Kitimtim comedy imulikwe

Kumbe upo bongo
Hapana, kwa sasa niko nchini Zambia nikifanya kazi ya muda mfupi consultancy, baadaye naenda Namibia. Huko home Tanzania narudi mwezi wa September 2023, nikirudi naenda moja kwa moja kijijini kwangu mkoa wa Katavi nimeyamis sana makande na maziwa ya mtindi. Mtu kwao, nafustilia tamthlia za bongo kupitia Mydstv applications huku huku nje ya nchi. Naomba usaidie kupaaza sauti, kuna maudhui yenye ukakasi huko Kitimtim, na drama zingine.
 
Kabla ya kurushwa huhakikiwa na hilo ndilo lalamiko kuu
Ni kweli, na ninakubaliana na wewe, lakini lalamiko hilo lingeelekezwa kwa wahariri wa ndani au DSTV wenyewe, na si wizara, baraza la sanaa na TCRA. Wahariri wa ndani ndiyo hupitia maudhui kabla ya kipindi kurushwa hewani.
 
Sasa Dr. Mariposa, saa tatu usiku ya jana, hadi saa moja na dakika ishirini na nane asubuhi ya leo, kweli Mama Mdogo anaweza walau wizara, Baraza la Sanaa na TCRA kwamba hawajafanya lolote..!!?? Wangefanyia kazi muda gani..!!??
Hao wadau, hasa Baraza la Sanaa huwa linapelekewa script kabla, wanasoma na kupitisha, kuboresha au kukataa. Shooting na recording zinaanza kwa kutumia script iliyopitishwa na baraza. Ina maana huo upuuzi wa jana umebarikiwa na baraza. Sijui kuhusu TCRA wanafanya monitoring muda gani. Lakini ninavyofahamu chombo kikiisema vibaya serikali au kuzodoa viongozi wakuu, within 24 hours TCRA inakuwa imechukua hatua. Sasa kwa hii episode ya Kitimtim ya kuombana ngono sijui na wao wanafurahishwa na hizo ngono au la, hata sijui.
 
Natoa rai kwa mamlaka husika (Wizara ya utamaduni na michezo, Baraza la ssna ka taifa, TCRA etc) kufuatilia kwa umakini maudhui ya Kitimtim comedy inayoneshwa kwenye chanel 160 DSTV/Multichoice.

Wameanza kuongelea mambo ya kufanya ngono kwa uwazi hadi inatia aibu mzazi kuangalia skiwa na watoto au wajukuu wake. Kipindi cha jana tarehe 15/05, kuna episode wahusika wawili wanaagizwa waingie ndani wapeane haki yao ya ndoa. Mara mhusika mmoja anasema hajatahiriwa, mara wasanii wengine huku nje wanashabikia walioko ndani wafanye ngono haraka.

Haya yote yanafanyika wakati Wizara ipo, Baraza la Sanaa lipo, na TCRA wapo.Very sarcastic and un professional.
Mbona kawaida
 
Je mwanzo wa kipindi hicho hawakuweka maelezo ya unero sahihi wa kutazama kipindi hicho? Kama wameweka maelezo hayo (ambayo kwa unachosema ni umri wa miaka 16 anaruhusiwa kutazama) basi hawawezi kufungiwa
 
Kwanini umewaza watoto tu?
Je unaweza kuangalia maudhui ya hivyo ukiwa na wazazi au ndugu au wakwe?
Kwanini huja weka Itv Tbc,, aljazeera, tumaini tv, imaan tv n.k

Hizo nyengine unazolalamikia ni chaneli za burudani, lengo lao kuvutia watazamaji, ambao miongoni mwao ni watu wasiotazama tivii na wakwe na watoto

kama hupendi maudhui yake kuna option ya kuzipinga password, kwanini hujaweka pass word?
 
Sijui hata kama umeelewa mada inahusu nini,
Isome tena kwa utulivu
 
Je mwanzo wa kipindi hicho hawakuweka maelezo ya unero sahihi wa kutazama kipindi hicho? Kama wameweka maelezo hayo (ambayo kwa unachosema ni umri wa miaka 16 anaruhusiwa kutazama) basi hawawezi kufungiwa
Ni kweli, kama wameweka PARENTAL CONTROL ambayo inahusisha umri, na yeye hajaweka hicho kitu hilo ni lake..!! Unfortunately, hakuna control inayoweza kuwekwa kwamba wewe na mkweo msikae kuangalia maudhui ya kikubwa kwenye TV moja. Hili la mtu kukaa na mama yake au baba yake au baba/mama mkwe ni la muhusika..!!
 
Back
Top Bottom