Jokate Mwegelo: Mpaka sasa Raia Samia hajakosea chochote, tukatae wote wanaotaka kumdhoofisha

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,906
10,390
Tukatae watu wanaotaka kumdhoofisha mwenyekiti wetu (Wa Chama Cha Mapinduzi Taifa) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Ameongeza kuwa kwa mara ya kwanza Tanzania imefiwa na Rais akiwa madarakani, ingeikuwa nchi nyingine basi pangechimbika, lakini kwa Tanzania chini ya Rais Samia

Anadhoofika kwani anapambana na nani!!?nani namdhoofisha!!?Mbona mnamfanya mwenyekiti apigane na hewa!!?

Mmeshasema kuwa mtachapisha fomu Moja tukakubali Sasa anadhoofishwa na nani!!?

Yale Yale ya marehem jpm ;Tume ya uchaguzi yake,Dola kaishika tayari,lakini alisikika akisema hivi kwenye kampeni:-"mwinyi mlimpa awamu mbili,mkapa awamu mbili!kikwete awamu mbili!!,kwanini mimi mnataka kunipa awamu moja!!?

Ikawa kweli akalazimisha awamu ya pili hakuimaliza coz alibishana na asili!!

Muulizeni mwenyekiti kwamba akiyatazama majani,mchanga,mawe,hewa,Jua,mwezi n.k anaona awamu mbili au moja!!?

Kama anaona awamu mbili basi akae kimya hakuna haja ya makelele tote haya toka kwa wapambe,kama anaona moja mwambieni arudi nyumbani akalee wajukuu!!
 
Tuna sababu zote za kumsemea Rais Samia kwasababu kazi zake zinaonekana ametugusa kila nyanja, Rais ambaye mpaka sasa hajakosea chochote, kwa lugha ya vijana tunasema mama hana baya.

Tukatae watu wanaotaka kumdhoofisha mwenyekiti wetu (Wa Chama Cha Mapinduzi Taifa) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Kuweza tu kusimamia nchi ilipopitia magumu kwa mara ya kwanza tulipoondokewa na rais akiwa madarakani, ingeikuwa nchi nyingine basi pangechimbika, vita ingelipuka lakini kwa Tanzania chini ya Rais Samia amani imetawala na maisha yanaendelea.

View attachment 2977298
masikini huyo dogo anafikiri siasa ni ngonjera
 
J

Jokate, umeokotwa kutoka kwenye kukaa uchi kwenye stage, leo lazima utamwabudu yeyote aliyekuokoa na kudanga kwenye stage!
 
Siasa haimpendezi kabisaa huyu Kipenzi changu,,havutii kabisa hapendezi kuwa mnafki nafki na muongo muongo,,Hafananii na Siasa kabisa huyu Binti!!
 
Siasa haimpendezi kabisaa huyu Kipenzi changu,,havutii kabisa hapendezi kuwa mnafki nafki na muongo muongo,,Hafananii na Siasa kabisa huyu Binti!!
Ameungana Na Wakina Makala, Sophia Mjema Yaani Hawana Mvuto Kama Futari Ya Magimbi
 
Anakuwa kisiasa god bless her mungu amfikishe mbali. Na speech zake sasa hivi zinaelekea kukuwa sio yale mambo yake ya viva (nonsense).

Anaponichefua mimi wakati kana angaika kama mlupo wa kina ICE Prince, Ali Kiba na Diamond na kuuza vibegi vya wachina.

Ni mimi ndio nilikuwa nampigania hapa kusema kanatosha kwenye uongozi (kana mvuto kwa watoto) wakati hakana mwelekeo wowote wa maisha nikijua JK ananisoma ampe nafasi, kakateuliwa chipukuzi CCM.

Kako hapo kwa sababu ya JF kukipigania halafu kanata kutuletea uthenge wakati kuna watu walikipania hadi kufika hapo kilipo ndio kinaponikera.
 
Tukatae watu wanaotaka kumdhoofisha mwenyekiti wetu (Wa Chama Cha Mapinduzi Taifa) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Ameongeza kuwa kwa mara ya kwanza Tanzania imefiwa na Rais akiwa madarakani, ingeikuwa nchi nyingine basi pangechimbika, lakini kwa Tanzania chini ya Rais Samia

Hawa kama wana akili wakae kimya tu kuhusu mada za mama samia wajikite kueleza mambo yenye tija, hii yabkukaa muda wote mnaongelea mama sijui kafanywaje sijui wamemsemeje ndio inazidi kufaya watu wahisi kuna mahali ana pwaya maana utetezi wa kujihami unaonekana kuwa unakuwa mwingi sana
 
Tunapangiana ?

Baada ya utetezi na utumishi kwa wananchi watu wanatumika kwa Mtawala..., Hawa ndio wa kuwakataa....
 
Hao wanaomzofisha ni kutoka kundi alilosema nduguye Sila au wepi tena!! Inawezekana wanatafutwa lakini watafutaji hawajui wawatafutie msitu gani.
 
Ameongeza kuwa kwa mara ya kwanza Tanzania imefiwa na Rais akiwa madarakani, ingeikuwa nchi nyingine basi pangechimbika, lakini kwa Tanzania chini ya Rais Samia
Hivi Hawa ccm huwa hawafikiri hata kidogo kabla waongee! Tanzania sio nchi ya kwanza kufiwa na rais aliyeko madarakani: Kenya (Kenyatta), Ghana (John A. Mills), Malawi (Bingu wa Mutharika), Zambia (Michael Sata na Levvy Mwanawasa), Chad, Ethiopia, Nigeria (Umaru M. Yaradua), Guinea etc.
Ccm wanawapa watu popular nafasi bila kujali popularity imetokana na kufanya jambo la maana au la ovyo. Mfano mwingine ni daudi Albert bashite- ni popular sana, lakini ni mtu wa ovyo kabisa.
 
Kuna wakati nawaona kama wanachama wengi wa CCM wako brainwashed hatari! Wanaongea bila kutumia akili!
Marehemu Mzee wangu aliwahi kunipa wosia kuwa "Njaa ni mbaya sana! Unaweza kukutana na Simba Serengeti ukawapa moyo watu kuwa ni Papa Sauna wa Tandale"
Njaa mbaya wakuu! Hapa anatafuta apate uteuzi kwenye mkeka wa bi mkubwa!
 
Tukatae watu wanaotaka kumdhoofisha mwenyekiti wetu (Wa Chama Cha Mapinduzi Taifa) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Ameongeza kuwa kwa mara ya kwanza Tanzania imefiwa na Rais akiwa madarakani, ingeikuwa nchi nyingine basi pangechimbika, lakini kwa Tanzania chini ya Rais Samia

Ngoja tuone kwenye Mei Mosi ameandaa "pekeji" ya aina gani safari hii.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom