine ni lile goli halali la Singida big star refa na kibendera wake kulikataa bila aibu! Singida big stars walikuwa bora sana ila refa alihakikisha hawashindi mechi, Ile mechi ilitakiwa iishe Simba ikipokea kichapo but ikawa tofauti. Ukweli niliwachukia sana marefa wa ile mechi kuwanyima ushindi wale waliostahili

Yani Simba ikicheza ni maamuzi mabovu tu yanaonekana sijui kuna nini kwenye hii timu na marefa wa kibongo kuipendelea bila aibu maana mpira tunauona live. Huwa najiuliza hivi hawa TFF hawaangalii hizi mechi?
Hizi ndizo dalili za uchawi wa utopolo
 
Simba huwa hainunui mechi ndio maana haina ushindi wa mwendelezo kama timu fulani ambayo wanaanzia kuhonga wachambuzi hata wakibebwa huwezi kusikia kelele.

Simba anakabiliana kwa haki kabisa na mechi za ukweli.

Achana na hawa jamaa mara beki kapewa pesa acheze chini ya kiwango,mara kiungo anahongwa ajifanye kaumia bado waamuzi na wachambuzi.Timu inaonekana inaupiga mwingi kumbe uhuni tu umetangulia.
 
Utadhani huko ulaya mnakodhaji wako vizuri hawafanyi makosa, wakati pamoja na hizo VAR zao bado makosa yapo tu.

Hapa kwetu marefa pamoja na vifaa duni ila wanajitahidi kwa kiasi chake.

Lile goli alipaswa kuamua kibendera, ila nae alichelewa kufika kabla ya mpira kumpita goalkeeper.
Hakuna goal line technology, hakuna VAR, ni refa wa kati na kibendera tu ndo waamue.
 
  • Thanks
Reactions: BRN
Waamuzi kama Amina na Tatu Malogo ambao wanaonesha dhahiri ushabiki wao na kununuliwa kwao na Simba basi Tz na Africa hatuwezi kufika kokote kwenye Dunia ya michezo.

Jambo hili lilionekana pia kule South Africa baada ya Vyura kukataliwa bao lao la wazi kabisa.

Mechi ya Leo ni wazi kuwa Tabora United wamenyimwa bao na Simba wamepata goli batiri la Counter attack iliyoanza kwa makosa. Ilitakiwa mpira uanza kati kwa kuwa Tabora walishafunga goli halali..
Tutalifanyia kazi tu aa taarifa ndan aya massa 44
 
Simba huwa hainunui mechi ndio maana haina ushindi wa mwendelezo kama timu fulani ambayo wanaanzia kuhonga wachambuzi hata wakibebwa huwezi kusikia kelele.

Simba anakabiliana kwa haki kabisa na mechi za ukweli.

Achana na hawa jamaa mara beki kapewa pesa acheze chini ya kiwango,mara kiungo anahongwa ajifanye kaumia bado waamuzi na wachambuzi.Timu inaonekana inaupiga mwingi kumbe uhuni tu umetangulia.
Mara kipa akimbie mechi
 
Back
Top Bottom