Kuelekea miaka 60 ya Muungano, NEMC yasisitiza umuhimu wa kufanya tathimini za athari za Mazingira kwenye uanzishwaji wa miradi

Nyakijooga

Senior Member
Dec 9, 2018
133
226
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), limeendelea kuwasisitiza wananchi wanaotaka kuanzisha miradi mbalimbali kuzingatia tathmini ya Athari kwa Mazingira ili kuepuka changamoto za uharibifu wa mazingira na kuchukuliwa hatua za kisheria endapo wataenda kinyume.
IMG-20240420-WA0005.jpg

Hayo yameelezwa na Afisa Elimu Jamii mwandamizi wa Baraza, Suzan Chawe kutoka Kurugenzi ya tathimini ya athari za Mazingira ambaye amesema kuwa bado kuna changamoto kwa baadhi ya wadau kuanzisha miradi bila kuzingatia utaratibu wa kisheria wa kufanya tathimini elekeze.

"Bado kuna changamoto ya miradi inayoanza kufanyika bila kufuata tathimini za athari za Mazingira lakini mingine haifanyi ukaguzi ili wapate cheti cha tathimini ya athari kwa Mazingira"amesema Suzan

Amedai "Hii ni changamoto kubwa kwa sababu baadhi ya maeneo ambapo miradi inaazishwa unakuta miradi haikupaswa kuwepo au haikupata baadhi ya vigezo, kwahiyo wengi kama wanakiuka Sheria ya mazingira"

Amesema kuwa wananchi hususani wadau wanaoanzisha miradi ni muhimu kutumbua suala hilo kwa kuwa ni takwa la kisheria ambapo miradi kabla ya kuanzishwa inalekezwa ifanyike tathimini ya athari za Mazingira kabla ya kuanza utekelezaji (kupitia kifungu cha 81 cha Sheria ya Mazingira namba 20 ya mwaka 2004 (Sura 191)

Baraza kupitia Suzan limeeleza kuwa umuhimu mwingine wa tathimini elekezi ni pamoja na kuwezesha kuweka mipango ambayo itaendelea kulinda mazingira katika nyakati tofauti kulingana na uendelevu wa mradi husika.
IMG_20240420_213859_053.jpg

Hata hivyo katika kuwezesha mazingira rafiki kwa wanaotaka kuanzisha miradi, Baraza linasimamia miradi inayofanya Tathmini ya Athari kwa Mazingira (TAM) kwa njia ya mtandao kupitia (eia.nemc.or.tz) ambapo njia hii inamuwezesha mwekezaji kuanzisha mchakato wa (TAM) au ukaguzi wa Mazingira (EA) kupitia mfumo wa usimamizi wa mradi (PMS).

Aidha baadhi ya malengo ya kuanzishwa kwa mfumo huo yameainishwa wazi kuwa ni pamoja na kuongeza ufanisi, kupata taarifa sahihi kutoka kwa wataalamu wa Mazingira, kuboresha utunzaji wa kumbukumbu, kuwezesha utengano wa majukumu kati ya mshauri na mwekezaji.

Lakini pia miongoni mwa matarajio ya Baraza ambayo wanatarajia yapatikane kupitia mfumo huo ni kupunguza malalamiko kutoka kwa mwekezaji kwenda kwa mtaalamu elekezi, kuboresha uwajibikaji sambamba na kuongeza uwazi.

Vilevile katika kuhakikisha jamii inaendelea kupata uelewa namna Baraza hilo linavyoendesha masuala mbalimbali ikiwemo mfumo huo, maonesho ya biashara ya miaka 60 ya Muungano katika viwanja vya Mnazi Mmoja ambayo yalianza April 19, 2024 huku yakitarajiwa kuhitimishwa April 25, 2024.

Katika maonesho hayo ikiwa ni kuelekea miaka 60 ya Muungano NEMC wanatoa fursa ya wadau kuelewa miradi wanayoitekeleza ili kulinda mazingira katika nyanja mbalimbali, mfano kati ya miradi hiyo ni pamoja na, Mradi kupunguza matumizi ya Zebaki kwenye uchimbaji kwenye uchimbaji uchimbaji mdogo wa madini ya dhahabu nchini.

Ambapo mradi huo unatekelezwa kwenye mikoa ya Geita, Mwanza Mara, Shinyanga Singida, Mbeya na Songwe. Mingine ni mradi wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi katika jamii za wakulima na Wafugaji, ambapo mradi huo unatekelezwa Wilaya ya Kongwa.
IMG_20240420_213831_997.jpg

Mradi wa kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi kwa wakazi wa Pwani, ambapo mradi huo unatekelezwa Pwani na Zanzibar, mwingine ni Mradi wa uvunaji maji wa kimkakati wa kuwezesha uhimili wa mabadiliko ya Tabianchi kwa wakazi wa vijijini kwenye sehemu kame za katikati ya Tanzania, ambapo mradi huu unatekelezwa Dodoma, Singida na Tabora. mwingine ni Mradi wa kubadili mabadiliko ya tabianchi, ambao unatekelezwa Wilaya ya Bunda.

Pamoja na hiyo miradi mingine ni, mradi wa uhifadhi na usimamizi wa Mazingira bonde la Kihansi, Mradi wa Energy Sector Capacity building Project (ESCBP).

Ikiwa ni kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano NEMC inawapa fursa na kuwakaribisha wadau kutembelea banda lao kufahamu juu ya miradi hiyo na mambo mengine ambayo wamekuwa wakiyatekeleza.

Sanjari na hayo Baraza linasisitiza wananchi pamoja na wadau kuendelea kuzingatia Sheria ya Mazingira ili kujiepusha na kuepusha changamoto mbalimbali.
 
Back
Top Bottom