Elections 2010 Kuelekea uchaguzi 2010: Tanzania tunahitaji viongozi bora na si bora viongozi

MANI

Platinum Member
Feb 22, 2010
7,320
6,376
Wana jamvi, katika kipindi hiki ambacho tunaelekea uchaguzi mkuu watanzania hatuna budi kutafakiri kuwa tumetoka wapi,tupo wapi na tunaenda wapi.Maana ya kusema kuwa tunahitaji viongozi bora na si bora viongozi ni kutokana na kuwa nchi yetu iliacha kuwa na viongozi bora baada ya kuvunja azimio la Arusha. Ndani ya azimio la Arusha kulikuwa na miiko na maadili ya uongozi kiasi kwamba viongozi waliwajibika kama maadili yanvyotaka. Kiongozi bora ni yule ambaye yupo tayari kusimamia rasilimali na ustawi wa anaowaongoza. Mara baada ya uhuru mpaka miaka ya mwanzoni mwa miaka ya 80 serekali yetu iliyokuwa na viongozi bora iliweza kutoa huduma bora za jamii pasipo malipo,kama elimu,afya nk. Lakini baada ya kuwa tumeua azimio hilo la Arusha hakukuwa na maadili yoyote na bora viongozi wakawa wako pale kwa maslahi yao binafsi na sio kwa umma ulio nyuma yao. Ndio maana baada ya hapo tumeweza kushuhudia mambo ya ajabu kutokana na kashafa mbalimbali juu ya fedha za umma,UFISADI,EPA NA MATUMUZI YA KUFURU.

Kwani chini ya viongozi bora nchi yetu ikiwa na watu wachache na vyanzo vichache vya kodi na kiwango kidogo cha kodi tuliweza kukusanya pesa ambazo kwa namna moja au nyingine zilirudi kwa wananchi kwa kupitia huduma walizopatiwa,tuliowahi tulisoma toka shule ya msingi mpaka vyuoni bila wazazi wetu kuchangia chochote zaidi ya nguo za shule tu. Viongozi bora walihakikisha kuwa kidogo tunachopata kinatumiwa na wote kwa faida ya wote.

Sasa baada ya kuwa na bora viongozi ni kuwa pamoja na kuwa vyanzo vya kodi vimeongezeka na viwango pia lakini hicho kinachokusanywa hatukioni kupitia huduma za jamii. Watoto wetu wanakaa sakafuni kwenye majengo ambayo hayana hata hadhi ya kuwa darasa lakini viongozi wanatumia magari ya kifahari na zana za kifahari. Ni kutokana na hilo tabaka la walionacho na wasionacho linazidi kukuwa kiasi ambacho ni hatari kwa usalama na ustawi wa taifa letu.

Kuna wapo ambao watakuwa na hoja ya kuwa hayo yaliwezekana kwa kuwa idadi yetu ilikuwa ndogo lakini naomba tuelewe hapo mwanzo kama ambavyo nilisema hapo awali tulikuwa na vyanzo vichache na viwango vidogo lakini sasa tunavyo vyanzo vingi na viwango vikubwa ni kwa nini hatuendelei? Chini ya viongozi bora tuliweza kujenga viwand a ambavyo vilikuwa vyetu wenyewe na serekali yetu ilikuwa inatumia pesa zetu wenyewe bila kusubiri msaada hata kwenye bajeti ya kawaida sikatai tulikuwa na misaada na mikopo lakini ilikuwa na kwa ajili ya maendeleo na sio uendeshaji.

Sasa wana jamvi kabla ya kupiga kura naomba tutafakari na kujiuliza wapi tumetoka wapi tupo na ni wapi tunataka kwenda na bila kusahau kuwa je tuendelee kuongozwa na bora kiongozi au kiongozi bora ambaye atasimamia mapato yetu kwa nidhamu na kufanya maisha yetu yawe na ahueni au tuendelee na hawa wanaotumia kama kwamba hakuna wa kuhudumiwa na serekali, bali matumizi yasiyo na msingi kama kuishi kama tupo kwenye dunia ya utajiri.

Kwa hayo naomba kuwakilisha "TUTAFAKARI NA KUAMUA"
 
Back
Top Bottom