Kongole kwa Rais Samia Suluhu Hassan

zagarinojo

JF-Expert Member
Jul 26, 2020
2,622
2,836
Hizi ni salamu zangu za dhati kutoka uvunguni ndani ya Moyo wangu zimfikie popote alipo Madam President. Wapo waliosema Pengo lake John P..Halitazibika ILA umetuonesha uthubutu halisi ulionao.

Wengine walidhani mwanamke hawezi kuliongoza Taifa kubwa kama Hili hasa lenye ndoto za kuyafikia Mafanikio yaliyotabiriwa na Mababu waliomwaga Damu zao kwa ajili ya UHURU wa Nchii hii...

Aliwahi Kusema Muasisi Wa Taifa Hili J.K Nyerere kwenye Moja ya Hotuba zake nanukuu"Chama/Kiongozi Atakaye puuza maoni ya wananchi anaweza kulia Machozi asipatikane mtu wa kumpangusa Machozi"

Ni Dhahiri kuwa usemi huu umeuzingatia kwa kuwa kwa sasa wananchi wako huru na unafanya like wananchi wanachotaka na unawasikiliza..

Nimefurahishwa na Jinsi Ambavyo umesema ukweli kwamba Nchi yetu bado ni Masikini haiwezi kusimama yenyewe bila kutegemea msaada kutoka kwa Wahisani..Hivyo ni vyema tukope Ili tumalize miradi kisha deni tutalipa kwa Pamoja kama Watanzania..

Nilifurahi pia niliposikia kuwa kwa sasa Watoto wa kike wenye ujauzito ambao wenda waliupata bila kujitakia wanaweza kwenda shule na kuendelea na masomo kwasababu ni haki yao..

Nimefurahishwa pia na pale ulipowafumbua macho watanzania kuwa kila Kitu Kitapanda bei kutokana na hali halisi ya Dunia kwasasa kushamiri kwa Vita.. Hivyo serikali haina makosa katika hili..Naam watanzania ni waelewa naimani wamekuelewa..

Lakini pia nimefurahishwa na pale uliposema ukweli kuwa si lazima serikali itoe ajira KILA mwaka kwani Hata Vijana wanao uwezo wa kujiajiri kwasababu walioko Serikalini wengi wamepandishwa vyeo na Madaraja hivyo kuajiri wapya itakuwa ni kuongeza matumizi...

Lakini pia hata pale uliposema tozo ya shilingi mia kwenye bei ya mafuta iongezwe kwani tayari bajeti ilikuwa imeshatengwa...Hii inaonesha kiasi Gani una msimamo naimani wananchi ni waelewa watakuwa wamekuelewa..

Umenifurahisha pia na safari zako za nje kwenda kutufungulia Tanzania milango nje ya Nchi hata lile la Tanzania kuonekana kwenye Jengo refu Duniani Burj Khalifa limenikosha sana naamini kwasasa wanatujua...


Nimeandika Waraka Huu huku Machozi yananilenga..Sijui ni kwanini Ila Wakuyafuta Machozi alishatangulia.....

BIG up Madam President You're doing a great Job
 
Hakika anastahili pongezi:
• Upigaji umerudi kwa kasi isiyomithilika

• Maisha yamezidi kuwa magumu, ajira hakuna hata pale Watanzania wanapojiongeza na kutafuta kipato kupitia Umachinga wamefukuzwa kama mbwa

• Vifo vinavyosababishwa na uzembe wa wafanyakazi wa umma na ajali vipo juu kuliko wakati wowote

• Mfumuko wa bei upo juu kuliko kipindi chochote kwa miaka zaidi ya sita iliyopita

• Madaraka wanapeana kwa urafiki na kujuana

• Deni la taifa linakua kwa kasi ya ajabu

• Wauza madawa ya kulevya na mafisadi wanatamba mitaani sasa hivi

• Uhalifu umeongezeka

• List ni ndefu sana.

Nani kama mama?
 
Acheni sifa madam anaupiga kmya kimya .nyie ndo mlimvimbisha kichwa kayafa hata kama alikuw anatesa watu mnampa utakatifu.achen unafik chapa kazi
 
Hakika anastahili pongezi:
• Upigaji umerudi kwa kasi isiyomithilika

• Maisha yamezidi kuwa magumu, ajira hakuna hata pale Watanzania wanapojiongeza na kutafuta kipato kupitia Umachinga wamefukuzwa kama mbwa

• Vifo vinavyosababishwa na uzembe wa wafanyakazi wa umma na ajali vipo juu kuliko wakati wowote

• Mfumuko wa bei upo juu kuliko kipindi chochote kwa miaka zaidi ya sita iliyopita

• Madaraka wanapeana kwa urafiki na kujuana

• Deni la taifa linakua kwa kasi ya ajabu

• Wauza madawa ya kulevya na mafisadi wanatamba mitaani sasa hivi

• Uhalifu umeongezeka

• List ni ndefu sana.

Nani kama mama?
 
Hakuna kama mama,Kila anaekata rufaa kesi za madawa ya kulevya na kesi zingine zote Anashinda rufaaa,Hakuna kama mama.
Nafurahi siku nikija Dar arena ya Wasanii itakuwa tayari na Treni ya Umeme pia sina hakika kama Umeme utakatika wakati Treni iko Katika mwendo...
 
Ukitaka kufa mapema na kununa kila saa fuatilia siasa na uongozi wa taifa hili... Siku hizi sifuatilii habari zozote zinazohusiana na mambo ya sirikali labda nikutane nazo humu.
Kuna mambo yanaumiza nafsi na kuyabadilisha huwezi. Watu wengine wako wanapiga vigelegele
Labda ipo siku kilio chao atakisikia Mola muumba Mbingu
 
Lazima ulieandika hii ni mwanamke. Eti unafurahishwa na tozo,sijui unafurahishwa na kupanda gharama kwa kila kitu. Ng'ombe ni wengi
 
Back
Top Bottom