Kuna siri nyingi zimefichika kwa mamillioni ya watu duniani kote, Afrika ndio balaa. Je, nifanyeje ili watu wapate kunielewa?

Mwamba3

Member
Nov 14, 2022
43
73
Habari Wana JF !
Ni hakika Kwamba ni mambo (Siri) mengi yamefichwa Kwa mamillion ya watu Duniani kote , lakini ukijaribu kuwaambia watu Ukweli HAWAKUELEWI .

Ni hivi Ulimwengu huu wa sasa ulijengwa Kwa mifumo dhabiti na ma - elites wa Dunia hii tangu zama za zamani sana. Hivyo namna ambavyo Binadamu anaishi Leo hii ndivyo ilivyopangwa na Wakuu wa Dunia hii .
Yaani, Mifumo ya uchumi , Siasa na Dini (Imani ) yote ni mifumo fake. Mifumo hii Ipo kuhakikisha Binadamu anatawalika na watu wachache sana ambao ndiyo wabeba Siri za Dunia hii. Yaani Mfumo wa maisha tuliyonao ulisharatibiwa Karne nyingi zilizopita
Mfano ;
-Katika historia ; HISTORIA tuliyonayo ni batili, imechanganywa na uongo mwingi ili tusijue Ukweli.
  • Elimu tunayopatiwa siyo halisi, Ipo tu ili kumzubaisha Binadamu alizike na mambo madogo ambayo hayana global future yoyotE. Mfumo wa Elimu unaamliwa uweje na watu wachache sana. Yaani ; Kuna Maarifa nje ya Elimu tunayopata ambayo yamezuiliwa kujifunza. Uhasibu , udaktari, uuguzi, ualimu , uanasheria, N. K ni miongoni mwa taaluma za viwango vya chini sana Duniani .
  • Mwanadamu kuamini kuwa Safari yake ni kwenda Mbinguni na wakati hayuko tayari kufa ili aende Mbinguni, huu ni uongo wa Hali ya juu sana . Mfumo wa Dini upo Kwa ajili ya kumfanya Binadamu awe Mtii mno Kwa wenye mifumo.
  • Haitakuja Kutokea hata siku moja kuwa mifumo ya Siasa tuliyonayo ndiyo mwarobaini wa matatizo ya Binadamu ni impossible. Siasa zipo Kwa ajili ya kuwagawanya watu ili kuwatawala. Hivi umewahi kufikiria ni nini kingetokea Duniani andapo Mwanadamu ameamua kuigomea mifumo ya Dini na Siasa ?

Yaani Katika Dunia hii Kila kitu kimegeuzwa uhalisia wake. Mwafrika utambulisho aliyonao siyo wa kweli, Mazingira nayo yamebadilishwa, Kilimo hakipo kwenye uhalisia, Biashara ni Giza Nene.

Swali langu ni Kwamba; AFRIKA tunajitihada gani ya kuitafuta kweli iliyofichwa Kwa miaka mingi inayotufanya tuwe Watumwa wa mataifa mengine. Ni Lini tunaachana na Imani za kutupeleka Mbinguni wakati siyo Mpango wa Mungu ?

Dah !.....
 
Unapokua unapinga jambo fulani lazima kuwe na mbadala. Je mbadala ni nini?

Mfano dini imewekwa kwa ajili ya kunyoosha watu wakae kwenye mstari na waishi kwa maadili. Binadamu kiasili ni mdadisi sana hvyo kufanya awe anafanya vitu vingi kupitiliza. Je ukiacha dini tuna mbadala gani (dini ni pamoja na za asili na ancestors wetu).

Elimu imewekwa ili watu waelewane pia kuwapa maarifa watu kuhusu gunduzi mbalimbali na namna ya kuzitumikia. Je mbadala ni nini?
 
Ukitaka vita chokonoa vile vitabu viwili maarufu, ayayayaaa ndio utajua vile ambavyo akili za wengi zimeshikwa. Lakini embu tupe kidogo kidogo mfano mmoja kwa lile unalolijua ambalo unaona kabisa hili tumefichwa na kweli yake ni hii.
 
