SoC03 Kuboresha Mfuko wa Bima ya Afya

Stories of Change - 2023 Competition

Kidaya

Member
Dec 20, 2011
55
50
Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) ulianza kufanya kazi Julai, 2001 kwa waajiriwa wa serikali kuchangia 3% ya mishahara yao na mwajiri kuchangia 3%. Mpaka kufikia Desemba 2019, mfuko wa Bima ya afya ulikuwa na wanufaika 4,856,062 sawa na 9% ya watanzania wote. Majukumu ya mfuko ni kuwaandikisha wanachama na kuwapatia vitambulisho, kukusanya michango, kuidhinisha watoa huduma za afya wa kuwahudumia wanufaika wa mfuko, kulipa madai ya watoa huduma, kuwekeza ili kupata faida, kufanya tathmini na kutoa elimu ya bima ya afya kwa umma.

Mfuko huu umekuwa na mchango mkubwa katika uendeshaji wa vituo vya afya ambapo 70% ya fedha za huduma za hospitali za umma na binafsi zinategemea mfuko huu. Pamoja na umuhimu huo kwa wanaufaika wa mfuko na vituo vya afya, mfuko umekumbwa na changamoto zinazotishia uhai wa mfuko zinazotokana na matumizi makubwa yasiyoendana na mapato kama ilivyobainishwa na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu (Mb) mwezi Septemba, 2022.

Ili kuunusuru mfuko huu na kuujengea uwezo wa kutimiza majukumu yake kwa mafanikio zaidi, ni muhimu kubuni njia za kuongeza mapato na kupunguza matumizi kama ifuatavyo;

A. Kuongeza mapato

1. Kuongeza wanachama

a) Sheria ya ulazima wa kuchangia 3% ya mishahara kwa wafanyakazi isiishie kwa watumishi wa umma bali ipanue wigo na kuwafikia waajiriwa wote wa taasisi binafsi wenye mikataba ya ajira, mfano waajiriwa wa viwandani, makampuni ya uchimbaji madini, usafirishaji, mawasiliano, taasisi za kifedha, afya, vyombo vya habari n.k. Kama mtumishi wa umma mwenye mshahara wa Tsh. 300,000 kwa mwezi anachangia Tsh. 9,000 ni wazi kuwa waajiriwa wa makampuni na taasisi zingine nao wanaweza kuchangia.

b) Sheria ya ulazima wa kuwa na bima ya afya iwahusu pia wasanii na wanamichezo kwani ni kundi ambalo liko hatarini kuugua kutokana na asili ya kazi zao, safari za mara kwa mara na maisha ya anasa. Kundi hili hupata fedha nyingi kwa kipindi kifupi, hivyo wanaweza kuchangia kiasi cha fedha kitakachowapatia huduma za bima ya afya kupitia kwenye mikataba ya kazi yao.

c) Sheria ya ulazima wa kuwa na bima ya afya iwahusu wanafunzi wa shule hadi vyuo vyote. Baadhi ya shule au vyuo kuna mchango wa matibabu, mchango huu uboreshwe na kuwa mchango wa bima ya afya badala ya kuwa utaratibu wa shule au chuo fulani pekee.

2. Kuwa na kifurushi cha watu maalum (VIP) - Watu maarufu na wenye fedha nyingi hawapendi foleni na mizunguko katika vituo vya afya hivyo inawalazimu kuwa na Bima za Afya za makampuni binafsi ili kupata huduma kwa haraka. Uwepo wa huduma hii utavutia watu wa kundi hili kujiunga na mfuko wa NHIF ulio na vituo vingi vya kuhudumia wanufaika wake tofauti kuliko bima za makampuni binafsi zinazotumika kwa vituo vichache vya afya nchini.

3. Kuwa na tozo ya afya katika bidhaa zinazochangia ongezeko la magonjwa yasiyoambukiza ambayo kwa kiasi kikubwa ndiyo yanayotishia uhai wa mfuko. Tozo hii itumike kusaidia matibabu ya wanachama watakaopata magonjwa hayo kama saratani, magonjwa ya moyo, figo, kisukari, ajali n.k. Bidhaa hizi ni kama tumbaku na mazao yake, pombe, vinywaji vyenye sukari, vyombo vya moto na vipuri vyake.

