Kesi ya Jerry Muro

"Muro alinitishia kuwa yeye ni afisa wa jeshi na ana nyota tatu amesomea Uingereza na Marekani, alifungua dashboard ya gari na kutoa pingu, akaniambia nikileta fujo atanifunga, alinitolea na bastola na kuniambia pia ikishindikana kunidhibiti ananipiga risasi kwa kutumia bastola hiyo," alidai.
Difficult to prove..........it is his word against mine.......no witnesses........no video cameras etc....................amounting to no evidence at all..............
 
"Baada ya kumaliza kuwapatia sh milioni moja, niliingia kwenye gari la Murro akaenda kunishusha mgahawa wa Best Bite na tutakubaliana kesho yake tukutane kwenye mgahawa wa City Garden ulioko mtaa wa Mkwepu… Nikapanda kwenye gari langu nikaenda nyumbani kwangu Bagamoyo nikawaeleza ndugu zangu kuhusu tukio la mimi kutishiwa bastora na kuombwa rushwa; wakaniambia nikatoe taarifa polisi….na kweli Januari 31 mwaka jana, nilivyokuja Dar es Salaam nilifikia moja kwa moja kituo kikuu cha Polisi Kati huku mfukoni nikiwa na sh milioni tisa," alidai Wage.

Ushahidi wa kutoa hongo ya milioni moja utamwumiza mtoa hongo kwa sababu mtoa na mpokea hongo wote ni mafisadi tu...............Ingawaje si rahisi kuthibitisha Mahakamani ya kuwa ukiwa pekee yako ulitoa hongo ya kiasi hicho na fedha hizo hivi sasa hazijulikani zilipo....na hazina namba za Takukuru chombo amacho kina ridhaa ya kuchunguza makosa ya rushwa...................
 
Polisi waliingilia kazi za Takukuru za kuchunguza rushwa na hili laweza kuwa la msaada mkubwa kwa Murro kama atalijengea hoja vizuri.....polisi walipaswa kuliwakilisha suala hili Takukuru na kwa kutofanya hivyo..............dai la Murro kuwa polisi wamemtumia mtuhumu ili kumkomoa kutokana na kuitekeleza kazi yake vyema ambako kunawakwaruza polisi na hivyo kunuia kumbambikizia kesi linaweza kuwa hoja ya kisheria ya kumtoa kwenye hili sakata....................

It all boils down to whom will the Hon. Magistrate believe..........................It is a criminal case of one man against three...........Who is more credible between the two sides?............

Hoja ya kwamba polisi waliingilia kazi za TAKUKURU haina mashiko na ni hoja dhaifu. Makosa yote ya jinai(rushwa ikiwemo) yanaainishwa ktk CPA na sheria nyingine zote zinazodili na jinai(PCCA 2007) ikiwemo, zinafanya kazi within the boundaries of CPA. Kwa hiyo kwa polisi kuzuia au kumkamata mtoa au mpokea rushwa na kumfikisha mahakamani ni sahihi kabisa though TAKUKURU wapo. Pia polisi wanaweza kumkamata mtu anayekwepa kodi though TRA wapo, kama wanavyoweza kuwakamata wahamiaji haramu ingawa Uhamiaji wapo.

Kumbuka kwamba unapoongelea jinai yoyoteile unaongelea Polisi. N a ndio maana sheria iliyounda TAKUKURU i.e PCCA inamtambulisha Afisa wa TAKUKURU pindi anapofanya kazi zake kuwa anakuwa na mamlaka ya polisi.

Kwa msingi huo, polisi walikuwa sahihi kabisa na hakuna kosa lolote walilolifanya kwa kutokuripoti TAKUKURU.

Lakini pia hata usipoongelea sheria. Bado polisi wanakuwa na uwezo wa kudili na rushwa na makosa mengine ya jinai(ingawa kuna mamlaka zingine zilizopewa nguvu ya kusimamia sheria nyingine), kwa kuwa polisi wana mtandao mkubwa sana tofauti na TAKUKURU ambayo mtandao wake umeishia wilayani tu.

In short, ukiongelea jinai yoyote ile, huwezi kuwatenga polisi hata kama kuna mamlaka nyingine yenye nguvu kisheria.

