Jifunze Jinsi ya kufanya Manunuzi kwa Ebay mtandaoni

Mkuu NingaR ni rahisi kujaribu mm nilianza na kitu cha bei chee nione ka ntatozwa ushuru na kama kitafika
Kilifika bila shida nakilinifikia mm maana,kilikuja,na jina langu na mm nkawaonesha ID yangu wakanipa
 
Last edited by a moderator:
Mkuu, ni vizuri ungetupa darasa kidogo process nzima maana watu wengi ni wageni na masuala haya ya e-commerce

mkuu ingekuwa poa mka toa somo vizuri kwa sababu watu wengi wana penda wa fahamu..msaada mkuu
wakuu ni bora mfungue uzi mpya ili mtueleze kwa kiref kuhusu ebay na paypal


Wakuu ebay ni sehemu ambayo wauzaji(Seller) na wanunuaji(Buyer) wanakutana
Muuzaji(Seller) anajiunga kwa kufungua Account ebay na kisha anatangaza kitu anachokiuza akiwa popote pale Duniani
Mnunuzi(Buyer) anajiunga kwa kufungua Account ebay popote alipo Duniani kisha anachagua bidhaa nayoitaka iliyotangazwa na Muuzaji(Seller) ana inunua online.

Ili kukamilisha zoezi la malipo na kuuziana bila kuibiana ndio sasa anaingia Pay pal
Pay Pal ni njia ya malipo ambapo mtu yeyote anajiunga ili mradi awe ni mteja wa Bank inayotoa Card za Master au Visa Card
Kibongo Bongo CRDB wapo vizuri, baada ya kufungua Acc na kupewa Master/Visa Card yako unarudi tena CRDB kuomba wai link Master/Visa Card yako iweze kufanya online Transaction kwa kujaza form maalumu then you're done

Baada ya kadi yako kuwa Linked unajiunga kwa kufungua Acc Pay Pal kwa maana ya kwamba unawapa details za Account yako na kuwapa ruhusa kutoa pesa kwenye account unapo waomba kufanya hivyo

Jinsi ebay na Pay Pal wanavyofanya kukamilisha mpango mzima
ebay ni kama soko ambalo watu hawaonani, mmoja yupo Hong Kong anauza iphone mwaingine Yupo Manzese Tz anataka kuinunua lakini wanakuta online through ebay. so huwezi ukamtumia tu mtu hela kwenye acc ya bank maana anaweza kuingia mitini na asiwepo wa kufuatilia
Sasa wanapotaka kulipana Pay Pal anaingia katikati kama bima wa malipo kwa kuhakikisha anamjua vyema Muuzaji(Seller) ambaye ndio mlipwaji

Mlipaji aka Mnunuzi(Buyer) aliyeko Manzese hamlipi direct mlipwaji aka Muuzaji(Seller) aliyeko Hong Kong,
Anachofanya Mnunuzi(Buyer) anampa ruhusa Pay Pal atoe pesa kwenye Acc yake ya bank kutumia Master/Visa kisha amlipe Muuzaji(Seller)
Kwakuwa Pay Pal anakuwa amechukua dhamana ya malipo ya mauziano yenu anawajibika kuhakikisha Muuzaji(Seller) ana bidhaa kweli anayouza na anaaminika atatuma kwa Mnunuzi(Buyer) kile alicho tangaza,....Fail to do so basi Pay Pal atawajibika kumrudishia Mnunuzi(Buyer) pesa yake, na baada ya hapo Pay Pal kushirikiana na ebay ndio watao mtafuta na kumbana Muuzaji(Seller) kwa utapeli alioufanya lakini wewe utakuwa tayari umerudishiwa pesa yako iwapo watajiridhisha kuna uvunjifu wa makubaliano.

CHANGAMOTO

Mara chache sana inaweza kutoke Muuzaji(Seller) akawa tapeli maana ili uwe Muuzaji ni lazima lazima ebay na Pay Pal watataka kujirisha lakini changamoto ipo baada ya kurudishiwa pesa zako
Mifumo ya Pay Pal yetu wanasema hairuhusu kupokea Pesa maana mabank nasikia sijui hayajaingia mikataba gani I dont know, so kibongo bongo acc zetu za pay pal ni kwa kulipia tu na si kupokea pesa(wataalamu watatusaidia katika hili)

Jambo lingine ni wizi wa mizigo Posta, binafsi ni muhanga wa hili.
Mwaka juzi niliagiza BlackBerry yangu lakini ilipotelea Posta na sijaipata hadi leo, nilianza kumsumbua Buyer lakini alinithibitishi mzigo umetumwa na hadi tarehe ulipopekelewa Bongo, nilipo wabana Posta wakaanza kunizungusha tu.
Na hii ndio maana Buyer wengi hawatumi(ship) mizigo Africa maana Posta za kiafrica ni majanga kwa wizi na hasa ukituma vitu vidogodogo vya thamani ya kuonekana kama Simu kamera nk, mara nyingi wana iba

Kuna baadhi ya items ukiagiza utakutana na mkono wa TRA, hawa jamaa ni wasumbufu balaa ukiingia kwenye kumi nanane zao, watakutwanga makodi hadi uchanganyike au la sivyo ukate "kitu kidogo"