B. Kupunguza matumizi

1. Kuweka bei za huduma zinazolipwa na NHIF kuendana na bei ya soko. Kwakuwa wanufaika wa Bima ya Afya huhudumiwa kwa utaratibu wa mkopo (huduma leo, malipo baada ya mwezi au miezi kadhaa baadae), bei ya huduma za Bima ya Afya zisizidi 5% ya bei ya soko (pendekezo hili nimerejea riba ya mkopo wa mshahara anaokopeshwa mtumishi na benki anayopitishia mshahara) tofauti na sasa ambapo baadhi ya bei za huduma za Bima ya Afya ni kubwa kwa zaidi ya 50% ya bei ya soko.

2. Bei za huduma ya afya zisitegemee ngazi ya hospitali. Kumuona daktari akiwa hospitali ya wilaya au kliniki kuna tofauti gani na kumuona daktari huyohuyo akiwa hospitali ya Taifa? Kipimo kikifanyika hospitali ya wilaya kina tofauti gani na kikifanyika hospitali ya mkoa au taifa? Kuwa na bei moja ya huduma kutaupunguzia mfuko gharama zinazoongezeka kutokana na utofauti wa ngazi za hospitali. Hili liliwahi kusemwa pia na madaktari katika kikao chao na Rais wa Awamu wa Tano mwezi Februari, 2020.

3. Kutumia kitambulisho cha NIDA badala ya kutengeneza kadi za wanufaika wa mfuko kwani mnufaika akienda hospitali kupewa huduma, jina lake tu ndio linahitajika kutoka kwenye kadi ili kumtafuta kwenye mfumo . Kwa mfano, kama kutengeneza kadi moja inagharimu Tsh. 10,000 kutengeneza kadi kwa wanufaika milioni 4.8 waliopo inagharimu Tsh 48,000,000,000. Kutumia kitambulisho cha NIDA kutaokoa fedha za kutengenezea vitambulisho vya wanufaika wa mfuko.

C. Maeneo mengine ya kuboresha

1. Mfuko uhudumie gharama zote za huduma za kiafya anazohitaji mnufaika tofauti na sasa ambapo baadhi ya huduma, vipimo au dawa za magonjwa fulani vinalipiwa kwa kiasi fulani au havilipiwi kabisa. Hili hurudisha nyuma jitihada za kuhamasisha watu kujiunga na mfuko.

2. Mfuko uwe na vifurushi viwili tu, cha kawaida na cha watu maalum (VIP). Utofauti wa vifurushi uwe kwenye uharaka wa huduma na huduma za ziada kama kulazwa wodini na sio kwenye kupata huduma za msingi, jambo linalopoteza maana ya kuwa na bima ya afya.

3. Kutumia teknolojia ya alama za vidole kutaondoa udanganyifu na kupunguza gharama za ukaguzi na uhakiki wa wanufaika. Teknolojia pia itapunguza muda wa kushughulikia madai na kuharakisha ulipaji wa madai ya watoa huduma.

4. Kuzingatia utekelezaji wa adhabu kali kwa watu na vituo vya afya vinavyofanya udanganyifu ili kujipatia mapato isivyo halali.

Kwa kuwa Bima ya Afya kwa wote bado ni kitendawili kutokana na vipato duni vya wananchi (26.4% wanaishi chini ya mstari wa umaskini) na gharama kubwa za huduma za afya zisizo rahisi kubebwa na Serikali, na kama kwa miaka 20 ya NHIF ina wanufaika 9% tu ya wananchi wote, ni vema mfuko ukawa na lengo linalotekelezeka kama la kuongeza wanufaika hadi 50% ya watanzania wote ifikapo mwaka 2030 kwa kuyafanyia kazi maoni niliyopendekeza ya kuusaidia mfuko wa Bima ya Afya kuwa imara kiuchumi ili kutimiza majukumu yake kwa mafanikio.

Rejea:
Takwimu rasmi zilizozotumika katika andiko hili ni kwa mujibu wa tovuti ya Mfuko wa Bima ya afya.
 
Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) ulianza kufanya kazi Julai, 2001 kwa waajiriwa wa serikali kuchangia 3% ya mishahara yao na mwajiri kuchangia 3%. Mpaka kufikia Desemba 2019, mfuko wa Bima ya afya ulikuwa na wanufaika 4,856,062 sawa na 9% ya watanzania wote. Majukumu ya mfuko ni kuwaandikisha wanachama na kuwapatia vitambulisho, kukusanya michango, kuidhinisha watoa huduma za afya wa kuwahudumia wanufaika wa mfuko, kulipa madai ya watoa huduma, kuwekeza ili kupata faida, kufanya tathmini na kutoa elimu ya bima ya afya kwa umma.

Mfuko huu umekuwa na mchango mkubwa katika uendeshaji wa vituo vya afya ambapo 70% ya fedha za huduma za hospitali za umma na binafsi zinategemea mfuko huu. Pamoja na umuhimu huo kwa wanaufaika wa mfuko na vituo vya afya, mfuko umekumbwa na changamoto zinazotishia uhai wa mfuko zinazotokana na matumizi makubwa yasiyoendana na mapato kama ilivyobainishwa na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu (Mb) mwezi Septemba, 2022.

Ili kuunusuru mfuko huu na kuujengea uwezo wa kutimiza majukumu yake kwa mafanikio zaidi, ni muhimu kubuni njia za kuongeza mapato na kupunguza matumizi kama ifuatavyo;

A. Kuongeza mapato

1. Kuongeza wanachama

a) Sheria ya ulazima wa kuchangia 3% ya mishahara kwa wafanyakazi isiishie kwa watumishi wa umma bali ipanue wigo na kuwafikia waajiriwa wote wa taasisi binafsi wenye mikataba ya ajira, mfano waajiriwa wa viwandani, makampuni ya uchimbaji madini, usafirishaji, mawasiliano, taasisi za kifedha, afya, vyombo vya habari n.k. Kama mtumishi wa umma mwenye mshahara wa Tsh. 300,000 kwa mwezi anachangia Tsh. 9,000 ni wazi kuwa waajiriwa wa makampuni na taasisi zingine nao wanaweza kuchangia.

b) Sheria ya ulazima wa kuwa na bima ya afya iwahusu pia wasanii na wanamichezo kwani ni kundi ambalo liko hatarini kuugua kutokana na asili ya kazi zao, safari za mara kwa mara na maisha ya anasa. Kundi hili hupata fedha nyingi kwa kipindi kifupi, hivyo wanaweza kuchangia kiasi cha fedha kitakachowapatia huduma za bima ya afya kupitia kwenye mikataba ya kazi yao.

c) Sheria ya ulazima wa kuwa na bima ya afya iwahusu wanafunzi wa shule hadi vyuo vyote. Baadhi ya shule au vyuo kuna mchango wa matibabu, mchango huu uboreshwe na kuwa mchango wa bima ya afya badala ya kuwa utaratibu wa shule au chuo fulani pekee.

2. Kuwa na kifurushi cha watu maalum (VIP) - Watu maarufu na wenye fedha nyingi hawapendi foleni na mizunguko katika vituo vya afya hivyo inawalazimu kuwa na Bima za Afya za makampuni binafsi ili kupata huduma kwa haraka. Uwepo wa huduma hii utavutia watu wa kundi hili kujiunga na mfuko wa NHIF ulio na vituo vingi vya kuhudumia wanufaika wake tofauti kuliko bima za makampuni binafsi zinazotumika kwa vituo vichache vya afya nchini.

3. Kuwa na tozo ya afya katika bidhaa zinazochangia ongezeko la magonjwa yasiyoambukiza ambayo kwa kiasi kikubwa ndiyo yanayotishia uhai wa mfuko. Tozo hii itumike kusaidia matibabu ya wanachama watakaopata magonjwa hayo kama saratani, magonjwa ya moyo, figo, kisukari, ajali n.k. Bidhaa hizi ni kama tumbaku na mazao yake, pombe, vinywaji vyenye sukari, vyombo vya moto na vipuri vyake.

B. Kupunguza matumizi

1. Kuweka bei za huduma zinazolipwa na NHIF kuendana na bei ya soko. Kwakuwa wanufaika wa Bima ya Afya huhudumiwa kwa utaratibu wa mkopo (huduma leo, malipo baada ya mwezi au miezi kadhaa baadae), bei ya huduma za Bima ya Afya zisizidi 5% ya bei ya soko (pendekezo hili nimerejea riba ya mkopo wa mshahara anaokopeshwa mtumishi na benki anayopitishia mshahara) tofauti na sasa ambapo baadhi ya bei za huduma za Bima ya Afya ni kubwa kwa zaidi ya 50% ya bei ya soko.

2. Bei za huduma ya afya zisitegemee ngazi ya hospitali. Kumuona daktari akiwa hospitali ya wilaya au kliniki kuna tofauti gani na kumuona daktari huyohuyo akiwa hospitali ya Taifa? Kipimo kikifanyika hospitali ya wilaya kina tofauti gani na kikifanyika hospitali ya mkoa au taifa? Kuwa na bei moja ya huduma kutaupunguzia mfuko gharama zinazoongezeka kutokana na utofauti wa ngazi za hospitali. Hili liliwahi kusemwa pia na madaktari katika kikao chao na Rais wa Awamu wa Tano mwezi Februari, 2020.

3. Kutumia teknolojia katika kadi za wanufaika kwa kuunganisha taarifa za bima ya afya na kitambulisho cha NIDA. Kwa mfano, kama kutengeneza kadi moja inagharimu Tsh. 10,000 kutengeneza kadi kwa wanufaika milioni 4.8 waliopo inagharimu Tsh 48,000,000,000. Kutumia namba za NIDA kwa utambulisho wa Bima ya Afya kutaokoa fedha za kutengenezea vitambulisho vya wanufaika wa mfuko.

C. Maeneo mengine ya kuboresha

1. Mfuko uhudumie gharama zote za huduma za kiafya anazohitaji mnufaika tofauti na sasa ambapo baadhi ya huduma, vipimo au dawa za magonjwa fulani vinalipiwa kwa kiasi fulani au havilipiwi kabisa. Hili hurudisha nyuma jitihada za kuhamasisha watu kujiunga na mfuko.

2. Mfuko uwe na vifurushi viwili tu, cha kawaida na cha watu maalum (VIP). Utofauti wa vifurushi uwe kwenye uharaka wa huduma na huduma za ziada kama kulazwa wodini na sio kwenye kupata huduma za msingi, jambo linalopoteza maana ya kuwa na bima ya afya.

3. Kutumia teknolojia ya alama za vidole kutaondoa udanganyifu na kupunguza gharama za ukaguzi na uhakiki wa wanufaika. Teknolojia pia itapunguza muda wa kushughulikia madai na kuharakisha ulipaji wa madai ya watoa huduma.

4. Kuzingatia utekelezaji wa adhabu kali kwa watu na vituo vya afya vinavyofanya udanganyifu ili kujipatia mapato isivyo halali.

Kwakuwa Bima ya Afya kwa wote bado ni kitendawili kutokana na vipato duni vya wananchi (26.4% wanaishi chini ya mstari wa umaskini) na gharama kubwa za huduma za afya zisizo rahisi kubebwa na Serikali, na kama kwa miaka 20 ya NHIF ina wanufaika 9% tu ya wananchi wote, ni vema mfuko ukawa na lengo la kuongeza wanufaika hadi 50% ya watanzania wote ifikapo mwaka 2030 kwa kuyafanyia kazi maoni niliyopendekeza ya kuusaidia mfuko wa Bima ya Afya kuwa imara kiuchumi na kutimiza majukumu yake kwa mafanikio.

Rejea:
Takwimu rasmi zilizozotumika katika andiko hili ni kwa mujibu wa tovuti ya Mfuko wa Bima ya afya.
Nzuri
 
Hakuna watu wanafirisi NHIF kama hawa ma specialists uchwara kwenye vi clinic vyao!!!

Wafanyakazi wa NHIF, kama walivyo watanzania wa bandalini.

Solution ni DP World tu, waje mapema waanza na CCM
 
Hakuna watu wanafirisi NHIF kama hawa ma specialists uchwara kwenye vi clinic vyao!!!

Wafanyakazi wa NHIF, kama walivyo watanzania wa bandalini.

Solution ni DP World tu, waje mapema waanza na CC
Kliniki zipo kwa ajili za kusogeza huduma za afya karibu zaidi na wananchi na kupunguza msongamano kwenye mahospitali Mkuu.
 
Taarifa ya hali isiyoridhisha ya mfuko wa NHIF kama ilivyoripotiwa na JF
 
Attachments

  • IMG_20230821_111319.jpg
    IMG_20230821_111319.jpg
    98 KB · Views: 14
Huu uzi una miezi mitatu lakini wachangiaji ni wachache.

Weka uzi unaohusu kula kimasihara uone watanzania tusivyo na akili
 
Back
Top Bottom