I STAND TO BE CORRECTED
 
Ushahidi wa kutoa hongo ya milioni moja utamwumiza mtoa hongo kwa sababu mtoa na mpokea hongo wote ni mafisadi tu...............Ingawaje si rahisi kuthibitisha Mahakamani ya kuwa ukiwa pekee yako ulitoa hongo ya kiasi hicho na fedha hizo hivi sasa hazijulikani zilipo....na hazina namba za Takukuru chombo amacho kina ridhaa ya kuchunguza makosa ya rushwa...................

Ref, nilipo-red! Ni kweli mtoa na mpokea rushwa wote ni wakosaji: NI KWELI. Lakini pia kuna exceptions kwa mtoa rushwa/mpokea rushwa ikiwa tu, baada ya kitendo kile(cha kutoa/kupokea) anawahi kwenda kutoa taarifa katika mamlaka husika.
Kama polisi/TAKUKURU wangepata taarifa za rushwa(kati ya Muro na Wage) kwa njia zao wenyewe basi mtoaji na mpokeaji wangekuwa katika hot soup.

Kwa Wage kuwahi kutoa taarifa ni dhahiri kuwa alilazimishwa na hakuhiari.
 
Mtego wa jerry Muro wawekwa bayana


Na Rabia Bakari

SHAHIDI wa nne katika kesi ya kuomba rushwa ya sh. milioni 10 inayomkabili aliyekuwa mtangazaji wa kituo cha televisheni cha TBC1, Bw. Jerry Muro na

wenzake, Inspekta Msaidizi wa Polisi Issa Seleman (37) ameieleza mahakama jinsi alivyoweka mtego na kufanikiwa kumkamata Bw. Muro.

Inspekta Seleman alidai hayo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wakati kusikilizwa ushahidi mbele ya Hakimu Mkazi, Bw. Gabriel Mirumbe anayesikiliza kesi hiyo.


Akiendelea kutoa ushahidi wake huku akiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Bw. Boniface Stanslaus alidai mnamo Januari 30,2010, majira ya saa 4:00 asubuhi, akiwa kwenye kazi za nje alipokea simu kutoka kwa Sajenti Gervas ikimtaarifu kuwa kuna watu wamemtishia na kumuomba rushwa ya sh. milioni 10, Mhasibu wa Halmashauri ya Bagamoyo, Michael Wage.


"Baada ya kupata taarifa hizo, nilikwenda ofisini na kumkuta Sajenti Gervas akiwa na Wage ambaye alinieleza malalamiko yake ya kutishiwa na kuombwa rushwa ya sh. milioni 10 na Muro," alidai shahidi huyo.


Aliongeza kudai kuwa baada ya kuyasikiliza malalamiko hayo, aliwasiliana na viongozi wake akiwepo Mkuu wa Upelelezi mkoa wa Ilala, SSP Duwan Nyanda ambaye alimuamuru kufungua jalada la uchunguzi na utaratibu wa kuwakamata Bw. Muro na wenzake ufuatwe.


Baada ya kupata maelezo hayo, Inspekta Seleman alidai kuwa walifungua jalada la uchunguzi na kumtaka Bw. Wage awasiliane na watu waliomtisha na kumuomba rushwa mbele yao.


Alidai wakati wanawasiliana na Bw. Muro, Bw. Wage alimtaka wakutane katika geti la TBC lakini akakataa na kumtaka wakutane Bamaga.


"Lakini nilimwambia Wage ampigie Muro amwambie kuwa wakutane kesho yake yaani Januari 31, 2010 saa 4 asubuhi katika Goteli ya City Garden.


"Siku hiyo ilipofika mimi kama Inspekta wa zamu, niliamuru Sajenti Omar na Koplo Masaka wakae nje ya hoteli na mimi na Sajenti Gervas tubakie ndani ya hoteli hiyo," aliongeza kudai.

Alidai kuwa nyakati za saa 6 mchana, Muro aliwasili hotelini hapo na kumtaka Wage atoke nje ya hoteli hiyo ili waonane na kwamba iliwabidi wao wajipange kwa kutumia ishara.


Wage alibeba sweetcase kutaka kuingia ndani ya gari la Muro lakini kabla hajaingia nilimuamuru ashuke na nikamuuliza Muro kama anamfahamu Wage, yeye akajibu kuwa hamjui ila Wage yeye alisema anamfahamu Muro na ni mmoja kati ya watu waliokuwa wakimtisha na kumuomba rushwa,� alidai Inpekta Seleman.


Aidha katika ushahidi wake alikiri kuwa hakuwahi kumuhoji Bw. Muro wala kumpekua katika gari yake.


