#COVID19 Jukwaa la Wahariri lawapa Tuzo Waandishi wa Habari za Watoto na walioripoti UVIKO-19

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,876
12,129
Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limetangaza kampeni ya kutoa elimu kwa waandishi ya namna ya kuhamasisha jamii kutoa maoni yao kupinga ndoa za utotoni.

40efa5f9-441b-4b84-bd22-edaf40b281be.jpg
Akizungumza katika hafla ya kutoa Tuzo kwa Waandishi wa habari za Watoto, pamoja na mambo mengine Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile amesema “Tutashiriki kikamilifu kupinga ndoa za utotoni kwa ajili ya kuhakikisha Watoto wanatimiza ndoto na malengo yao.”

Akilishukuru Shirika la Maendeleo la Kusaidia Watoto (UNICEF), Balile amesema kabla ya mradi huo wa habari za Watoto kuanza kuendeshwa nchini msamiati wa udumavu haukuwa ukifahamika sana katika nchi yetu.

Amesema: “Tunawashukuru Wahariri kwa kuwafahamisha Wananchi mambo kama haya. Lakini tunawashukuru waandishi wa habari kwa kutumia gharama, muda wetu katika kuitafuta habari hizi za watoto, gharama mnazozitumia ni kubwa kuliko kiwango cha zawadi mnazotunukiwa leo. Niwaombe UNICEF ushirikiano huu uliozaa matunda msituache.

"Kipekee namshukuru Neville Meena kwa kusimamia mradi huu bila kukata tamaa.”

7d0c4d00-e9ad-47c1-b66f-54aa97f278de.jpg
Akizungumza katika hafla hiyo Guru la uandishi wa habari, Salim Said Salim amesema lengo la hafla hiyo ya kutoa Tuzo ni kuhamasisha maendeleo katika kuandika habari za Watoto.

Ushindani huu tulioukusudia katika uandishi ni kushawishi waandishi wa habari ni kuleta mabadiliko katika jamii kuhusu malezi ya Watoto. Ombi langu kwa wanajamii ni moja kama tunazaa basi tuwalee Watoto, tuwahudumie, tuwatunze na tuwalinde.

Naye, Jesse Kwayu, Mjumbe Kamati ya Mradi wa Habari za Watoto amesema kazi ya kuwa na habari za Watoto ni kuwapa kipaumbele waweze kusikika.

9cc22338-b219-4def-9ecf-e003be0151a9.jpg
Amesema "Kumekuwa na kazi nzuri zimefanyika habari 76 zimeandikwa na kutangazwa, ni mafanikio makubwa pamoja na mafanikio haya yako mambo ya kuangalia tangu Mwaka 2017 na leo tunaingia 2023 kuna impact gani.”

Ameongeza kuwa kuna umuhimu wa kuweka msisitizo katika kuhamasisha umma kutoa maoni yao kupinga sheria inayoruhusu ndoa za utotoni.

"Kutoka hapa tunafanya nini katika sheria ya ndoa, Je, waandishi kwa ujumla wetu tunaifahamu hii Sheria ya Ndoa ya 1971? Lengo tujikiite kufanya kampeni ili iweze kufanyiwa mabadiliko, lengo mtoto aliye chini ya umri wa miaka 18 aweze kutimiza malengo na si kuolewa katika umri mdogo ambao ni chini ya miaka 18,” anasema Kwayu.

Akizungumza katika hafla hiyo ambayo waandishi mbalimbali walipata Tuzo, Naibu Muwakilishi wa UNICEF, Ousmane Niana amepongeza TEF kwa kufanikisha hafla hiyo pamoja na kupongeza mapambano ya kuandika habari za Watoto na kupunguza hali ya utapiamlo nchini.

"Tanzania ihamasishe kuzuia Watoto kuolewa wakiwa na umri mdogo ili waweze kusoma na kufikia ndoto zao,” anasema Niana.

Miongoni mwa waliotunukiwa katika hafla hiyo ambapo pia kulikuwa na kipengele cha Kuripoti Vizuri Taarifa za UVIKO -19 kwenye vipindi vya redio, ni Aidan Mhando (Channel Ten) Simiyu, Faraja Masinde (Mtanzania Digital), Anod Kalembo, (Kagera) na Stansilaus Lambart (Dar 24 Media).

35019156-abae-4631-8bc5-064e8b01d0e5.jpg
 
Back
Top Bottom