Kuna utapeli wa mtandaoni unautumia jina la UNICEF

Edger Ezekiel

Member
Feb 20, 2024
9
9
Jamii naomba tusaidiane kuelimisha juu ya utapeli unaofanyika hasa kwa mtandao wa facebook kwa kutumia jina la UNICEF.

Utapeli huu sasa umekithiri na watu wengi sana wanaendelea kuumia juu ya utapeli unaofanyika na kikundi kinachotumia jina la UNICEF na kudai kuwa wanatoa msaada wa fedha mara tu baada ya kuchati nao kwa njia ya WhatsApp.

Serikali pamoja na wamiliki wa mtandao wa facebook waingilie kati swala hili pia mfumo wa kuingia kwenye account ya mtu bila ruhusa ya mmiliki wa account hiyo ubadilishwe maana account nyingi hazina ulinzi kitu kinachofanya watu waibiwe account zao na zinatumika kufanya utapeli.
 
Serikali yenyewe inatukanwa mtandaoni imeshindwa kujilinda watawezaje kuwadhibiti hao UNICEF fake
 
Kwanini utapeliwe?

Unayetapeliwa na wewe ni mshamba

Haiingii akilini mtu anakwambia kuna pesa zimetumwa kwa ajili yako ili kuzipata sasa unatakiwa utume kiasi cha fedha ili kuweza kukomboa hizo pesa..

Na watu hapa wapo wanaotuma ..

Acha mpigwe tu na ushamba wenu, hakuna pesa ya kukomboa.

Yaani utume elfu 12 ukomboe Dola 5000..
 
Mimi katika maisha yangu huwa siamimi kama naweza kupata fedha bure bila kuzitokea jasho!
Nikishasikia Toa fedha utapata mara mbili,fanya hili utapata fedha bure,nk huwa sipotezi muda kusikiliza huo ujinga!
 
Back
Top Bottom