Shahidi wa tano katika kesi hiyo, Inspekta Anthony Mwita (45) alidai mahakamani hapo kuwa Februari 2, 2010 alikwenda katika Hoteli ya Sea Cliff kuonana na Meneja wa Kitengo cha IT ili awapatie picha za kamera za CCTV za watu waliongia na kutoka Januari 29, 2010.


Pamoja na kuangalia picha za CCTV, pia alidai kukagua kitabu cha kumbukumbu ya wageni na kilikuwa na kumbukumbu ya usajili wa gari la Muro lenye namba za usajili T 545 DEH aina ya Cresta ambalo lilipewa kadi namba 673 ya hoteli hiyo ya Sea Cliff ambalo liliingia saa 7:33 mchana na kutoka saa 8:48 mchana.


Pia katika ushahidi wake, alidai kuwahi kukabidhiwa stakabadhi ya kununulia pingu yenye namba 34357310 aliyoinunua kwa sh 25,000 katika duka la jeshi la Mzinga lililopo Upanga Mei 26, 2009, ambapo pia baada ya kufanya upelelezi katika duka hilo, walinithibitisha kuwa ni kweli duka hilo lilimuuzia pingu.


Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Bw. Deogratius Mgasa na Bw. Edmund Kapama ambao wote kwa pamoja wanakabiliwa na kesi ya kuomba rushwa, na kujivika vyeo bandia.Kesho hiyo inaendelea leo kwa mashahidi upande wa mashtaka kuendelea kutoa ushahidi wao.




1 Maoni:

blank.gif

justine said... si mnaona wanavyojichanganya wenyewe
January 25, 2011 10:31 PM
 
Askari aieleza Mahakama Muro alivyonaswa mtegoni

Imeandikwa na Regina Kumba; Tarehe: 26th January 2011 @ 07:46

SHAHIDI wa nne katika kesi ya kupokea rushwa, askari Issa Chabu (37), amedai kumshuhudia aliyekuwa mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Jerry Muro, alivyokwenda kupokea rushwa kutoka kwa mlalamikaji Michael Wage.

Akitoa ushahidi wake jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Chabu alidai alipokea simu kutoka kwa askari aliyemtaja kwa jina moja la Gervas , Januari 30, mwaka jana na kutaarifiwa kuwa kuna watu walimtishia na kumuomba rushwa Wage ambaye alikuwa Mtunza Hazina wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo.

Mbele ya Hakimu Mkazi Gabriel Mirumbe, Chabu alidai kuwa baada ya kupokea taarifa hiyo, alirudi ofisini saa nane mchana na kumkuta Wage aliyedai kudaiwa rushwa hiyo ya Sh milioni kumi kwa vitisho akiwa kituo cha kati cha Polisi.

Baada ya hapo askari huyo alidai alipewa maelekezo na mkuu wake wa kazi kufungua jalada la uchunguzi na kuwakamata watuhumiwa ambao ni Muro na watu wengine wawili waliotajwa kuwa walijitambulisha kwa Wage kama maofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

Alidai alimwambia Wage ampigie Muro simu na wapange kuonana siku hiyo lakini baadaye aliahirisha na alimwambia Wage wafanye kazi ya kuwakamata kesho yake.

Kwa mujibu wa madai ya askari huyo, siku hiyo akiwa kituoni, Wage aliwasiliana na Muro na kukubaliana wakutane kwenye mgahawa wa City Garden karibu na klabu ya Bilcanas ili ampatie fedha hizo.

Askari huyo alidai Muro alikubali na alifika kwenye mgahawa huo ambao maaskari walikuwa wamejipanga kumkamata nje ya mgahawa na wengine ndani.

Shahidi huyo alidai Muro akiwa kwenye gari bila kujua mtego huo, alimpigia Wage simu kuwa atoke nje ya mgahawa huo na alipotoka alimuoneshea ishara aliko ili aende.

Kwa mujibu wa madai hayo, Wage alipofika kwenye gari la Muro kabla hajaingia ndani, mshitakiwa huyo alishtuka akataka kuingia kwenye gari aondoke lakini askari walimpa amri ya kutoondoka.

Chabu anadai alimuuliza Muro kama anamfahamu Wage lakini alikana na hivyo wakamuamuru kuendesha gari lake hadi kituo cha kati cha Polisi.

Kesi hiyo inaendelea leo mahakamani hapo.

