KERO Kaliua, Tabora: Huduma za Afya kituo za Ulyankulu zina walakini mkubwa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Nimempeleka mke wangu Kwa ajili ya kujifungua katika kutuo cha AFYA cha serikali Ulyankulu. Na ikahitajika kufanyiwa upasuaji ila cha ajabu gharama nilizopewa nilishangaa sana. Huduma ilisuasua hadi pale nilipotoa pesa waliyohitaji.

Nilijaribu kukutana na Daktari na kumuuliza kwanini fedha na najua huduma ya upasuaji Kwa Kuna mama wajawazito Ni bure alinijibu kuwa serikali haitoi dawa WALA fedha za kutosha kuendesha kutuo so lazima kulipia Kama sitaki wanipe rufaa na mgonjwa wangu.

1. Je kwanini serikali inafumbia Jambo hili macho?

2. Kama serikali inasema huduma Ni bure na tunatozwa pesa kwanini watu Hawa wasichukuliwe hatua

3. Kumekuwa na changamoto ya dawa. Dawa muhimu zote zinazoletwa na serikali Kwa ajili ya watoto na wajawazito zinauzwa katika maduka ya dawa
 
Mbona lodge ulilipia room mkuu.........malizia tu mchakato tupate anko wetu aje salama.........
 
Mbona lodge ulilipia room mkuu.........malizia tu mchakato tupate anko wetu aje salama.........
Mkuu Bora ulipie huduma ikiwa unaona hata mazingira Ni rafiki. Sio unalipa unakuta bado changamoto Ni nyingi mfano vyoo na bafu Hakuna Mtu anajifungua then anaoga na kujisaidia polini. Ona hapa
 
Back
Top Bottom