Kilimo cha Mihogo (Cassava): Mbinu, Ushauri, Changamoto na Masoko yake

Mkuu mikoa yote ya Pwani muhogo unakubali vizuri tu ila kama utapenda kuwa mdau kwa eneo letu au ungependa kuzalisha ili tununue ningeshauri ili kupunguza ghrama za usafirishaji ni nzuri kama utaelekea barabara ya Kilwa maeneo ya kuanzia Mkuranga kuelekea njia ya Mtwara hadi karibu na Mbuga ya Selous maeneo yapo wazi sana mkuu na yanakubali muhogo ile mbaya. Tutahitaji muhogo uingie kwenye mashine kabla ya kuzidi umri wa siku 3 tangu kuvunwa ambayo najua hiyo ni feasible kabisa kwa sehemu kubwa ya Tanzania kufikisha kiwandani.

So Mlandizi pia sio mbali nimeongelea kupanua profit margin kwa kupunguza transportation costs tu hapo
What about fukayosi mkuu? Mhogo unaota?
 
wataalam pia tuombe mtusaidie kujua aina gan ya mbegu ni bomba!, tayar niko kazini. Kuna watalaam weng hapa lakn naona msimu unakaribia wako shamban, akina malila , ngoshwe n.k! Hawasikk

Kweli kabisa nilikuwa shamba, nimeona vitu vizuri ktk safari ya shamba niliyokwenda

Nirudi ktk topic, mbegu zimeshatajwa hapo juu. Kimanzichana panaweza kuwa pazuri sana kwa sasa kwa ajili ya kufungua mashamba makubwa ya mhogo, kule nyuma ya mji kuna eneo kubwa lililotupu. Na mkuu Ngeleja anapeleka moto pale,siku si nyingi moto utawaka. Kididimo ni pazuri, bado mafisadi hawajafika na kuharibu bei. Maeneo ya Hoyoyo Mkuranga ni mazuri,tatizo wakubwa wameshalamba mapande makubwa,unaweza ukauziwa kipande cha mtu.
 
Kweli kabisa nilikuwa shamba, nimeona vitu vizuri ktk safari ya shamba niliyokwenda,
Nirudi ktk topic, mbegu zimeshatajwa hapo juu. Kimanzichana panaweza kuwa pazuri sana kwa sasa kwa ajili ya kufungua mashamba makubwa ya mhogo, kule nyuma ya mji kuna eneo kubwa lililotupu. Na mkuu Ngeleja anapeleka moto pale,siku si nyingi moto utawaka. Kididimo ni pazuri, bado mafisadi hawajafika na kuharibu bei. Maeneo ya Hoyoyo Mkuranga ni mazuri,tatizo wakubwa wameshalamba mapande makubwa,unaweza ukauziwa kipande cha mtu.

Malila asante, mim nilikuwa huko maeneo ya mlegele pwan kule mhogo unakubal tatizo ni wanyama waharibifu!, kididimo iko maeneo gani? je eka 1 bei gan?, wakubwa wamekamata mashamba huko pwan sijawah ona!
 
niona umeme uko njia moja, pia na value ya ardhi imepanda sana maeneo ya njia kuu kwenda m/mango ambapo 1acre ni 1mil. Nimetembelea vijiji kadhaa huko kisarawe, na kujionea hal halisi.Kuna vijiji vina rutuba sana.
 
malila asante, mim nilikuwa huko maeneo ya mlegele pwan kule mhogo unakubal tatizo ni wanyama waharibifu!, kididimo iko maeneo gani?, je eka 1 bei gan?, wakubwa wamekamata mashamba huko pwan sijawah ona!.

Kididimo iko Mkuranga,mara baada ya kupita kijiji cha Mbezi njia ya kisiju kabla ya kufika Mpafu, panalimwa sana tikiti. Nikipata bei yake nitaiweka peupe mkuu. Maji ya kubangaiza yapo.

Ukanda wa pwani una nyani balaa,nguruwe pori ni wengi sana. Tusikate tamaa.
 
niona umeme uko njia moja, pia na value ya ardhi imepanda sana maeneo ya njia kuu kwenda m/mango ambapo 1acre ni 1mil. Nimetembelea vijiji kadhaa huko kisarawe, na kujionea hal halisi.Kuna vijiji vina rutuba sana.

Kisarawe bei imepanda sana, week jana nilikwenda Visegese, kuna ardhi kubwa sana, ina rutuba, barabara nzuri ipo, kunajengwa plant ya saruji, lakini kuna ukame ile mbaya. Kunafaa kwa makazi, barabara hiyo inaunganisha Kisarawe na Kiluvya. Huko ni ardhi ya kilimo hakuna mchanga, wanyama kama ng`ombe wa kisasa nimewaona, ila mbuzi wako vizuri. Maji ni ya malambo kwa sasa. Mapori mengi yana wenyewe, usiende kichwa kichwa.
 
Wana JF, naombeni msaada kwa mwenye uzoefu na utaalamu wa kilimo cha mihogo. Ninaomba msaada katika mambo yafuatayo.
1. Kama kuna aina tofauti za mihogo na maeneo inakostawi vizuri
2. Msimu ambao mihogo inapandwa ni miezi ipi?
Je? Inaweza kupandwa misimu yote ya mwaka?
3. Mihogo inashambuliwa na magonjwa yapi? na kama upo uwezekano wa kuzuia hayo magonjwa?
4. Mihogo inachukua muda gani hadi kuvunwa?
5. Hekari moja inaweza kutoa magunia mangapi?

Natanguliza shukrani zangu za dhati kwa wote watakaonisaidia kwa mchango wa uzoefu na utaalamu katika eneo hili. Kwa pamoja uchumi wa Tanzania utasonga mbele.
 
Kuna member anaitwa Mzuzu atakusaidia. Ana project kubwa sana ya zao la mihogo.
 
Wana JF, msaada wa mawazo tafadhali kuhusu thread hapo juu nipo serious sana kufanya hii shughuli, Many thanks.
 
Asante Mpwa, subiri wanywe chai wanakuja, mie mmmhhh wee acha tu
 
my step mom is kulima mihogo....whats this all about kuna mtu anaweza kunitafsiria na kunisamarazia.....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom