Jinsi Bamia lilivyoniponyesha vidonda vya tumbo

HSE Officer

JF-Expert Member
Apr 10, 2023
661
853
Habar wana Jf

Leo nimekuja kutoa ushuhuda jinsi nilivyopona vidonda vya tumbo kwa kutumia bamia narudia mara 2 ni kiboko ya vidonda vya tumbo.

Nimeteseka kwa muda sana nimetumia dose za gharama lakini sikufanikiwa kupona mpaka nikahisi narogwa nikaenda mpaka kienyeji sikupona nimekuja kuponea kitu ambacho sikuwahi hata kuwaza ambacho ni bamia.

Kitu cha kufanya chukua bamia osha weka pale then chemsha maji yapoze yawe ya vuguvugu then katakana vibamia vidogodgo weka kwenye kikombe cha nusu lita cha maji ambayo umeyapoza anza kupondaponda hizo bamia ili upate mlenda mzito sana ikiwezekana fikicha hata na mkono ili uwe mzito sana then chuja anza kunywa huo mlenda wa bamia mara 3 kwa siku ndani ya sku 7 ukimaliza hizo pumzika,
let say baada ya siku nne hivi unatengeneza tena kama nilivyo elezea juu unapona kabisa mpaka utajishangaa kama ni wewe ambaye ulisumbuka sana na vidonda vya tumbo.

Sent from my SM-A115F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom