Kumkwamisha Rais Samia Suluhu ni kuikwamisha Tanzania

Mwananchi Huru

JF-Expert Member
Nov 20, 2021
1,555
1,157
IMG-20220125-WA0002.jpg

====
Ukweli ni kwamba, lipo kundi ndani ya Taifa hili tukufu la Tanzania linaloinyooshea vidole Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwamba imekumbwa na Rushwa na Ufisadi wa kutisha ghafla.

Kundi hili hatari kwa Taifa letu linamwona Rais Samia Suluhu Hassan kama ni mtu aliyeshindwa kupambana na Rushwa na Ufisadi ila tu Hayati Dkt John Pombe Joseph Magufuli ambaye hata hivyo kutetea mfu ni kumkufuru Mungu aliyemwita na kumchukua,

Wakati flani,Rais Samia Suluhu Hassan akiwa bandari ya Dar es Salaam alilishambulia vikali kundi hili hatari linalodai kulinda na kutetea Legacy ya Hayati Dkt John John Pombe Joseph Magufuli kwa kuinyooshea vidole Serikali yake kwa Rushwa na Ufisadi yenye muda mfupi sana madarakani.

HOJA YANGU KWENU NI HII

Sote tunafahamu,Kati ya nafasi zaidi ya 1,000 za Uteuzi alizopewa Rais Samia Suluhu na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Rais Samia Suluhu Hassan hadi leo Viongozi wapya aliowateua hawajafika watu 100 sijui kwanini hataki kuteua watu wapya hilo tumwachie yeye.

Kwa lugha rahisi hawa Viongozi zaidi ya 900 ni Viongozi walewale wa awamu zilizopita hasa hasa awamu ya Nne na tano.

SWALI LANGU KWA MSOMAJI,

1. Hawa watu wanaonyooshewa Vidole wameleta tabia mpya ya Rushwa na Ufisadi awamu ya Sita wametoka Wapi kwa kipindi hiki kifupi au ni hawa wapya 100 walioteuliwa na Rais Samia ?

2. Je, nihawahawa waliotoka awamu zilizopita leo hii wote wamegeuka ghafla mashetani weusi au ndicho walichokifanya huko nyuma ila Utawala uliwaatamia tu na leo wamekwama kuiba wanaanza kubeza awamu ya 6?

3. Au wanaposema wanalinda legacy maana yake ni kutekeleza vitendo vya Rushwa na Ufisadi kisha kuisingizia Awamu ya Sita ambayo hata mwaka haina au ndio Legacy kwa Vitendo hii?

4. Au mambo haya yanafanyika kwa maksudi mazima ili kumdhoofisha Rais Samia Suluhu Hassan na Serikali yake?

5. Je nikweli Rushwa imekithiri awamu ya Sita au nihadaa tu wanafanya kwa Wananchi ili wasimwamini Rais Samia ?

6. Mnaotetea Legacy ya Hayati Dkt John Joseph Pombe Magufuli kwa kutafuna mali za umma kwani yeye alipenda Rushwa na Ufisadi?Msitafute laana,

NB: Uwekeni Uzalendo wa Taifa letu mbele kuliko masilahi yenu binafsi kwani nchi hii ni kubwa kuliko yeyote kila mmoja aupinge Ufisadi toka ndani ya moyo wake
,
 
Dawa ya hii Mama bila kuwatazama usoni awafute wote

Huwezi kuongoza kwa Staff iliyowekwa na mtangulizi wako never

Mama weka watu wapya wenye Dira na Mwelekeo wako otherwise hawa wataharibu huku wakijiondoa,

#Kaziiendelee
 
Hayo maswali kamuulize mzee wa Msoga, ilikuwaje aliachiwa nchi hazina ikiwa imeshiba lakini mpaka anatoka ilikuwa nyeupe?

Kiongozi legelege hufanya watu wawe legelege,maana hawawezi kufanya zaidi ya uwezo wa kiongozi.

Hujawahi kujiuliza watoto akiwepo baba adabu inajaa gunia,ngoja wabaki na mama Sasa,adabu nusu debe.
 
Kondoo hawezi kuongoza zizi lenye wanyama aina zote, SSH ni mweupe, hana dira wala maono, siku zinavyopita ndio anazidi kuonyesha udhaifu wake kichwani.
 
Kwani ata Magufuli aliwafuta wote wa Jakaya? Wapo aliwakuta na akaawacha kama Mataragio kamkuta na kamuacha! Wakina Prof Janabi etc
 
Magufuli ndiye Rais fisadi Papa wa muda wote kwani haijawahi kutokea tokea uhuru Rais akapiga ufisadi wa TZS 1.5 trilioni ndani ya awamu moja ya uongozi.

Ufisadi aliopiga Magufuli ni mkubwa kuliko ufisadi wote wa awamu zote nne za nyuma yake ukijumlisha kwa pamoja.

Sifa na utukufu zimwendee CAG Profesa Musa Assad ambae alifanya kazi nzuri sana ya kuibua ufisadi ule.

Mama yupo sahihi kusema kuwa awamu ya tano ndiyo walikuwa mafisadi papa na ukweli lazima usemwe.

20211206.jpg
1638703545.jpg
 
Hayo maswali kamuulize mzee wa Msoga, ilikuwaje aliachiwa nchi hazina ikiwa imeshiba lakini mpaka anatoka ilikuwa nyeupe? Kiongozi legelege hufanya watu wawe legelege,maana hawawezi kufanya zaidi ya uwezo wa kiongozi. Hujawahi kujiuliza watoto akiwepo baba adabu inajaa gunia,ngoja wabaki na mama Sasa,adabu nusu debe.
Ndio watajua hawajui, Mama apige chini kila jizi hata kama ni mia moja kaiba
 
Back
Top Bottom