Mgalula MzTz
JF-Expert Member
- Jul 3, 2013
- 457
- 411
Unafikiri bila ukatili angeweza kuyafanikisha yote aliyoyaanzisha?Dikteta alikuwa vizuri tatizo lake ilikuwa ni ule ukatili wake
Fikiria swala la watumishi hewa tumeishi nalo kwa miaka nenda rudi inamaana watangulizi wake hawakulijua.
Kiongozi legelege huzalisha Taifa legelege na hapo ndipo wananchi hubaki wakiogelea kwenye dimbwi la ufukara huku wanasiasa na wafanyabiashara wakubwa wakitajirika.
Mimi nilishawahi kuambatana na Mh Hamfrey Polepole kipindi ni mkuu wa wilaya kibamba kwenda kwenye taasisi moja ya selikali kudai mafao ya mzazi wangu na kufanikiwa kuyapata, sina hakika kama hiyo dhana ya uwajibikaji ipo mpaka leo.
Itoshe tu kusema Tz ilimuhitani sana huyu mzee.
Tulikuwa kwenye mchakamchaka wa kimapinduzi hasa,kuanzia kwenye viwanda,.miundombinu,kuondokana na utegemezi wa misaada kwa kulinda na kutegemea lasrimali zetu kupitia secta za madini kwa kuzuia utoroshwaji na mikataba ya kinyonyaji,na mambo mengine mengi tu.
Leo hii ukiniuliza dira yetu ni ipi, kwakweli sijui hata tumedhamilia nini ili tufike wapi kama Taifa.
Kwa sasa selikali na mwananchi wa kawaida ni kama mbingu na aridhi.