#COVID19 Jinsi wasafiri na wasafirishaji wanavyoweza kuepuka kupata maambukizi ya COVID19

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
633
962
Ugonjwa wa COVID-19 ni ugonjwa wa kuambukiza unaosababishwa na Virusi vya Corona vilivyogunduliwa Mwaka 2019. Virusi vinavyosababisha COVID19 husambazwa haswa kupitia vitone vinavyotokana na kukohoa, kupiga chafya au kushusha pumzi kwa mtu aliyeambukizwa.

Unaweza kuambukizwa ukivuta pumzi yenye virusi hivi ikiwa uko karibu na mtu aliye na COVID-19, au kwa kugusa sehemu iliyoambukizwa kisha ujiguse macho, pua au kinywa.

Wasafiri na Wasafirishaji, wapo katika hatari kubwa ya kupata Corona kutoka na muda mwingi wanakutana na watu tofauti.

SEHEMU HATARISHI KWA WASAFIRI NA WASAFIRISHAJI.

A. Wasafiri
Wasafiri wanaweza kupata virusi vya Corona kama:
i) Atakaa kiti kimoja na mtu aliyeambukizwa na akamkoholea au kupiga chafya na matone ya maji yakamfikia.
ii) Kama atachangamana na watu sehemu yenye mkusanyiko wa watu hasa wakati wa kusubiri Usafiri
iii) Atapanda gari iliyojaza sana abiria, ni hatari kwani kuna uwezekano mkubwa wa kupata Maambukizi
iv) Kama atagusa sehemu iliyoguswa na mtu mwenye maambukizi. Sehemu hizo ni kama;

● Egemeo la kujishikilia wakati wa kupanda na Kushuka kwenye basi au daladala.

● Vishikio vya kujishikilia hasa kwenye daladala na Mabasi ya mwendo kasi. Magari mengine wanaweka bomba la kujishikilia wakati ukiwa umekosa siti na kulazimika kusimama ndani ya gari, wengine wanaweka vishikio vya plastiki hata kwa mtu aliyepata siti.

● Vitufe vya kubonyeza. Mfano kwenye daladala kuna vitufe vya kubonyeza ili gari isimame, kwenye basi kuna vitufe vya kubonyeza au kuzungusha ili kuongeza au kupunguza Kiyoyozi. Kuna vitufe vya kufunga na kufungua Madirisha.

v) Kugusa Tiketi au risiti ya Malipo ambayo imeguswa na Mtu aliyeambukizwa.
vi) Kugusana na mtu ambaye ana maambukizi.
vii) Kununua vyakula na mapochopocho ya kula safarini au ndani ya gari
viii) Kuazimana Magazeti ya kusoma ndani ya gari.
ix) Kujigusa Usoni, puani machoni na Mdomoni
x) Kuvua Viatu ndani ya basi au daladala
xi) Kuwa na safari za mara kwa mara zisizo za lazima. nk

B. Wasafirishaji

Wasafirishaji wa Mizigo na abiria, sehemu hatarishi kwao ni pamoja na;
i) Sehemu za kupakilia Mizigo na Abiria
ii) Sehemu ya ukaguzi kama Uhamiaji, TRA, TFDA
iii) Sehemu ya kubadilishia fedha hasa mipakani.
iv) Wakati wa kusubiri Kuvuka Mpakani(Kunakuwa na msongamano wa watu)
v) Sehemu ya kupata vyakula na vinywaji wakati wa Safari
vi) Sehemu ya Malazi wakati wa Safari
vii) Kupakia abiria wa njiani ili kujiongezea Kipato(Madereva wa Malori na Wasafirishaji wa Magari ya IT)
viii) Kusimama mara kwa mara kwenye vituo visivyo rasmi
ix) Kubadilisha Dereva njiani(day worker) n.k.

NINI KIFANYIKE ILI KUPUNGUZA UWEZEKANO WA KUAMBUKIZWA?

Ili kujiepusha kuambukizwa, jiepushe na jihadhari na vitendo vinavyoweza kukufanya ukaambukizwa na kuzingatia miongozo ya Wataalam wa afya pamoja na;
i) Kunawa mikono Mara kwa mara na kutumia Vitakasa mikono( sanitizer)
ii) Jihadhari kukaa kwenye makundi ya watu wengi(Kaa umbali wa mita mbili kutoka mtu na mtu)
iii) Msafiri epuka kupanda gari ambayo imejaza abiria.
iv) Epuka kugusa uso, macho, mdomo na pua
v) Tumia Malipo ya mtandaoni kufanya malipo
vi) Usikae muda mrefu sehemu za kutolea huduma kama TRA, Uhamiaji TFDA n.k
vii) Msafirishaji, epuka kusimama vituo visivyo rasmi na kushuka mara kwa mara uwapo safarini.
viii) Wasafirishaji wa masafa marefu wanashauriwa kubeba vyakula na kujipikia wawapo safarini
ix) Wasafirishaji, epuka kubeba abiria kwenye Malori na magari ambayo hayajasajiliwa kubeba abiria
x) Pendelea kula matunda ya kuongeza Vitamin C kama Limao, Machungwa, Nanasi na Tangawizi.
xi) Tumia barakoa unapokuwa sehemu yenye msongamano

Hadi sasa hakuna tiba au chanjo dhidi ya virusi vya Corona lakini kwa sababu virusi hivyo vinaleta dalili mfano wa zile za mafua makali, mchanganyiko wa tiba unatumika kupunguza athari za virusi vya Corona.
 
Asante sana kwa andiko hili murua, nimepata kitu. Naona limefafanua vyema nyanja nyingi za Wasafiri (Wasafiri na Wasafirishaji). Nachoweza kuongezea kidogo tu katika hili, nadhani ni muhimu kwa wasafiri kuwa na Sanitizer vitakasa mikono binafsi hata chupa ndogo ili awapo kwenye siti au pahali pa kusafiria aweze kusafisha eneo analohisi anaweza kuligusa kwa urahisi.

Lakini pia nakazia tu kwenye barakoa hapo, ni muhimu wasafiri wavae barakoa ili kujiepusha na vitone tone vya mate vinavyotokana na watu kukohoa au kupiga chafya.

Wakati mwingine ni ngumu sana kufata miongozo hii kwa tuliowengi lakini kwa usalama wa afya zetu ni muhimu sana tuizingatie.
 
Asante sana kwa ushauri huu mzuri, binafsi nitafuata kanuni hizi ili nibaki salama nikiwa kwenye vyobo vya usafiri.

Tuendelee kuchukua tahadhari.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom