Kukosa umakini wa kutoa taarifa kuhusu majanga kidunia

Mama Mdogo

JF-Expert Member
Nov 21, 2007
2,961
2,139
Ndugu wanajamvi,

Nimefuatilia hotuba ya Waziri Nauye wakati akiwa mkoani Tabora akisisitiza kuwa TBC ni lazima ibadilike iwe na umakini wa hali ya juu wa kufuatilia matukio ndani na nje ya nchi, na ikiwezekana iwe ni ya kwanza kuripoti.

Hata hjivyo hadi leo niko najiuliza hii TBC imeshindwa kutoa taarifa na kuwaeleza Watanzania kuhusu maafa ya tetemeko la ardhi lililotokea siku ya Ijumaa tarehe 15.04.2016 huko nchini Japani katika Mkoa wa Kyushu, Kumamoto Prefecture lenye kiwango cha 7 Ritcher na kuua watu 32.

Vilevile bado TBC iko kimya kuhusu tetemeko la ardhi liliotokea leo huko pwani ya Ecuador lenye kiwango cha 7.8 Ritcher na kuua watu 238. Mimi nafikiri kwa kuwa haya ni maafa ni matokeo muhimu yaliyopawswa kupewa umuhimu na TBC. Nawasilisha!!!
 
Back
Top Bottom