 
Code:
Shahidi huyo alidai Muro akiwa kwenye gari bila kujua mtego huo,   alimpigia Wage simu kuwa atoke nje ya mgahawa huo na alipotoka   alimuoneshea ishara aliko ili aende.  

Kwa mujibu wa madai hayo, Wage alipofika kwenye gari la Muro kabla   hajaingia ndani, mshitakiwa huyo alishtuka akataka kuingia kwenye gari   aondoke lakini askari walimpa amri ya kutoondoka.

hapa kuna rushwa ipi?
 
Pingu za Jerry Muro zatolewa ushahidi mahakamani Wednesday, 26 January 2011 20:36

muro.jpg
Jerry Muro

Tausi Ally MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha TBC1, Jerry Muro, alimfunga pingu Mhasibu wa Halmashauri ya Bagamoyo, Michael Karoli wakati akimtisha na kumwomba rushwa ya Sh10 milioni.

Pingu hizo ambazo zilitolewa mahakamani hapo kama sehemu ya ushahidi, zilidaiwa kuwa zilikutwa kwenye gari la Muro wakati akikaguliwa na Inspekta wa Polisi.

Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, SSP Duwan Nyanda (49), alitoa madai hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi, Gabriel Mirumbe, wakati akitoa ushahidi katika kesi hiyo.

"Wage aliniambia kuwa pingu hizi zilitumiwa na Muro kumfunga wakati anamtishia na kumuomba rushwa,"alidai shahidi huyo wa sita wa upande wa mashtaka.

Nyanda alidai kuwa Januari 31,2010, Kamishna Msaidizi wa Polisi Charles Mkumbo, alimtaka asimamie upekuzi katika gari aina ya Toyota Cresta nyeupe ya inayodaiwa kuwa ya Muro.

Alidai kuwa alifanya upekuzi huo baada ya Wage kulalamika kuwa alitishiwa kufungwa pingu na Muro na pia alisahau miwani yake katika gari hilo, hivyo walitaka kuthibitisha kama ni kweli ndani ya gari hilo kulikumo na vitu hivyo.

"Nilipofanya upekuzi nilipata jozi moja ya miwani, ambayo Wage aliitambua kuwa ni ya kwake na jozi moja ya pingu ambayo Wage alidai kuwa ilitumika kumfunga wakati akitishwa na Muro," alidai Nyanda. Nyanda alidai kuwa baada ya kupata vitu hivyo aliviandika katika hati ya upekuzi ambayo Jerry aliisaini.

Alisema hati hiyo pia ilisainiwa na askari Lugano. Baada ya kueleza hayo, Nyanda aliiomba mahakama ipokee hati hiyo ya upekuzi, miwani na pingu kama sehemu ya vielelezo katika kesi hiyo edapo upande wa utetezi hautakuwa na pingamizi.

Mawakili wa utetezi, Richard Rweyongeza, Paschal Kamara na Majura Magafu walidai kuwa hawana pingamizi na vielelezo, hivyo mahakama ilivipokea kama vielelezo katika kesi hiyo.

Hakimu Mirumbe aliiahirisha kesi hiyo hadi Machi 7, mwaka huu itakapoendelea kusikilizwa ushahidi. Mbali na Muro kesi hiyo inawakabili Deogratius Mgasa na Edmund Kapama.
 
‘Nilikuta pingu, miwani kwenye gari la Murro'


na Happiness Katabazi


amka2.gif
MKUU wa Upelelezi wa Mkoa wa Ilala, Duani Nyanda, jana ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jinsi alivyopekua gari la Jerry Murro, anayetuhumiwa kuomba rushwa ya sh milioni 10 ambapo alikuta pingu na miwani ya kusomea.
Nyanda ambaye ni Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, ambaye pia ni shahidi wa sita katika kesi hiyo inayomkabili Murro, Kapama na Deo Mgassa, wanaotetewa na mawakili wa kujitegemea Richard Rweyongeza na Majura Magafu, alitoa ushahidi huo akiongozwa na Naibu Mkurugenzi wa Mashitaka nchini, Stanslaus Boniface, mbele ya Hakimu Gabriel Mirumbe.
Alieleza kuwa Januari 31 mwaka jana saa 12 jioni akiwa ofisini aliamriwa na aliyekuwa Mkuu wake, Charles Mkumbo, kwenda kulipekua gari la Murro lenye namba za usajili T 545 BEH Toyota Cresta lililoegeshwa kwenye viunga vya Kituo Kikuu cha Polisi.
"Baada ya kupewa jukumu hilo nilimchukua Murro ambaye alikuwa ofisini kwa Mkumbo na mashahidi wengine akiwamo Koplo Lugano Mwampeta na waandishi wa habari, nikaenda nao kwenye gari lake lilipokuwa limeegeshwa.
"Baada ya Murro kulifungua nikaanza upekuzi wa gari lile, kwa sababu polisi tulipata malalamiko kutoka kwa aliyekuwa Mhasibu wa Halmashauri ya Bagamoyo, Michael Wage, kwamba kuna watu akiwamo Murro walimtishia kwa pingu, bastola na kumwomba rushwa na kwamba Wage alisahau miwani yake katika gari la Murro," alidai SSP Nyanda.
Nyanda alieleza kuwa katika upekuzi wake alifanikiwa kupata pingu ambazo Wage alizibaini ndizo alizotishiwa nazo na Murro na miwani ya kusomea ambayo anadai ni yake aliisahau kwenye gari hilo Januari 30 mwaka jana na kuongeza kuwa alikuwa na hati ya polisi ambayo Murro na Wage walisaini kuthibitisha kushuhudia upekuzi huo na kuitoa mahakamani kama kielelezo namba tano kilichopokewa.
Pamoja na hati hiyo, pingu na miwani pia vilitolewa mahakamani kama vielelezo namba sita na saba. Kesi hiyo iliahirishwa hadi Machi 8 na 9 mwaka huu itakapoendelea.
 
Tatizo la polisi ni kuwa wao wanatoka wapi na kesi za rushwa?

kwa nini hawakuripoti Takukuru ili kuondoa dhana iliyojengeka ya kuwa polisi walimbambikizia kesi kwa kufanya kazi zisizo za kwao?

Hii hoja pekee inatosha kumwachia huru Jerry murro akaendelee na kutupasha habari bila ya zengwe lolote lile................................
 
PHP:
TAKUKURU ni wababaishaji hawajui hata wanachokifanya.

Hiki siyo kigezo cha polisi kuwanyang'anya majukumu yao ya kisheria.........................................
 
Hii kesi ni ya kubambikiziwa na huyu shahidi ushahidi wake unagongana......................Haiwezekani Murro ajitambulishe ni afisa wa TBC1 halafu tena ajigeuke utambulisho huo awe afisa wa Takukuru......................

Acheni unafiki na sympathy za ajabu . eti kabambikiwa. ushahidi wa kimazingira tu unaonyesha. hiyo miwani wakipima DNA wakakuta ni ya wage?

Simply muro alijisahau na inaonekana wengi walimpa rushwa. Bahatimbaya kwake siku za mwizi.
 
PHP:
TAKUKURU ni wababaishaji hawajui hata wanachokifanya.
Hiki siyo kigezo cha polisi kuwanyang'anya majukumu yao ya kisheria.........................................

Sheria gani inamkataza polisi kushughulikia makosa ya rushwa? Nijuavyo mimi polisi wanashughulikia kila kosa katika la jinai. Unaposema polisi walikosea, authority hiyo unaipata wapi? Usipotoshe. Makosa yote yale ya jinai ni wajibu wa polisi kuyashughulikia
 
