Kilio kwa waajiriwa wote mwakani kutoka TRA

Mkuu acha kupotosha au kama hujui uliza uelimishwe. Ofisini kwangu ( Private sector) tumeanza kutumia TIN tangu mwezi wa 8 mwaka huu baada tu ya TRA kutoa mwongozo. Hiyo TIN hakuna makato yanayoongezwa kwenye mshahara wako isipokua ile pesa unayokatwa kodi ( PAYE) ndio sasa italipwa kupitia TIN yako na sio manually kama inavyolipwa sasahivi. Hii imefanyika ili ku control mapato yanayopatikana kupitia kodi za wafanyakazi. So usitishe watu Mkuu.
I think ni internal control within TRA tu

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
 
Nadhani serekali imeshatangaza Kuwa hakuna mtu atalipwa mshahara bila kuwa na TIN number .

Tatizo ni kwa watumishi ambao ulikua na TIN number ya biashara na ulifunga biashara na hukuenda TRA kuifunga iyo TIN kuwa biashara huendelei nayo. TRA wanapiga mahesabu ya pesa yao kwa miaka yote ambayo hukulipa na ongezeko la riba juu. Pesa yote wanajua wanakukata pindi mwajiri anapokulipa had watakapo maliza.

Wengi wamekuta TIN zinadaiwa mamilioni na huwezi kubadilisha iwe non business TIN hadi ulipe pesa yote. Mwajiri hatoweza kukulipa mshahara hadi umpe TIN na pia huwez kuwa na TIN zaidi ya moja.

Ubaya ni kuwa pia TIN number yako ina link had na account yako ya bank so hakuna namna yakukwepa.

MAKATO NAYOYAONA MWAKANI
1. PAYE
2. NSSF
3.LOAN BOARD.
4.TIN PAYMENTS.
5. NHIFView attachment 1630910
Safi sana naomba utabiri wako utimie. Itakua vizuri sana nchi ijengwe na kila mtu.
Mitano tena
 
Kuna jamaa alikuwa na biashara, baadae akaifunga na kwenda biashara ya kununua mazao ambayo haikuhitaji chochote. Baada ya kama 5 yrs akanunua gari kwa mtu, sasa kimbembe kwenda kubadili kadi ya gari TRA wakamdaka kwamba ana deni kubwa mpaka alilipe... Alihangaika weee mwishowe wale vishoka wa TRA sijui walimpa mbinu gani akawakatia mpunga ndo akafanikiwa kubadili kadi...
Kuna watu hawajawai kukutana na ili sele seke hawawezi kukuelewa boss. Sheria ya kuingilia mshahara moja kwa moja inaweza isiwepo ila kuna sheria inayowaruhusu TRA kufanya makubaliano na wewe namna utakavyolipa na sio kwamba usilipe kabisa. Mimi siwez kuwa nakudai labda milioni 1 alafu hunilipi na wakati naona kila mwezi unalipa kodi ya zaidi ya laki 3 au 5 na nisikutengenezee utaratibu wakunilipa namimi.

Huu utaratibu utakuja tu ni swala la muda January sio mbali .
 
Mleta Uzi Kajichanganya, Kilichobaki Anajihami Kwa Kuwaona Wenye Mawazo Tofauti Wana Uelewa Mdogo!!!!
Hapana mkuu siwezi kukuona una uwezo mdogo ni sijasema mawazo yangu nisahihi. Ila utakapoleta hoja namimi naweka hoja yangu ili majadiliano yaendelee kupitia hayo kuna mtu anajifunza hata kama hachangii. Na hata tunaochangia tunajifunza pia na kuongeza kitu kutoka kwenye mitazamo tofauti.
 
Mbona niko private na sijaombwa Tin number?

Haya mambo yanakuja kimitego mitego halafu baadae mnapigwa penalty bila sababu.

Kama kuna mtu wa TRA humu aseme,je,wameshatoa maelekezo hayo kwa taasisi binafsi ama ni kwa watumishi wa serikali tu?

Iwapo mmetoa taarifa kwa taasisi zisizo za kiserikali,na sisi wafanyakazi hatujaombwa hizo Tin ijapo tunazo,tufanye nini au kuna hatua zipi zinafuata?Maana hivi Sasa hii nchi tunaogopa maana hata ukiviziwa hakuna anayetetea.
 
Naomba kuelimishwa, hiyo TIN itakayo tumika kulipia kodi yangu kutoka kwenye mshahara wangu nitapewa ili niweze kuitumia kufanya mambo mengine kama biashara, leseni nk au itabaki tu ya kulipia kodi?
 
Naomba kuelimishwa, hiyo TIN itakayo tumika kulipia kodi yangu kutoka kwenye mshahara wangu nitapewa ili niweze kuitumia kufanya mambo mengine kama biashara, leseni nk au itabaki tu ya kulipia kodi?
Iyo iyo moja inatumika kwenye kila kitu .
 
Kama ndivyo Serikali ilitakiwa kuziandaa hizo TIN na kuzigawa kwa waajiriwa!! Mbona kama wanamlazmisha mtumishi yeye ndo apange folen TRAKwa ajili ya hiyo kitu!!!!!

Nashaur sirikali isumbukie yenyewe kutoa TIN NAMBA kwa waajiriwa wasokuwa nazo
 
Labda km sio serikali ya huyu jamaa isiyopenda watumishi.Kila mara wanabuni mbinu za kuwabana watumishi.
 