Hakikisha unaangalia Feed back na Reputation ya Muuzaji(Seller)
Hakikisha unasoma kwa makini na kuelewa discription ya item, ikiwezekana muulize Buyer kama hujaelewa.
Epuka kutumia njia zingine zaidi ya Pay Pal kama means ya malipo.Unaweza ku bid item alafu ukashangaa unapoke email ianakuambia ipo items kama hiyo kwa bei ndogo......usi jaribu

Shipping nayo ni topic ndefu kidogo natumai wapo wadau wataifafanua vizuri
 
C6 In case kama ungelipia shipping, cost ingekua around sh ngapi??
na kwa nini hakuna tax?

shipping inategemea ni wapi mzigo unatoka, mfano mzigo unaotoka marekani na mwingine unatoka hongkong bei itakuwa tofauti, au mzigo unakuja kwa meli au kwa ndege bei zinakuwa tofauti na uwa wanazitaja,

kama huna haraka na mzigo chagua free shipping
 
Me kuna Laptop nimeipnda saan na kuna bro wangu kajiunga na visa CRDB but umentsha kuibiwa vp ukienda exactly tme ambayo mzgo wako imefka bado utakumbana n majang and yale bidhaa znazoandkwa Worldwide c ndo ininclude na TZ?
 
Kumbuka kuwa CRDB wanapiga online transaction fee ya 22,000/=
uwe umefanya 1 au 100

Hakikisha email unayoitumia paypal usiitumie for other registration kama fb etc phinshing nyingi
Wala usi expose popote wajanja wengi
Maana mm juzi juzi njunwawamavoko@gmail ilikuwa hijacked na ilikuwa ndo ya Payza ivo hata Payza alisema forgot passwd na akatumiwa kwenye inbox na akafuta

Mwisho kabisa rejea uzi wangu unaaema "hivi eBay ni genuine market Place?"
Nilianzisha sababu niliona iPhone 5 inauzwa 14.99$ na Mac book 24.99$
vitu hivi nilivinunua na baada ya masaa nilipokea email inasema "items # so and so have been removed" if u arleady made payment go to resolution center

Item ilikuwa inauzwa na mchina na hakuwa na reputation hata moja

Nilifungua case moja eBay na nyingine PayPal, moja nilifungua paypal sababu item reseller hakui mark as paid

Fortunately nilipewa refund na unfortunately sikuwai kuiona kwenye bank statement na nilipotezea

ENJOY
 
Kumbuka kuwa CRDB wanapiga online transaction fee ya 22,000/=
uwe umefanya 1 au 100

ENJOY

Shukran kwa somo mkuu, unachomaanisha ni kwamba hiyo 22,000 ni flat rate kwa mwezi ama ni kwa kila transaction. Sijakupata vema hapo mkuu. Na kwa maelezo ya wadau humu, naona akaunti ya crdb inahitajika kwa urahisi wa paypal. Ngoja nijipange
 
Naona watu wengi sana wapo behind sanaa na maswala haya ya online shopping ila pole pole tu mtafahamu,sema hiyo ebay inabidi kuitofautisha maana mkisema ebay basi mtaje na ebay ya sehemu gani??maana Europe yote kila nchi ina ebay yake, Ebay ya UK na Ebay ya US ni tofauti kabisa au Ebay ya France ni tofauti so mkizungumzia Ebay ni vizuri ku point Ebay ipi mnazungumzia...

Mfano kuna mdau mmoja amesema kwamba kuna ebay akifungua akicheck laptop katika zile nchi haionyeshi nchi ya Tanzania kama wana ship,yes ni kweli kabisaa Ebay ya UK ukicheck 99% seller wake huwa hawa ship africa kwa sababu mizigo inafika bila tatizo Tanzania ila inaibiwa kwenye postal zetu,so inabidi kuweka mambo sawa kila mtu afahamu....kuna maswali mengi yameulizwa ila naamini yamejibiwa na mkuu @C6.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Papizo, kwa ushauri wako, ebay ipi ni nzuri kwa watanzania?

Kwa uzoefu wangu me naona Ebay nzuri ni ya UK na US hizo zingine kwanza kuna baadhi ya vitu vina limit na vikitumwa na kudundulika kama ni counterfeit itakula kwako mnunuaji,so kwa ujumla ni vizuri kufatilia hizo site 2 ndio mta enjoy ebay na sio zaidi,maana kwanza sio site zote wanatumia US so ukiingia kwenye site lazima utajuwa utofauti tu...

Ni vizuri kuwa makini zaidi maana kila nchi wana restrictions zao wenyewe so inabidi kufahamu hayo yote...

Zaidi i will be happy kutoa any kind of information ambazo mtahitaji kwa wale ambao hawajajuya zaidi namna ya kuitumia vile vile Ebay kwa africa ni 50/50 maana tatizo hizi postal zetu wanatulet down sanaaa....sio kila kitu mtanunua vitawafikia,ila zaidi Ebay ni the best kuliko amazon...

So kwa watanzania kama mnataka kununua vitu original na kuepukana na vitu fake ambavyo mtapata matatizo navyo vikigundulika ni fake,bora mtumie Ebay ya UK au US..

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Papizo, kuna mdau hapo mwanza alisema ametumia sanduku la posta(S.L.P), je hii njia ni nzuri kwa kuagiza vitu?
Vipi kuhusiana na kodi, ni vitu vyote wanakata kodi?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom