Kafulila: Tunatekeleza agizo la Waziri Mchengerwa ndani ya muda mfupi ujao DART itasaini mkataba na Mbia nia ni kupunguza gharama Kwa wananchi

Mwananchi Huru

JF-Expert Member
Nov 20, 2021
1,555
1,153

Kufuatia agizo lililotolewa na Serikali kupitia kwa Waziri wa TAMISEMI nchini Mhe Mohamed Omary Mchengerwa,

Agizo hilo limeitaka DART kuhakikisha inakamilisha taratibu zote za Ubia na Mbia wa UDART ndani ya miezi Saba.

Mkurugenzi wa Ubia nchini PPP Bwana David Kafulila amesema ndani ya muda mfupi ujao watakuwa tayari wamekamilisha mkataba baina ya DART na Mbia ili kuhakikisha Wananchi wa Dar es Salaam hawapati adha ya usafiri na Usafirishaji.

Kafulila amesema, Mbia huyo wa UDART atanunua Mabasi yeye mwenyewe na atayaendesha kwa Ubia na Serikali katika kipindi Cha mkataba na hivyo kuifanya gharama ya usafiri kuwa nafuu Kwa wananchi na wakazi wa Jiji la Dar es salaam.

Kafulila amesema kuwa 40% tu ya wafanyakazi waishio Dar es salaam ndio wanakwenda kazini kwa miguu ( working distance).

Hivyo zaidi 60% wanafanya kazi sehemu ambazo wanalazimika kulipa nauli kila siku ili kwenda kazini na kurudi nyumbani.

Nia ya Serikali ikiwa ni kutoa unafuu wa gharama za Usafiri na usafirishaji Kwa Wananchi hasa wakazi wa Jiji la Dar es salaam.

 
Halafu tunatupa huko hizo basi tufunga Trams

1715703013199.png
 
Tumbili ...snich
Tumbili ...snich
How ?

au kwakuwa simu yako inabando tu?

Kila anayezungumzia uwekezaji ni mwizi?😡😡

#Trust the Process chini ya Kafulila.

 
Mmmh,porojo na usanii tu,hakuna lolote..ni hadi mkiri kwamba Mradi huo wa DART uliundwa katika UBATILI...

Mngekuwa hamna kulindana lindana kama kawaida yenu,wengi wangekuwa Mahabusu na si Kisena pekee
Kisena ni inshu ya mahakama Sasa mkuu.
 
Mzee wa Kaliua Le Profesa n Marehemu Iddi Simba..ila wao wanawafahamu wengi zaidi kwa kuwa wana vyombo vya Uchunguzi@ Mwananchi huru
 
Bora angebaki kwenye porojo zake za kumpamba ‘bi tozo’ siasa ndio kitu anaweza.

Huku kwenye kutetea miradi ya PPP bila kufahamu details za mikataba yenyewe ipo siku hizo porojo zake zitamtokea puani.

Anatetea miradi ambayo yeye mwenyewe ukimuuliza mfano TANESCO wanauwezo wa kununua huo umeme wa wind kwa guarantee ya miaka 20 kwa bei wanayopewa sidhani kama anaweza jibu. Wakati shirika juzi tu limepeleka madeni serikalini lipate nafasi ya kupumua chanzo cha kikubwa cha madeni yenyewe ya kuuziwa umeme na wazalishaji wengine.

Barabara bado kutakuwa na option ya njia ya kawaida iliyopo sasa, au unaondoa hiyo option na kulazimisha watu wote watumie toll road maana huu sasa ni uporaji kama mwisho wa siku ni lazima kupita toll road.

Hayo mabasi ana guarantee gani bei itakuwa nafuu wakati ajaona business plan wala mkataba wenyewe.

Mambo mengine ajiwekee mipaka na kutunza maneno; sio kukomalia kutetea mambo ambayo wewe mwenyewe huna final nitty gritty details za mikataba.

Ubia sehemu zingine ni muhimu hasa kwenye public transport especially kama business partner ana experience ya kutosha, lakini kutetea vitu ambavyo ujaviona kimkataba huko ni kujikaanga kwa mafuta yako huko mbele mambo yakienda mrama. Sio kila kitu siasa.
 
Bora angebaki kwenye porojo zake za kumpamba ‘bi tozo’ siasa ndio kitu anaweza.

aviona kimkataba huko ni kujikaanga kwa mafuta yako huko mbele mambo yakienda mrama. Sio kila kitu siasa.
Mkuu anaachaje kutetea wakati yeye pia ni inclusive?

Ushauri unaoweza kumpatia Kafulila ni kuwa critical kwenye hiyo mikataba isije ikamaliza integrity yake kidogo aliyobakiwa nayo toka enzi za Escrow.

I submit ,
 
Back
Top Bottom