Mkuu acha kupotosha au kama hujui uliza uelimishwe. Ofisini kwangu ( Private sector) tumeanza kutumia TIN tangu mwezi wa 8 mwaka huu baada tu ya TRA kutoa mwongozo. Hiyo TIN hakuna makato yanayoongezwa kwenye mshahara wako isipokua ile pesa unayokatwa kodi ( PAYE) ndio sasa italipwa kupitia TIN yako na sio manually kama inavyolipwa sasahivi. Hii imefanyika ili ku control mapato yanayopatikana kupitia kodi za wafanyakazi. So usitishe watu Mkuu.
Hili jambo inabidi TRA walitolee ufafanuzi na si kuleta press release. Hapa udhaifu mkubwa umeonekana ktk public relations.
Jambo zito wanatoa taarifa kisanii.
 
Wewe ndo hujaelewa kilichoandikwa. Makato yatakua makubwa kwa mfanyakazi ambaye alikua na biashara na akaifunga iyo biashara na hakuweza kuandika barua kwa TRA ya kufunga iyo TIN . Kwasasa analizimika kutumia TIN iyo kwa mwajiri na TRA ndipo watakapoona malimbikizo ya kodi na kuanza kukukata kila unapolipwa
Sasa hapo nani alaumiwe
 
Kama ndivyo Serikali ilitakiwa kuziandaa hizo TIN na kuzigawa kwa waajiriwa!! Mbona kama wanamlazmisha mtumishi yeye ndo apange folen TRAKwa ajili ya hiyo kitu!!!!!

Nashaur sirikali isumbukie yenyewe kutoa TIN NAMBA kwa waajiriwa wasokuwa nazo
Tin Number Unaipata Katika Website Ya TRA, 2 Minutes And Its Done.
 
Nadhani serekali imeshatangaza Kuwa hakuna mtu atalipwa mshahara bila kuwa na TIN number .

Tatizo ni kwa watumishi ambao ulikua na TIN number ya biashara na ulifunga biashara na hukuenda TRA kuifunga iyo TIN kuwa biashara huendelei nayo. TRA wanapiga mahesabu ya pesa yao kwa miaka yote ambayo hukulipa na ongezeko la riba juu. Pesa yote wanajua wanakukata pindi mwajiri anapokulipa had watakapo maliza.

Wengi wamekuta TIN zinadaiwa mamilioni na huwezi kubadilisha iwe non business TIN hadi ulipe pesa yote. Mwajiri hatoweza kukulipa mshahara hadi umpe TIN na pia huwez kuwa na TIN zaidi ya moja.

Ubaya ni kuwa pia TIN number yako ina link had na account yako ya bank so hakuna namna yakukwepa.

MAKATO NAYOYAONA MWAKANI
1. PAYE
2. NSSF
3.LOAN BOARD.
4.TIN PAYMENTS.
5. NHIFView attachment 1630910
Tena hao waalimu Wakatwe tu maana waliipenda wenyewe
 
JINSI YA KUPATA TIN NAMBA TOKA TRA

Swali: Nini maana ya TIN?
Jibu: TIN ni namba ya utambulisho kwa mlipakodi.

Swali: Inatumika kwenye vitu gani?
Jibu: TIN inatumika kwenye matumizi ya biashara na yasiyo ya biashara.

Swali: Matumizi yasiyo ya biashara ni yapi?
Jibu: Matumizi hayo ni pamoja na ajira, umiliki wa chombo cha moto, leseni za udereva na kadhalika

Swali: Kwa hiyo TIN inayotokana na ajira inakuwa siyo ya biashara?
Jibu: Ndiyo

Swali: Kwanini imeletwa jambo hili mnalihitaji hivi sasa
Jibu: Kila anayelipa kodi anapaswa kuwa TIN na muajiriwa analipa kodi kutokana na ajira yake.

Swali: Inamaana kodi itaongezeka ?
Jibu: Hapana makato ya kodi yatakuwa yale yale.

Swali: Ikiwa mimi ninayo TIN tayari kuna haja ya kupata TIN kwa ajili ya ajira?
Jibu: Hapana TIN hiyo ya mwanzo ndio itatumika na TIN huwa ni moja kwa mtu mmoja.

Swali: Mimi nina leseni ya udereva TIN yangu nitaijuaje.
Jibu: Fika katika ofisi yoyote ya TRA utapata TIN yako.

Swali: Ikitokea sina kabisa TIN?
Jibu: Unaweza kuipata kwa kuingia www.tra.go.tz kisha usajili wa TIN, weka namba ya NIDA na namba ya simu kisha jaza taarifa zako utapata TIN.

Swali: Ikiwa sina namba ya NIDA nafanyaje?
Jibu: Fika ofisi ya TRA na kitambulisho cha kura au barua ya serikali ya mtaa, utachukuliwa alama za vidole na kupata TIN yako.

Swali: TIN inapatikana kwa bei gani?
Jibu : TIN ni bure kabisa hakuna malipo yoyote.

Swali sasa ninayo ya biashara inatumika?
Jibu: Itatumika kwa sababu inayohitajika ni TIN .

Swali: Nikishapata TIN nitaifanyia nini?
Jibu: Kwa wewe muajiriwa ipeleke kwa muajiri wako aweze kuijaza katika taarifa ya makato ya kodi kwa waajiriwa.

USIPOELEWA HAPO NENDA OFISI ZA TRA.
 
Back
Top Bottom