ZeMarcopolo
Platinum Member
- May 11, 2008
- 14,019
- 7,223
Baada ya Mbowe kusema mbele ya watanzania kuwa Zitto Kabwe ni mnafiki, itakuwa ni unafiki zaidi kwa Mbowe kuendelea kufanya kazi na Zitto kama Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni.
Hii ni sawa na siku Kikwete akisema hadharani kuwa Pinda ni mnafiki na kumvua vyeo vyote vya CCM lakini akamuacha kuwa Waziri Mkuu. Jambo hilo haliwezekani!
Kwa mantiki hii, iwapo hotuba ya Zitto ya leo haitatangaza kujiuzuru unaibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Mbowe atalazimika kuvunja Baraza kivuli la Mawaziri na kuliunda upya. Asipofanya hivyo atakuwa ni mnafiki mara dufu.
Wakati huohuo, kwa kutumia busara, ingawa sheria hailazimishi, Mbowe au Dr. Slaa anawajibika kumpa Spika taarifa rasmi ya maandishi kuhusu Zitto kuvuliwa uongozi Chadema, Spika wa Bunge baada ya kupata taarifa hiyo anawajibika kumuuliza KUB kwa maandishi iwapo anaridhika na Zitto kuendelea na uenyekiti wa PAC.
Busara inataka hivyo kwa sababu Zitto amepewa uenyekiti wa PAC kutoka upinzani, anawakilisha upinzani. Kwa vile upinzani unamuona Zitto msaliti, Spika akikaa kimya tu ataingizwa kwenye lawama ya kuingiza wasaliti kwenye nafasi za wapinzani. Lakini ili hata yote yatokee ni LAZIMA Mbowe au Dr. Slaa amuandikie barua rasmi Spika kumjulisha msimamo wa Chadema juu ya Zitto.
Iwapo KUB atasema haridhishwi na Zitto kuongoza PAC, basi Spika atawajibika "kumshauri" ajiuzuru nafasi hiyo.
Kama tuko seriuos na utawala bora, hivi ndivyo tunavyotakiwa kufanya...