Jerry Muro ana kesi ya kujibu


na Mwandishi wetu


amka2.gif
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, imemuona aliyekuwa Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji la TBC1, Jerry Murro na wenzake wanaokabiliwa na kesi ya kula njama, kushawishi na kuomba rushwa ya sh milioni 10, kuwa wana kesi ya kujibu.
Uamuzi huo wa kustua ulitolewa jana na Hakimu Mkazi Gabriel Mirumbe ikiwa ni muda mfupi baada ya shahidi wa sita wa upande wa Jamhuri, D/C Koplo Lugano Mwampeta kumaliza kutoa ushahidi wake na Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka nchini, Stanslaus Boniface kueleza kuwa wamefunga ushahidi.
Baada ya Naibu Mwendesha Mashtaka Boniface kueleza hayo, Hakimu Mirumbe alisema anaahirisha kesi hiyo kwa dakika kumi, ili aweze kupitia jalada la kesi hiyo na ushahidi wote uliokwishatolewa na mashahidi sita wa upande wa jamhuri kisha atarudi kutoa uamuzi wa ama washtakiwa wana kesi ya kujibu au la.
Ilipofika saa 6:47 mchana Hakimu Mirumbe aliingia kwenye chumba cha mahakama hiyo na kutoa uamuzi wake ambapo alisema baada ya kulipitia jalada la kesi hiyo mahakama imeona upande wa jamhuri umeweza kuthibitisha kesi yake na hivyo mahakama hiyo imewaona washtakiwa wote wana kesi ya kujibu.
“Baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na upande wa jamhuri katika kesi hii mahakama imewaona washtakiwa wote mna kesi ya kujibu na ninaaharisha kesi hadi Machi 29 ambapo washtakiwa mtaanza kukjitetea,” alisema Hakimu Mirumbe.
Awali, shahidi wa sita, D/C Koplo Lugano Mwampeta akiongozwa na Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka nchini, Boniface, kutoa ushahidi wake, alidai Januari 31, 2010 alikuwa ofisini katika ofisi za Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, ambapo mkuu wake wa kazi ambaye ndiye mkuu wa upelelezi wa mkoa huo(RCO)-Duwani Nyanda alimpatia kazi.
Mwampeta alieleza kuwa RCO-Nyanda alimpatia kazi ya kumsaidia kulikagua gari la Murro ambapo kiongozi wake huyo ndiye aliyekuwa mkaguzi mkuu, ambapo katika ukaguzi kwenye gari hilo walipata miwani na pingu na wakati wakifanya upekuzi huo Murro alikuwa akishuhudia.
Mbali na Murro, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Edmund Kapama na Deogratius Mugasa ambao wanadaiwa Februari 15 mwaka jana walikula njama kushawishi na kuomba rushwa ya sh milioni 10 kutoka kwa aliyekuwa Mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Michael Karoli Wage. Kati ya mashtaka matatu yaliyofunguliwa dhidi yao, Murro anakabiliwa na mashtaka mawili.
 
‘Muro na wenzake wana kesi ya kujibu' Send to a friend Tuesday, 08 March 2011 20:25
muro.jpg
Tausi Ally

JERRY Muro na wenzake Edmund Kapama na Deogratias Mgasa wamepatikana na kesi ya kujibu katika mashtaka matatu yanayowakabili likiwemo la kuomba rushwa ya Sh 10 milioni kutoka kwa Mhasibu wa Halmashauri ya Bagamoyo, Michael Kalori.

Mashtaka mengine yanayowakabili washtakiwa hao ni kula njama, na kujitambulisha kuwa wao ni maofisa wa serikali.

Uamuzi huo, ulitolewa jana na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam, Gabriel Mirumbe Mara baada ya Wakili wa Serikali Mkuu, Boniface Stanslaus kufunga ushahidi wao wa upande wa mashtaka.

Stanslaus alifunga ushahidi wa upande wa mashtaka mara baada ya mashahidi sita kati ya 11 waliotarajiwa kutoa ushahidi dhidi ya kesi hiyo, kutoa ushahidi wao.

Akitoa uamuzi kama Muro na wenzake wana kesi ya kujibu au la, Hakimu Mirumbe alisema baada ya kupitia vielelezo na ushahidi uliotolewa na mashahidi sita wa upande wa mashtaka washtakiwa wote wana kesi ya kujibu hivyo watatakiwa watoe utetezi wao.

Baada ya hakimu Mirumbe kutoa uamuzi huo, mawakili wa utetezi, Richard Rweyongeza, Majura Magafu na Pascal Kamala waliiomba mahakamani iruhusu wateja wao waanze kujitetea Machi 29, mwaka huu, kuanzia saa 4:00 asubuhi.

Hakimu Mirumbe alikubaliana na ombi hilo na kuiahirisha kesi hiyo hadi Machi 29, mwaka huu, Muro na wanzake watakapoanza kutoa utetezi wao dhidi ya mashtaka hayo yanayowakabili.

Wakili huyo wa Serikali Mkuu alifunga ushahidi wao mara baada ya shahidi wa sita, Koplo Lugano Mwampeta (32) kumaliza kutoa ushahidi wake dhidi ya kesi hiyo.

Akitoa ushahidi, Mwampeta alidai kuwa Januari 31,2010 nyakati za jioni akiwa ofisini kwake, Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam (RCO), Duwan Nyanda alimpa kazi ya kumsaidia kupekua gari la Muro.

