Kuwa na dhamana ya maisha ya watu ni pamoja na kuwajibika zaidi hata dhidi ya ujinga wao.
Babu wa Loliondo angekuwa hai Kenya lakini si Tanzania.
Heko rais Kenyatta kwa maana heri lawama kuliko fedheha. Kenya kwa mtumishi wa umma, chanjo ni lazima.
Pole pole tutafika tu.
Kwanza Janssen zenyewe zimekuja 1m peke yake.
----
Nairobi: Serikali ya Kenya imetoa siku 13 kwa watumishi wote wa umma nchini humo kuhakikisha wanapata chanjo dhidi ya virusi vya corona na kwamba watakaokiuka agizo hilo hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yao.
Taarifa iliyotolewa na mkuu wa utumishi wa umma nchini humo imesema agizo hilo limetokana na idadi ndogo ya watumishi waliopata chanjo hasa waalimu na wale walio katika sekta ya usalama.
“Baadhi ya watumishi wa mma wamekwepa chanjo hiyo kwa makusudi ili wasihudhurie kazini hatua ambayo imezorotesha utoaji wa huduma,” amesema.
Hadi kufikia jana Jumatatu Agosti 9, 2021 Kenya iliripoti maambukizi mapya 745 na kufanya idadi ya maambukizi iliyothibitshwa nchini humo kufikia 212,573 tangu kuanza kwa janga hilo.
Wiki iliyopita serikali ilisema imetoa chanjo milioni 1.7 ya AstraZeneca, nyingi kati ya hizo ni dozi ya kwanza.
Kenya inalenga kuchanja watu milioni 10 mwishoni mwa mwaka huu.
Chanzo: Mwananchi

Summary
- Serikali ya Kenya imetoa siku 13 kwa watumishi wote wa umma kuchanjwa dhidi ya maambukizi ya corona.