Kusema tumefichwa bila kuonesha njia ya kufumbuwa tuliyofichwa ni uzandiki mtupu. Mwache binadamu afurahie kile anachokiona ni chema mbele yake as long as amani imemtawala
 
mada nzuri sana hii..ila ukweli nikwamba haya yote yapo kinyume chake nadunia inasiri nzito nazaidi hakuna utakae mueleza siri hizo japo kwauchache akakuelewa ningumu sana nazaidi utaonekani nichizi usie na elimu yakutosha au shule ujapita.
😢😢😢😢 dunia inamambo mengi sana.
 
Habari Wana JF !
Ni hakika Kwamba ni mambo (Siri) mengi yamefichwa Kwa mamillion ya watu Duniani kote , lakini ukijaribu kuwaambia watu Ukweli HAWAKUELEWI .

Ni hivi Ulimwengu huu wa sasa ulijengwa Kwa mifumo dhabiti na ma - elites wa Dunia hii tangu zama za zamani sana. Hivyo namna ambavyo Binadamu anaishi Leo hii ndivyo ilivyopangwa na Wakuu wa Dunia hii .
Yaani, Mifumo ya uchumi , Siasa na Dini (Imani ) yote ni mifumo fake. Mifumo hii Ipo kuhakikisha Binadamu anatawalika na watu wachache sana ambao ndiyo wabeba Siri za Dunia hii. Yaani Mfumo wa maisha tuliyonao ulisharatibiwa Karne nyingi zilizopita
Mfano ;
-Katika historia ; HISTORIA tuliyonayo ni batili, imechanganywa na uongo mwingi ili tusijue Ukweli.
  • Elimu tunayopatiwa siyo halisi, Ipo tu ili kumzubaisha Binadamu alizike na mambo madogo ambayo hayana global future yoyotE. Mfumo wa Elimu unaamliwa uweje na watu wachache sana. Yaani ; Kuna Maarifa nje ya Elimu tunayopata ambayo yamezuiliwa kujifunza. Uhasibu , udaktari, uuguzi, ualimu , uanasheria, N. K ni miongoni mwa taaluma za viwango vya chini sana Duniani .
  • Mwanadamu kuamini kuwa Safari yake ni kwenda Mbinguni na wakati hayuko tayari kufa ili aende Mbinguni, huu ni uongo wa Hali ya juu sana . Mfumo wa Dini upo Kwa ajili ya kumfanya Binadamu awe Mtii mno Kwa wenye mifumo.
  • Haitakuja Kutokea hata siku moja kuwa mifumo ya Siasa tuliyonayo ndiyo mwarobaini wa matatizo ya Binadamu ni impossible. Siasa zipo Kwa ajili ya kuwagawanya watu ili kuwatawala. Hivi umewahi kufikiria ni nini kingetokea Duniani andapo Mwanadamu ameamua kuigomea mifumo ya Dini na Siasa ?

Yaani Katika Dunia hii Kila kitu kimegeuzwa uhalisia wake. Mwafrika utambulisho aliyonao siyo wa kweli , Mazingira nayo yamebadilishwa , Kilimo hakipo kwenye uhalisia , Biashara ni Giza Nene.

Swali langu ni Kwamba; AFRIKA tunajitihada gani ya kuitafuta kweli iliyofichwa Kwa miaka mingi inayotufanya tuwe Watumwa wa mataifa mengine. Ni Lini tunaachana na Imani za kutupeleka Mbinguni wakati siyo Mpango wa Mungu ?

Dah !.....
Mkuu! Umeoa? Unamwambiaga mke wako ukweli wako wote? Ni hatari gani utaipata ukimwambia ukweli. Wanasaikolojia walisema "the less you know the better! It is for your own good". Wewe kama ni Mkristo, Mungu tunayemwabudu ana siri nyingi ambazo hata Yesu Kristo na Roho mtakatifu hawazijui! Kwa mfano! Siku ya kuja mara ya pili Yesu Kristo duniani hakuna haijuaye (hata mwana) ila Mungu tu peke yake!
Mathayo 24:36
[36]Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake.

Kwahiyo hata wakuu wa dunia na maarifa ya kutawala dunia hawawezi kukuambia! Japo kuna basic za kwamba ili ufanikiwe lazima ufanye kazi kwa bidii ukitumia AKILI+BUSARA+NGUVU ZA KIROHO
 
Back
Top Bottom