Kuna viongozi wana picha nyingi mitandaoni zisizoendana na utatuzi wa kero za maendeleo; kila jambo wamejiposti

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
912
4,247
Ukiona kiongozi anapenda kila anapokwenda vyombo vya habari vimpige picha na kuposti tambua huyo hana maono.

Utendaji kazi haupomwi kwa wingi wa picha na ziara ulizofanya; utendaji kazi upimwa kwa idadi ya kero ulizotatua . Na siyo kero ulizotatua pekee bali namna ulivyotafuta ufumbuzi wa kudumu wa changamoto

Kuna tabia imezuka ya viongozi wanasiasa wa vyama vyote na watumishi wa umma kupiga picha na matatizo au kero za wananchi bila kuzitatua. Kwao wanatumia kero na changamoto kujitangaza kwamba wanafanya kazi lakini kutathimini hakuna kero hata moja alizotumia kupiga picha anayotatua.

Viongoz wa aina hizi wanapenda sana kuwaona wananchi kama hawana akili na utumia sana kauli za WANYONGE.

Ukisikia kiongozi anahubiri kwamba wananchi ni wanyonge maana yake amewafanya wasiwe watu wakisema wala kufikiri. Kama jamii tuepukane na wapiga picha wanaotumia matatizo ya jamii kujinufaisha kiuchumi na kisiasa
 
Back
Top Bottom