Mwampeta alidai baada ya kupewa kazi hiyo, yeye na Nyanda walilipekuwa gari la Muro na kuwa walifanikiwa kupata miwani na pingu.

Aliongeza kudai kuwa wakati upekuzi huo ukiendelea kufanyika Muro alikuwepo na kwamba yeye mwenyewe kwa hiari yake alimkabidhi silaha aina ya Bastola na magazini inayobeba risasi 10.

Alidai Muro alikuwa ameiweka silaha hiyo kiunoni mwake na kwamba alipomkabidhi alizihifadhi kiofisi.
Hata hivyo shahidi huyo aliiomba mahakama ipokee vitu hivyo kama sehemu ya vielelezo vya ushahidi katika kesi hiyo na mahakama ilikubali baada ya upande wa utetezi kutokuwa na pingamizi navyo.

Akiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Boniface Stanslaus kutoa ushahidi wake, Mwampeta aliongeza kudai kuwa Februari 2, mwaka jana alichukua maelezo ya onyo kutoka kwa Muro na kwamba katika maelezo hayo, alikana kumtambua mlalamikaji katika kesi hiyo, Michael Kalori.

Muro ambaye ni mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha TBC1 na wenzake Edmund Kapama, maarufu kama ‘Doctor' pamoja na Deogratias Mgasa ambaye anajulikana kama Musa walipandishwa kizimbani Mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Februari 5, mwaka huu.

Awali wakili Stanslaus akishirikiana na Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Ben Lincoln, alidai kuwa washtakiwa hao walitenda kosa hayo Januari 29, mwaka jana.

Wakili Stanslaus alidai kuwa washtakiwa hao pamoja na wenzao wengine ambao hata hivyo hawajafikishwa mahakamani walitenda makosa hayo ya kula njama na kuomba rushwa kinyume cha kifungu cha 15 (1) (a) cha Sheria ya Kuzia na Kupambana na Rushwa ya mwaka 2007.

Stanslaus alidai kuwa Muro aliomba rushwa hiyo kutoka kwa Wage katika hoteli ya Sea Cliff Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, ili asimtangaze habari zake zinazohusiana na matumizi mabaya ya fedha za umma.

Aliongeza kuwa siku hiyo hiyo ya tukio washtakiwa Edmund Kapama na Deogratias Mgasa walijipachika nyadhifa zisizokuwa zao kwa kumlaghai Karoli kuwa wao ni maofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wakati wakijua ni uongo.

Washtakiwa hao wako nje kwa dhamana baada ya kila mmoja wao kusaini bondi ya Sh 5 milioni pamoja na wadhamini wao wawili kwa kila mmoja.

Comments




0 #3 josephjoel 2011-03-09 15:28 Bwana Jerry Muro,usifanyie masihara hiyo kesi ni kitanzi kwako.Ingia magotin kwa mungu umwite atakuitikia.
Quote









0 #2 josephjoel 2011-03-09 15:23 Bw.Jerry hiyo kesi usifanyie masihara itakupoteza.Inabidi uombe sana mungu akusaidie uepuke na kesi hiyo.
Quote









0 #1 mekaki 2011-03-09 13:25 sheria ichukue mkondo wake ili iwe fundisho kwa watangazaji wengine
Quote
 
uyu jamaa akienda jela miaka kama kumi hivi itakuwa safi, ili kiburi chake kikaishie hukohuko, watu wasio na maadili kama jeri muro hatuwataki hapa tz...alikuwa anawang'ang'ania wenzie kumbe yeye naye ni mbaya..unafiki huu. haponi huyu lazima akashike debe.
 
Uamuzi huo wa kustua ulitolewa jana na Hakimu Mkazi Gabriel Mirumbe ikiwa ni muda mfupi baada ya shahidi wa sita wa upande wa Jamhuri, D/C Koplo Lugano Mwampeta kumaliza kutoa ushahidi wake na Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka nchini, Stanslaus Boniface kueleza kuwa wamefunga ushahidi.

Mhhh waandishi wengine bwaa eti uamuzi wa kushtua. huyu mwandishi ndhani hat mimi nazidi knowldge ya sheria. Au kaweka taaluma pembeni na anchomeka ushabiki.

Sasa huo uamuzi umeshtua nani? afanye reseacrh kwa wanasheria mbali mabli wasiohusika na kesi n wasio na ushabiki ndo utaju ukweli. SImply Jery alizidisha na alijisahau.
 
Back
Top Bottom