Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 21,642
- 52,460
Habari wakuu!
Hichi kinachoendelea ni moja ya Maendeleo makubwa ambayo Kwa awamu ya tano isingewezekana, serikali ipongezwe Kwa kurejesha Maendeleo haya ya Watu kuwa Huru.
Kimsingi nchi inaamani, inautulivu, Watu wanaparangana na kutoa Maoni Yao Kwa Amani bila ya hofu. Unajua kuna Watu wanaweza wasielewe Jambo hili(wala sio kosa Lao), Kwa Sababu ni kawaida kutolewa Jambo ambalo huna uzoefu nalo.
Mambo ya Bandari yaendelee kujadiliwa, serikali ichukue hatua stahiki Kwa kuboresha maeneo ambayo yanaleta utata Kwa Watanzania Kwa maslahi ya Taifa.
Hata hivyo niseme tuu kuwa Uhuru huu wa Maoni uendane na uwajibikaji na kusikiliza Maoni yaliyobora. Na sio uwe Uhuru WA Maoni yanayopuuzwa. Hiyo itahesabika kama dharau, kudharau wananchi. Na sidhani kama serikali makini yenye viongozi Bora wanaweza kukubali kuwa na Sifa Mbaya kama hiyo.
Ninawatakia maandalizi Mema ya Sabato.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam