TANZIA Kamanda wa Polisi ACP Jonathan Shana afariki Dunia

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,240
4,768
Ni huzuni & majonzi

Ameumaliza mwendo

Kazi ya Mungu Haina makosa

Mshiriki, Mzee wa Kanisa na Muinjilisti wa Kanisa la Waadventista Wasabato Mjini Kati Arusha

Alishiriki vema akitoa Zaka na Sadaka

Aliishi vizuri sana na washiriki Wenzake

Alikuwa Mnyenyekevu na mwenye hofu ya Mungu

Aliongoza kwa mafanilio makubwa harambe ya ujenzi wa nyumba ya Mchungaji wa Kanisa la Waadventista Wasabato Mjini Kati Arusha
RIP Kamanda Shana
=====

TANZIA: KAMANDA JONATHAN SHANA AFARIKI DUNIA

Aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Jonathan Shana amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu

Alifahamika zaidi katika kujihusisha na shughuli za Vyama akiwa na sare za kipolisi. Aidha, aliwahi kufananisha Chama Tawala, Serikali na Dola kwa Kanuni za Kihesabu

Kamanda Shana aliwahi kuwa RCO Mikoa Mbalimbali Nchini ikiwemoRPC-Mikoa ya Pwani, Mwanza na Arusha pia aliwahi kuwa Mkuu wa Upelelezi Simiyu.

ACP Jonathan Shana amefariki akiwa Afisa Mnadhimu katika Chuo cha Polisi (CCP) Moshi


Updates: RATIBA YA USAFIRISHAJI WA MWILI NA MAZISHI

Taarifa.

Mwili utachukuliwa Muhimbili Mortuary siku ya Alhamis 17 September 2020 na kupelekwa kilwa Road kwa ajili ya kuagwa.
Baada ya utapekekwa kwa Dr. Musika Mbweni na kulala uko.

Siku ya Ijumaa wataanza safari kuelekea Ikizu Bunda watafika Dodoma majira ya Mchana saa Saba na utafikia nyumbani kwake watakaa kwa Nusu saa yaani saa 7:30 Mchana wataondoka nyumbani kwake Dodoma Ipagala kuelekea Kanisani Dodoma Kati watafika saa 8:00 Mchana. Kanisani kutakuwa na Chakula kwa Wageni na waombolezaji ; itafanyika Ibada fupi; Salamu za Kijeshi na kuaga mwili watu Wote.

Saa Kumi na Moja Jioni wataanza safari kutoka Dodoma Baada ya mapumziko kwenda Kijijini Ikizu mission . Wanatarajia kufika Bunda Asubuhi na watashinda Kwa Mama yake pale CCM Bunda Mjini na Jioni siku hiyo ya Jumamosi wataondoka na kwenda Ikizu Mission kwa Mzee Samwel Musika Waryoba Kaka yake na Marehemu Baba yake aliye mlea Shana.

Asubuhi Jumapili mwili utaondoka kwa Mzee Samwel kwenda kwa Kaka yake Shana Bukama Ikizu Mission ( Ikizu Secondary).

MAZISHI YA MPENDWA WETU SHANA NI JUMAPILI

1600232588386.png



FB_IMG_16002275367369033.jpg


Pia soma >>> RPC Shana anavyotikisha Arusha, awadaka Majangili hatari, AK 45, Meno ya Tembo

Watu 9 waliohusika kutungua chopa na kumuua rubani wakamatwa
 
View attachment 1571069
Pumzika kwa Aman kamanda shana
Msiba wake umetokea Leo saa 11 alfajir.
Amefanya nini zaidi ya kuwa polisi kada wa chama cha mapinduzi? Na yeye kupitia nafasi yake amekuwa akiunyanyasa upinzani. Ametumika vibaya kisiasa,pia amesababisha niichukie kada yote ya polisi. Naombeni mnisamehe kama nimewakwanza.
R.I.P kamanda kada w CCM
 
Huyu ndiyo yule aliefanya jeshi letu la polisi kuwa la ccm na kuvunja katiba yetu kwamba polisi ni kwa kila raia wa Tanzania?

Kwamba if A = B and B = C then A = C nakwamba akatamatisha kuwa hakuna tofauti kati ya ccm na polisi.

Ali manipulates Logics kishabiki sana nakufedhehesha elimu ya hesabu

Au siyo yeye ?
 
Back
Top Bottom